Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Kazi ngumu
Wanawake wazee
Kazi nzito
Chakula Duni
Pombe kali
 
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume wengi walioko kwenye ndoa wanakufa mapema na kuwaacha wake zao, ingawa swali linabaki kuwa ni kwanini?

Zifuatazo ni sababu 6 za wanaume wengi walioko kwenye ndoa kufa mapema na kuwaacha wake zao.


1. Ugumu katika kufunguka.
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia
mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza.


2. Ugumu katika kusamehe.
Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu, hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote.
Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sana kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.

3. Tabia hatarishi.
Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao
waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni mkoani.

4. Ugumu katika kujali afya.
Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe mwongo.
Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.

5. Msongo wa mawazo.
Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo “stress” ingawa kwa nje wanajitahidi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, stroke, kusimama kwa
moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.


Hizi Ndio Sababu Zinazowafanya Wanaume Kufa Mapema Kabla ya Wanawake | UDAKU SPECIAL BLOG
 
NI KWELI KABISA WANAUME HUFA NAPEMA, Nyongeza, NENO ambalo halirudi bure linasema Kwakuwa ulitwaliwa ktk navumbi, na mavumbini utarudi(MWANZO 3:19) Hilo neno linaonyesha kuwa aliyeambiwa atakufa ni mwanaume, kwahiyo mwanaume yu karibu sana na kifo zaidi ya mwanamke.
 
Nyongeza. Ajali za gari boda boda bajaji wengi madereva wanaume. vitani wanakufa wengi wanaume. Wanaume ni washiriki sana ktk maisha hata hatarishi ujambazi mkubwa mdo
 
Asante kwa kutukbusha upande wa pili pia
 
Nyongeza. Ajali za gari boda boda bajaji wengi madereva wanaume. vitani wanakufa wengi wanaume. Wanaume ni washiriki sana ktk maisha hata hatarishi ujambazi mkubwa mdo
Kweli kabsa mkuu... Umeongeza point nondo
 
Safiii....pia tunatumia akili nyingi sana kutongoza aisee
 
Habari ya wakati huu,

Katika uchunguzi wangu usio rasmi nimebaini asilimia kubwa ya wanawake walio kwenye ndoa huamini waume zao watawatangulia kufa. Isitoshe wengi pia huwaombe wanaume wao wafe mapema kama mwanaume huyo ana vijisenti.

Ndio maana unakuta wanawake wanawashinikiza wanaume wao kuwaambia kila wanachofanya ili wanaume watakapokufa mwanamke awe anajua kila kitu kilipo ajimilikishe. Utasikia mwanamke anasema inabidi ajue kila kutu maana kinaweza kutokea la kutokea, maana yake mwanaume atakapokufa gafla mwanamke awe anajua kila kitu kiko wapi.

Wanawake hawajiwazii wao kuwahi kufa mbele ya waume zao, sijui huu uhakika wa wao iutokuwahi kufa wanautoa wapi.

Naomba ieleweke kua huu ni mtazamo wangu na sina nia ya kukashfu mtu yoyote.
 
Nafikiri hapo sababu kubwa ni kwamba kwenye ndoa nyingi mume anakua na umri mkubwa kuliko mke. So its obvious kwamba mume ndio atatangulia kufa kama mambo yote yatakua kawaida. Ni sawa hakuna mtoto anaewaza atakufa kabla ya mzazi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…