Je Waliowahi Kutendwa Hupenda tena?

Je Waliowahi Kutendwa Hupenda tena?

Gagurito

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Posts
5,600
Reaction score
806
Ni muda mrefu sasa umepita tangu nipotee jamvini, wakuu mambo yalibana sana then ubize wa maisha ulichangia. Niliwamiss sana ndugu zangu, nashukuru mungu kuona mambo yanakwenda vyema, kwa wale memba wageni nachukua nafasi hii kujitambulisha pia kuwakaribisa!

Wakuu kama ilivyo jadi yetu ya kufahamishana, kuelimishana, kufarijiana, kukosoana na kushauriana ilivyo, napenda mnijuze juu ya hoja hapo juu, Napenda kufahamu juu endapo mtu ametendwa or alikwishawahi kutendwa ANAWEZA KUPENDA TENA? Nakama akipenda je atapenda kama alivyopenda awali? Na ni nini madhara yakutendwa katika mahusihano? Tujadili.
 
Huwa wanapenda tena ila mara ya pili huwa wanakuwa makini sana!
Madhara yake ni kwamba baadhi ya watu huathirika kisaikolojia na kuwaona wote ni kama yule aliyemtenda mwanzo.
 
Madonda ya kuumizwa yakipona upenda tena.Tena huwa upendo na heshima.
 
as long as we live we can't stop loving...and ever one deserve second chance.love is hard,hard is love.
 
Gagu
Hujambo kakaake..
Pole na majukumu na karibu tena dear ..

maswali yako ntakujibu Ijumaa jioni au Jmosi usiku..
Kwa sasa nayaacha ya teleze tu .. asante dear na karibu tena..
 
tena unapenda zaidi ya wa awali sa kama hujui ..............iila ndio uapate wa kukupa faraja na kukushow wats love,ana care feelins zako ,kukuheshim na kukulinda pia,sio wa machungu unaweza kua mwejeji wa mirembe mana itakua machungu square
so itategemea na huyo uliyempata
 
Bahati nzuri mungu alitupa moyo wa kusahau ,uwezekana wa kufungua moyo tena upo ingawa kwa tahadhari zaidi

karibu tena gagurito
 
umewahi kutendwa jibu ndiyo unaweza kupenda tena jibu ndio kwa sababu nina hisia , kwa sasa nina maumivu ngoja niyasikilizie kwanza . Usiombee kutendwa mkuu utaomba duniani ipasuke maana unaona kama ndio last hope .................
moyo najipa kuna ambaye ameandaliwa kwa ajili yangu.........
 
Waswahili wanasemaga

1. Mkuki mtamu kwa nguruwe ila kwa binaadamu mchungu
2. Mzigo wa mwenzio begani kwako ni kama kanda la sufi
3. Mtenda akitendewa hujihisi kaonewa
4. Malipo ni hapa hapa duniani

Kwa kifupi kutendewa si masihara hata kidogo, wengi tunawatendea wenzetu lakini sisi tukitendewa inakua ngumu sana, na inasemwa ukifanya dhambi huku unacheka utaingia motoni huku unalia.

Kikubwa ukitendwa utangalia na kosa liuzito gani, na hapa kikubwa kinachotuumiza zaidi ni AIBU kwa yale yaliyotendeka, je kupenda tena huku ni kwa yuleyule ama kwa mwengine.

Kama kwa yuleyule, utapenda japo utakua bado na majeraha moyoni. TUWE WAAMINIFU KWA WAPENZI WETU
 
Kutendwa naweza kusema nijambo la kawaida kwa maisha yetu ya leo,nimeshatendwa na sio kama nimesahu la hasha bado sijasahau na wala sitosahau sema unajipanga tena upya na maisha lazima ya songe mbele...
 
IMO wanadamu tumetofautiana katika kila aspect... Hasa katika kuhimili maumivu ama kukabiliana na Matatatizo.... Na katika MAPENZI... that is the worst of all na hapo ndo zaidi saana... watu wakitendwa wapishana jinsi ya kurespond; ama jinsi watavokua affected. Kuna watu wa aina tatu (i would say) thou there maybe more..


  1. Kuna mtu anatendwa, but hakati tamaa.... Yeye kila siku anatendwa na kila siku falls again in love - tena sio ile ya mguu moja. No! But ile ya both feets in. Mara nyingi mtu wa namna hii anashindwa kabisa kuishi bila patner (yaani gap ya toka one relationship to another akijitahidi saana ni two weeks maximum); Wana tabia ya kua desperate ile mbaya, hio mara nyingi tokana na kutojua their potential hivo kufanya wapenzi wao mara nyingi kuwachukulia advantage mpaka pale penye kutendwa.... This person mara nyingi hawanaga raha, na hata aweza jiua kwa ajili ya wapenzi..... Sad.
  2. Kuna yule ambae akitendwa mara moja na hasa kama alipenda kuvuka mpaka with all his/her heart and Soul ni kwamba mchezo hapo unakua umeisha!! No loving again.... Ever! Na akipata mtu(mwenza) na akahisi kuahisi kua s/he is falling in love, anakimbia haraka saana for hataki tena those feelings akiamini atatendwa tena. Hawa watu waweza pata mtu wa kumpenda ukweli kabisa BUT hawathamini hilo penzi wala they don't give a damn!
  3. Kuna Mwingine hupenda.... na akitendwa, anaumia na kuugulia moyo wake kwa mda mreeeefu, hata miezi/miaka kadhaa. Then anarudi kwenye mstari na kuamini kua yule Ex alikua tu mpuuzi na hakuona umuhimu wake, hivo basi falls in love again... Anaumizwa, anaugulia kwa mda mrefu, then again..... Mpaka ampate yule ambae anaona ni wake. Hawa watu huamini kua haiwezekani kabisa kua mwanadamu anaweza kosa mtu ambae watapendana sawa.....

Gagurito missed you..... Habari yako bana!
 
Huwa wanapenda tena ila mara ya pili huwa wanakuwa makini sana!
Madhara yake ni kwamba baadhi ya watu huathirika kisaikolojia na kuwaona wote ni kama yule aliyemtenda mwanzo.

Mkuu hii ni kwa nin?
 
Mimi ni mmoja wa wahanga wa kutendwa,kwasasa nishapenda tena,lakini bado ninaogopa ogopa(aliye umwa na nyoka ..........................)

Huku kuogopa ogopa ndio kwanitia shaka, na wasi wasi na aina ya upendo wenyewe!
 
Nafikiri kutenda na kutendwa ni kawaida sana katika mapenzi hivyo basi inatupasa kusamehe, kusahau na kuendelea mbele. Forward forever, backward never!
 
Back
Top Bottom