Je, wajua Wazaliwa wa Pwani huwaona wazaliwa wa Bara kama washamba tu?

Je, wajua Wazaliwa wa Pwani huwaona wazaliwa wa Bara kama washamba tu?

We're the smartest generation nyie someni sisi talents kibao tunajitambua hatuna ujinga sana someni sana maana despite na anavyokazana kusoma ila bado elimu haimisaidii[emoji28][emoji28][emoji28]zaidi ya kuajiriwa
[emoji23][emoji23][emoji23] Mna talent gani sasa? Ya kufunga kikoi au kupanda mnazi?
 
Basi hivo ndivo ilivo.

Wazaliwa wa mikoa ya pwani kihistoria wanawachukulia watu wa bara kama watu washamba tu walioukuta ustaarabu Pwani.

Kwa mfano ustaarabu wa mapishi, usafi hasa kuoga yaani hadi kuingia chooni na maji wabara inasemekana walikua hawajui maana walitumia udongo na magunzi kujitawazia.

Sasa basi mzaramo au mkwere ukijitambulisha umetoka chato au umetoka lamadi au umetoka mpitimbi akilini mwake anakuchukulia mshamba tu hata uwe umemzidi kila kitu lakini mentality yake inamweleza wewe ni mshamba.

Lakini pia watu wengi walitoka bara kwenda maeneo ya pwani kutafuta maisha kiufupi maeneo ya pwani yalianza kua miji kabla ya maeneo mengi ya bara.

Ndio maana huwezi mweleza kitu Ramadhan Dau, Sykes, JK, Mohamed Said, Rupia, hawa na wengine wengi kwanza wanafahamiana kabisa ndio maana kuna vitu ukifanya wanakuita mshamba au limbukeni.

Nadhani mlimsikia Nape akisema Boss wake mshamba au mliona polepole kujisifia v8 aliitwa mshamba, hilo kuanzia leo mlichukue.
Watu wanapenda mnanda, mchiriku watu wanapenda wacheze vanga na wanywe mnazi na huo ndio utamaduni wao.

Ndio maana hata watoto wa manzese hawachelewi kumwita vunjabei mshamba yaani pisi wanayokula watu kwa chips yeye anatumia mabilioni kuipata hapo ndio kizaazaa huanzia.
Habari ndo hiyo!
 
Kwenye huu uzi tuweke na trending stories za ajabu from Pwani na Bara ndiyo utaona wapi wanatisha kwa mambo ya hovyo.
Kuna lecturer wangu (RIP) alisoma Israel, alituambia kule wanaamini bora Muafrika asiyeenda shule unaweza mwambia kitu akaelewa kuliko alieenda shule.
 
Ukweli ni huo Mkuu,

Bara ni shamba na dunia ilianza kuchangamka maeneo ya pwani tokea kitambo.

Wakati watu wa pwani wanajenga miji yao na kuishi pamoja kule sigimbi ndio kwanza watu walikuwa wanagombea mapango na mawe yaliyolainika Kwa ajili ya makazi.

Wengi wao wakiishi katika koo zao pasi na kuchanganyika na watu wengine.

Unakuta Kila ukoo na chaka lake,ustaarabu utatokea wapi. Unakuta binadamu anatoa harufu Kali ya beberu,mwili wake umefunikwa Kwa vipande vya ngozi (lubega) huyo ndo mtawala wao na wale watawaliwa wameficha pale mbele kwenye kiwanda Cha kuchakata watoto Kwa kipande Cha ngozi huku makalio yakiendelea kufurahia mandhari.

Huwezi kumfananisha mtu wa pwani ambaye anaujua ustaarabu tokea zamani na mtu ambaye akiamka asubuhi anasafisha uso wake Kwa mkojo wa punda hata siku moja.

Watu wa pwani wazee wa vibarakashia wanywa kahawa huku wakishushia na kashata nyakati za jioni wamejivalia misuli huku wakibalizi Kwa mbaali wavuvi wanatoka baharini na samaki walionona. Wakati huo ukipita mitaani unakutana na mpishano mkali wa harufu ya chakula kinachoandaliwa Kwa ustadi wa hali juu.

Kadiri usogeavyo unapata kusikia sauti za pe pe pe pe ni wale wanaopepeta mchele,na zile za kro kro kro za wale wanaokuna Nazi. Si mtu wa pwani yule asiyeijua ladha halisi ya wali nazi.

Wakati huo kule bara ni muda wa kula mihogo na viazi Ile iliyochomwa kwenye jivu la moto. Vitoto vyao vikifukuzana na kuparamia mtu huu na ule. Na wale vijana ndo muda wao wa kurudi kuokota mabungo na wengine wakiburuza minofu ya nyumbu kutoka mawindoni.

