Je, Walinzi wa Rais aliyefariki huhamia haraka kwa Makamu ambaye atakuwa Rais au ndiyo itakuwa imeshakula kwao?

Je, Walinzi wa Rais aliyefariki huhamia haraka kwa Makamu ambaye atakuwa Rais au ndiyo itakuwa imeshakula kwao?

sijui umeandika nin yaan, kuna watu humu mnatafutaga likes kwa nguvu tuu. sas kwa ujinga wako unazan inakula kwao kivip sasa ?????
 
Wale mabaunsa wakatafute kazi ya ulinzi kwenye makampuni ya ulinzi hasa wale wa chama. Samia atalindwa na wanawake wenzake. Madume ya nini hata akose raha? Ajifunze toka kwa Gadaffi kuwa wadada wanaweza. Kiutendaji na uadilifu ajifunze kwa Angela Merkel.
😂😂😂 wale wanaweza kustaafu au wakapewa majukumu mengine na watalipwa mishahara na huduma nyingine bure maisha yao yote...
 
Mi nitammisi yule jamaa mrefu mweusi ambaye mara nyingi kwenye matukio ya Rais akiwa kwenye watu wengi daima yeye huvaa miwani meusi huku akiwa anaongea na mic ya mkononi.

Afu yule mlinzi mwingine mpemba mwenye sigda, najua anaweza akabaki na Mama Samia kwakuwa wote ni wa njia moja.
Yule siyo mpemba kwao ni mafia/rufiji siku moja Jiwe alimtambulisha barabarani. Alikuwa anapata wakati mgumu na shida sana wakati wa mfungo kwasababu wakati huo mara nyingi ziara za Jiwe zilikuwa sokoni.
 
Yule mpambe arudi kambini.

Samia ana mpambe wake wa Kike.

Wengine waje huku mtaani waje tujumuike kwenye kujiajiri!
Kuna watu wanafikiri mtu akitoka kwenye nafasi anarudi kupigika kifukara pamoja nao mitaani
 
Tena nimedokezwa hivi sasa anakuja na best cream ya Vijana wa CDF Mabeyo kutoka pale Sangasanga ( Kizuka ) Mkoani Morogoro ila wamepata Mafunzo ya kisasa kabisa kutoka nchi zilizoiva Kimedani na Kijasusi pia.
Si useme tu Israel taifa teule.
 
Wale mabaunsa wakatafute kazi ya ulinzi kwenye makampuni ya ulinzi hasa wale wa chama. Samia atalindwa na wanawake wenzake. Madume ya nini hata akose raha? Ajifunze toka kwa Gadaffi kuwa wadada wanaweza. Kiutendaji na uadilifu ajifunze kwa Angela Merkel.
Sio suala la kuweza ni suala la ujinsia

Mwanaume hawezi kubeba mkoba wa mwanamke wenye taulo

Bosi mwanamke akianguka mwanaume hawezi kumuingia mwilini
 
Kuna watu wanafikiri mtu akitoka kwenye nafasi anarudi kupigika kifukara pamoja nao mitaani
Endapo wakirudi mtaani, hawatapigika wale wenye mitazamo mizuri tu. Kumbuka sio wote wenye mitazamo mizuri
 
Kweli nimeamini kufa kufaana na kwamba Mafanikio yako kwa muda fulani yasikufanye ukawadharau wa chini yako kwani huenda nao Siku Moja wakawa juu na Wewe ukawa chini yao.

Kutesa kwa zamu na sasa ni zamu ya Walinzi Wengine waliokuwa Wakichekwa na waliokuwa Juu yao na Kutanua na Boss wao anayepanda Ngazi nao Kunenepeana kwa kula Kuku na Mibufee ya maana tu.

Binafsi nitammisi sana tu yule Bonge.
Before and after,
Mwaka 2015 na 2021
20210319_113813.jpg
20210319_113921.jpg
 
Back
Top Bottom