Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Mwanaume mpumbavu hujisababishia kifo cha mapema.
 
Duu!! Binafsi namini kuna vitu tunawawazia vibaya cjui lakini!! Yani mke Wangu Padri alituambia tuu mwili mmoja Leo awaze Mali Nikifa? Binafsi siamini kama Ipo ila siyo kwa Mkewangu. "Penye mafanikio ya mume jua mke yupo nyuma mna anasapoti" Ndiyo mna kuna marais wanagombea urais ila lazima wahakikishe mke yupo, Sijui ni mtazamo Wangu
Braza unaishi dunia gani? Je Padri hakukwambia uishi nae kwa akili?
Hahahha, kumbe kweli ee

Wanawake wengi walioolewa wao ndio chanzo cha vifo vya waume wao!
 
Kwani kitabu cha dini yako kinasemaje? Umesoma angalau hata sheria za nchi zinasemaje kuhusu jukumu la mume kumtunza mke? by the way unataka mali zako arithi nani kama si mke na watoto?
Hii ni tabia ya roho mbaya na choyo.

Binafsi napata benefit zote kutoka kwa mke wangu through her rights, health insurance and likes.

Mimi myahudi,hebu niambie kitabu changu cha dini kinasemaje kwny hili?!
 
Habari ya wakati huu,

Katika uchunguzi wangu usio rasmi nimebaini asilimia kubwa ya wanawake walio kwenye ndoa huamini waume zao watawatangulia kufa. Isitoshe wengi pia huwaombe wanaume wao wafe mapema kama mwanaume huyo ana vijisenti.

Ndio maana unakuta wanawake wanawashinikiza wanaume wao kuwaambia kila wanachofanya ili wanaume watakapokufa mwanamke awe anajua kila kitu kilipo ajimilikishe. Utasikia mwanamke anasema inabidi ajue kila kutu maana kinaweza kutokea la kutokea, maana yake mwanaume atakapokufa gafla mwanamke awe anajua kila kitu kiko wapi.

Wanawake hawajiwazii wao kuwahi kufa mbele ya waume zao, sijui huu uhakika wa wao iutokuwahi kufa wanautoa wapi.

Naomba ieleweke kua huu ni mtazamo wangu na sina nia ya kukashfu mtu yoyote.


Hii ni tabia ya wanawake wa kichagga a.k.a. Majambazi Meusi!
 
Kweli Mkuu hasa kuna kabla flani ukioa hizo stress lazima uondoke kabla hujapata mjukuu


Ule mkoa wenye ule Mlima...lile kabila mimi hata unipe demu wa kuoa bure sichukui labda wa kuchapa tu, tena porini na kumkimbia. Na kabla ya hapo inabidi nimsachi kwanza.
 
Make sense, doesn't it?...Takwimu zinaonyesha wanaume wanakufa kwa wastani wa umri mdogo kuliko wanawake, na wanaume wanaoa wanawake waliowazidi umri mara nyingi, so wana kila sababu ya kuamini hivyo
Mkuu eti mfano Mimi ni mwanamke sasa mwanaume kanikuta na Mali zangu, akanioa hivi pia zile mali zangu pia ni za kwetu wote kisheria???
 
Research hii ilifanywa kwenye ule mkoa uleee.

Watu wale wanajulikana kwa kutanguliza waume zao kwa makusudi kabsa.
 
Nilipokuwa mdogo niliamini lazima aanze kufa baba,afuate mama then mtoto wa kwanza na wa mwisho kufa ni kitinda mimba kama mm,.basi kuna muda nilikuwa nafarijika nikiamini mpaka wote hawa waishe nitakuwa Na cku nyingi za kuspend duniani,..
Hahahaha kumbeeee ni mipango ya MUNGU tuu Na utoto ulinidanganya
Ila kwa upande wa ndoa hata mm nimeliona hilo, wanawake wengi hujiongelea kuwazika waume wao kabla ya wao.
 
Habari wapambanaji, nataka kufanya kilimo cha mihogo kibiashara zaidi naomba kupata somo ASA kuhusu masoko, na usimamizi wakee mzima..naomba sana mwenye uzoefu wa kilimo ichi anipe uzoefuu
 
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume wengi walioko kwenye ndoa wanakufa mapema na kuwaacha wake zao, ingawa swali linabaki kuwa ni kwanini?