Ama Kwa hakika watu wa pwani duniani kote ndio kielelezo cha kustaarabika.
Uzi umenifurahisha sana [emoji16][emoji16]
 
ALLAAH Aliyetukuka Anasema:
“Enyi watu! Hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na Tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa ALLAAH ni huyo aliye mcha Mungu zaidi katika nyinyi” (al-Hujuraat 49: 13).

Na Mtume wa ALLAAH (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Hakuna ubora wa Mwarabu kwa asiyekuwa Mwarabu, wala mweupe juu ya mweusi ... isipokuwa kwa taqwa (ucha Mungu)”.
 
..Aliwahi sema Dully Skyes kuwa Fid Q ni mtoto wa mjini lakini ni mjini Mwanza, mimi (Dully) ni mtoto wa mjini lakini ni mjini Dar es Salaam tena Kariakoo....kwa hiyo kuna mtoto wa mjini na mtoto wa mjini Dar es salaam hawawezi kuwa sawa!
 
Washamba nyie angalia mwenyewe talent zote then fananisha na huko kwenu mmetuzidi kuoza meno tu
Hahaha, nani aliyeoza meno sasa? [emoji23] ninyi hamna akili zaidi ya kutawaza na kufunga kikoi
 
Wazaliwa wa Bara huwaona wazaliwa wa Pwani, wakuja, lihoya!
[emoji23]nilienda Nyamongo nikaitwa LIHOYA! Kutuliza nikaambiwa Sisi tunapenda kuita watu oyaah!

Makavu tu naulizwa wewe umetokea wapi, mwingine akadakia huyo ni lihoya!
Mkuu nipo Nyamongo hapa Nyangoto, hatari sana
 
Silaha ya mtu dhaifu ni kubagua wengine, atabagua wengine kwa rangi ilimradi yeye ndio aonekane bora zaidi. Akishindwa kwenye rangi atahamia kwenye kabila, dini nk
 
Mie nakiri mshamba ila yupo mzee wa kizaramo ananimegea eneo huko shamba Mbezi kila baada ya miezi mitatu ananiitia miguu ishirini tunaenda kumalizana serikali za mitaa na wanasheria juu.

Nimeshachukua 40×40 huku wanae wapo kwenye nyumba yao ya urithi nasikia Mburahati huko kwenye maji machafu na msongamano wakija kustuka mshamba mimi nakula upepo murua kwenye ardhi iliyokuwa yao.
 
Wapi weyeee....wabara ndio wameinvest na kutawala hiyo pwani. Wewe nenda kafunge kikoi ukatawaze kisha upeleke pesa ya minazi kwa Mangi [emoji23][emoji23][emoji23]
Hata uinvest ushamba ni mzigo
 
Ustaarabu na maendeleo siku zote huanzia pwani na kuelekea bara, ila Tanzania imekuwa tofauti kidogo,Ustaarabu umeshamiri pwani ila maendeleo kidogo, kuna maendeleo makubwa bara ila wanazidiwa Ustaarabu na pwani.
 
Sio maeneo waarabu walioyokaa.
Duniani kote maendeleo huanzia pwani kisha kusambaa bara, nenda bara lolote au nchi yoyote hali huwa hivyo na hiyo husababishwa na muingiliano mkubwa wa watu kutoka sehemu mbalimbali.
Huu ni ukweli maeneo ambayo waarabu walikaa ustaarabu uliingia mapema Sana tofauti na maeneo Kama shinyanga
 
Huu Uzi haupo sawa kabisa.

Sifa zote za wasukuma walizonazo mjini ukifika kwao huku wanaonekana si chochote si lolote na ni wavivu.
Maeneo kama shinyanga mpaka kwa wanyantuzu huku Dutwa, Lalago mpaka Itilima

Nimeenda mbeya Nako hivyo hivyo kwa wenyeji wa Mbeya mjini ambao ni Wasafwa.

Hata Tabora kwa wanyamwezi,
Kigoma kwa Waha na
ndugu zao wamanyema
Wafipa kule sumbawanga
Wapimbwe kule mpanda

Hadi wameru kule Arusha.

Hivyo ni kawaida kwa wenyeji kudharaulika
Kwa sababu wageni huja na mitaji, fursa kupata kazi pamoja na connection.

Yaani ukifika mjini bariadi mkoa wa simiyu hakuna anayedharaulika kushinda msukuma, Tena anayedharaulika zaidi ni msukuma kutoka Shinyanga na huko Geita.
Ila Mnyantuzu akigundua wewe ni mswahili utaona shobo zake.
 
Back
Top Bottom