Je, wanaharakati wa kisiasa barani Afrika wanapigania kwa dhati mabadiliko ya kidemokrasia au maslahi yao binafsi?

Kabla ya demokrasia tulikuwa na mfumo gani wa utawala?
Badala ya demokrasia ungependa tuwe na mfumo gani wa utawala?
 
Nchi nyingi Africa wana siasa bado wanafight ili waweze kujaza matumbo yao. Angalia wakosoaji wakipewa madaraka wanavyobadilika ghafla.
Rais Museveni alipokuwa na miaka 3 ofisini alisema; "Matatizo ya Afrika ni marais kuktawala muda mrefu bila kungatuka". Alipigiwa makofi sana! Leo hii mwenyewe anaikana kauli yake kwa vitendo.

Ni vipi leo wananchi wanaweza kumuamini mwanaharakati yeyote yule hata akiwa na maneno matamu kama asali? Hata Lissu, Lipumba, Membe wangeingia madarakani, sijui kama wangetoka baada ya mihula miwili - miaka 10. Sishawishiki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…