DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Wanabodi,
Jambo lolote jema ambalo limeleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya watu, liwe la serikali au mtu binafsi linahitaji pongezi. Pongezi sio tu katika kuonyesha maisha yaliyoguswa na kitendo hiki bali pia kumpa motisha aliyefanya tendo hilo kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa mwenendo huohuo.
Ila tuelewe kwamba kuna pongezi za kweli na katika vipindi vingine kuna pongezi zingine zinazo onekana kama njia ya kujikosha kwa kiongozi. Kwa mfano, falsafa ya 4R ya Rais Samia ambayo imepigiwa debe na wanasiasa wengi ni mfano wa kupongeza ila kwa njia ya kujikosha. Kiongozi anayepongezwa kwa njia kama hii hawezi kujua kama kweli wanao muunga mkono wanafanya hivyo kwa kutumia viashiria hai au ndio basi tu, kwasababu yeye ni mkubwa na Rais wa nchi.
Falsafa ya 4R haielezei kwa undani kuhusu jinsi ambavyo inaweza kutumika kwenye taasisi mbalimbali kuongeza uchapakazi au kuleta maendeleo (yaani 4R sio specific na ni vague). Tofauti na hilo, kama kweli unakubali kwamba falsafa ya 4R imechochea kwa kiasi kikubwa Tanzania kupiga hatua fulani na upo radhi kuinadi na kutangaza falsafa hii kwa watu wengine basi na wewe utakuwa unajikosha tu bila kuchanganua 4R vizuri
Mfano mwingine ni filamu ya royal tour ambayo imeigharimu serikali fedha nyingi, ikitumiwa kama njia ya kutangaza vivutio vya utalii nchini. Kuna njia mbadala za kutangaza vivutio hivi. Kwa mfano matangazo kwenye majarida yanayo somwa na wengi kimataifa, matangazo ya runinga kwenye chaneli za kimataifa na kadhalika. Siamini kwamba filamu ya royal tour imetazamwa na watu wengi na kwasababu hiyo sikubali kwamba ongezeko la watalii ni kwasababu ya filamu ya royal tour. Ila tumpongeze Rais Samia kwa njia mbadala zilizotumika kuongeza watalii wanaokuja Tanzania ila tusiseme kwamba ni kwasababu ya royal tour.
Anaye jikosha atakuwa anafanya hivyo akifikiria kwamba maslahi yake yanaweza kubadilika kwasababu hiyo au labda anaweza kupata cheyo kikubwa zaidi serikalini kwasababu ya kujikosha.Labda Rais Samia ameisha kuwa Rais wa misifa, labda kuwa na watu wanaomuunga mkono bila kumpa challenge yoyote ndio mwenendo wa serikali hii, labda hutujiulizi maswali ya kutosha kabla ya kuchakata kaulimbiu za serikali. Usikubali kutekwa akili kiurahisi na kitu kinacho trend kwenye
mitandao