Je, Wanaume wanaogopa ku-date na Wanawake waliowazidi kipato?

Mimi ni mmoja wa wasiogopa status ya mwanamke wa aina yoyote ila tu niwe na income ambayo ntaacha kodi ya meza na pango la nyumba, siku hizi waoga wengi, angalizo mwanaume alishe familia na alipe kodi ya nyumba yeye, kama anapesa basi awe na moyo wa kunipa kiasi cha pesa kikae kwenye account yangu pasipo masharti wala mikataba sijui nini wala nini. Mwaume lisha na lipa kodi hapo siogopi kiumbe ila unilishe na ulipe kodi halafu pocket inasumbua ntakula mzigo ntasepa tu kilazima
 
Wanawake mlio na vipato hamtaki kujishusha mnataka mpambane na wanaume ndo maana yote yanatokea hayo unatakiwa mwanamke ujishushe sasa hlo kwenu gumu.
 
Majibu someni hapa

 
Maneno ya wanawake wenye vipato huwa yanaumiza sana. Anakwambia wewe huna jeuri ya kunitunza mimi, mimi naweza kukuweka ndani na kukuhudumia, labda amekupigia simu umechelewa kurudi home anakwambia kwenda huko hata usiporudi mimi sijali. siku umetoka safarini bila ya kuleta kitu home badala ya kupokelewa unaambiwa si bora ungebaki hukohuko.Kuishi nao inahitaji uvumilivu sana ndo maana tuliambiwa tuishi na kwa umakini

Sent from my SM-A500H using JamiiForums mobile app
 
Asilimia kubwa ya wanawake waliowazidi kipato wanaume zao hujiona kuwa wao ndio babaz wa familia hivyo mambo ya heshima sijui kuhudumiwa sijui kuwa chini ya mwanaume utayasikia kwa makungwi tu.
 
HEKIMA
Bado naangaza macho kuona wanawake wenye uchumi uliosimama Kama ndoa zao zinadumu ??
 
wasababu hii mada ni story ya kweli ninachukua muda hasa kusoma na kutafakari mtazamo wa mwanaume juu ya kudate na mwanamke aliemzidi kipato.

Nimejivua uhusika nikasimama pembeni kuangalia Wanawake ambao mnawataka nyie kaka zetu sifa mlizoweka hajasoma sana au asiwe na kipato kukuzidi meaning wewe ndio umtunze na kuangalia mahitaji mengine.

Hili ni jambo jema kabisa hata mimi ningependa wa hivyo ila je mmewaza huyu unae taka awe goli kipa ndie mama wa watoto wako ? Ndio partner wako na ndio mtunza siri wako na mshauri wako?

Mnajua wanawake wa hivi siku mkifa hua wananyanyasika sana kwa kunyang'anywa mali, je nani atatunza wanao ikiwa mama yao hakua na kipato cha kutosheleza?

Siku ukiugua ni yeye atakaehangaika kukuhudumia wakati ndugu zako na marafiki zako hawakujali. Tena siku utakayo ugua ukamaliza fedha zote hadi kuuza baadhi ya mali ili ujitibie mwanamke huyu ndio atatakiwa ahakikishe bado unapata huduma ipasavyo na aangalie hapo ndani mnaishije?!

Nyinyi ni mashahidi namna familia inavyoteseka siku yule breadwiner akiugua au kufariki. Vipi kama angekua na kazi ambayo ingeweza kusupport mahitaji na matunzo ya hapo ndani?

Ninaifahamu familia ambayo mume aliugua haswaaa ikafika sehemu ambayo alihitaji kwenda India....hakua na bima wala kazini kwake hawakua na utaratibu wa kutibwa nje ya nchi ila baba huyu kilichomsaidia ni Bima nzuri ya kazini kwa mke kwake alipokua anafanya kazi ndio iliwezesha matibabu. Mwingine ni baba alikumbwa na hizi tumbua jipu za mwendazake pila alieshikilia mhimili na kuficha aibu ya familia ni mama. Watoto wanasoma, wanakula na maisha yanaendelea.

Tukiangalia nchi zingine baba haoni shida kua stayhome dad, yani anabaki nyumbani anatunza watoto mama ndio aende kazi ( Japo hii kiukweli hata mimi inanipa ukakasi hahahaha)

All in all sioni sababu ya mwanaume kuogopa kua mwanamke akimzidi kipato atamdharau au atapata wa level zake kikubwa mwanaume ajue namna ya kumtiisha mke wake lazima mwanaume accomand respect .

Mwanamke aliefundwa na mwenye akili atamzidi kipato mumewe lakini nyumbani atabaki kua mke na mama wa familia na kufanya yanayompasa kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…