new forest
Member
- Mar 28, 2024
- 35
- 97
Nimelazimika kuleta Uzi huu, kutokana na kuona ongezeko kubwa la watoto wa mitaani, yatima, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, machokoraa, "panya road" na kadhalika.
Ukichungiza matatizo yote hayo, mwanzo wake ni kutokana na mimba zisizotarajiwa.
Kwa vyovyote vile mtoto akiletwa duniani Kwa wakati sahihi, Kwa malengo sahihi, na watu sahihi, hawezi hata siku moja akaishia kuwa chokoraa, mtoto wa mitaani au panya road.
Nafikiri ni wakati umefika kwa jamii yetu kuondoa dhana potofu kuwa Kila tendo la UTOAJI MIMBA ni haramu. Kuna nyakati binti/mwanamke anaweza akapata mimba katika mazingira yasiyotarajiwa au kwa bahati mbaya mfano kubakwa, au binti ni mwanafunzi au umri bado mdogo nk.
Kuna mazingira mengi yanaweza yakatokea, na "option ya kutoa mimba ikawa sahihi zaidi Ili kuepusha matatizo yanayoweza kuzuilika siku za usoni.
Nafikiri ni wakati Kwa jamii yetu kuondoa kasumba ya kuamini Kila tendo la kutoa mimba ni haramu. Na kusema kutoa mimba unakuwa umeua kiumbe hai sio sahihi kwani kiumbe hai kinaanza kuhesabika siku unayo zaliwa.
Wakati umefika Kwa nchi yetu kitunga Sheria kuhalalisha utoaji mimba salama (safe abortion) kama baadhi ya nchi zinavofanya Ili kuepusha jamii na matatizo lukuki yanayosbabishwa na mimba zisizotarajiwa ambazo baadaye zinasababisha watoto wasiotarajiwa, na baadaye tunakuwa na jamii isiyotarajiwa.
Naomba kuwasilisha, wakuu. Matusi, mapovu ruhksa kabisaa. Karibuni.