GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
NILIMWAMBIA CHAMA AONDOKE SIMBA SC
"Baada ya ligi kuisha tu mimi ndo nilimwambia Chama aondoke kwenye timu ambayo yeye ndo anaibeba. Yaani wachezaji 10 anawabeba yeye mgongoni,nikamwambia aje huku ambako kuna wachezaji wazuri ambao hawatomchosha kama kule.
Wewe angalia kikosi chetu kuna mtu anaitwa Bhoka ana balaa zito sana na yule watu watamfaidi kwenye viwanja vikubwa ndo watamjua vizuri Bhoka" Hersi Said, Rais wa klabu ya Yanga.
Chanzo: SR Sports TZ
Kama anadiriki kabisa kusema aliongea na Chama alishindwa kumwambia Manula, Kapombe na Inonga watuumize?