Zifuatazo ni sababu 6 za wanaume wengi walioko kwenye ndoa kufa mapema na kuwaacha wake zao.


1. Ugumu katika kufunguka.
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia
mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza.


2. Ugumu katika kusamehe.
Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu, hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote.
Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sana kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.

3. Tabia hatarishi.
Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao
waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni mkoani.

4. Ugumu katika kujali afya.
Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe mwongo.
Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.

5. Msongo wa mawazo.
Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo “stress” ingawa kwa nje wanajitahidi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, stroke, kusimama kwa
moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.

Kuwa open, roho safi and less agressive
aiseee namba 6 vipi
 
Kila binadamu aliyezaliwa huongezeka kimo kuanzia akiwa mtoto, kijana na hatua ya mwisho ni uzee na kifo. Kifo hakina kanuni na kinaweza kumpata mtu yoyote wakati wowote.

Matarajio ya watu wengi ni kuishi mpaka uzeeni lakini umri wa kuishi hutofautiana toka nchi moja hadi nyingine kulingana na mazingira yanayowazunguka watu wa taifa husika.

Umri wa kuishi pia hutofautiana kati ya wanaume na wanawake, ambapo wanawake katika maeneo mbalimbali wanaishi miaka mingi kuliko wanaume. Nchi ya Sweden ambayo inaaminika kuwa na huduma bora za kijamii, umri wa kuishi kwa wanawake ni miaka 83.5 na wanaume 79.5.

Utafiti uliofanywa na Chuo cha Imperial cha London (2017) na Shirika la Afya Duniani uliangazia umri wa kuishi katika mataifa 35 yaliyostawi kiviwanda na ulibaini kwamba wanawake nchini Korea Kusini watakuwa wa kwanza duniani kuwa na umri wa kuishi wa zaidi ya miaka 90.

Utafiti huo unaeleza kuwa watu watakuwa wakishi miaka mingi kuliko sasa kufikia mwaka 2030 na pengo kati ya wanaume na wanawake litaanza kufutika katika mataifa mengi.

Kwa Tanzania, idadi kubwa ya wanawake wanaishi hadi miaka 63 na wanaume miaka 61, ambapo umri huo wa kuishi umeongezeka kutoka miaka 57 kwa wanawake na 54 kwa wanaume kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi, 2012. Tofauti inayojitokeza ni kuwa wanawake wanaishi muda mrefu kwa zaidi ya asilimia 2 kuliko wanaume.

Licha ya wanawake kuishi muda mrefu lakini inatajwa katika tafiti mbalimbali kuwa wanawake wa Afrika hufariki zaidi wakiwa katika umri wa miaka 15 na 34 kutokana na matatizo ya uzazi na huduma duni za afya.

umri_24851656_1e7cd2408107b528ae4b62e182cb64e2dd66dfe4.png


Zimekuwepo hisia kuwa kazi ngumu kwa wanaume ndizo zinawamaliza mapema. Lakini hoja hii haina nguvu kwa wakati huu kwasababu wanaume na wanawake wote wanajihusisha katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali toka migodini, mashambani hadi katika biashara.

Unywaji wa pombe, kuvuta sigara na kula chakula kupita kiasi imetajwa kama sababu nyingine ya wanaume kufa mapema. Watetezi wa sababu hii wanasema matumizi ya pombe na sigara huathiri baadhi ya viungo vya mwili.

Wanatoa mfano wa wanaume kutoka nchi ya Urusi ambao hufariki miaka 13 mapema kuliko wanawake kwa sababu wengi wao wamekithiri kwenye unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara.

Kutokuwa na ajira kwa mwanaume kunaweza kumsababishia afe mapema. Kulingana na riport ya Mtandao wa Afya ya Wanaume (MHF) inasema 20% ya wanaume wasio na ajira wana uwezekano wa kufa mapema kuliko wanaume walio na kazi. “Wote tunafamu kuwa wagonjwa wengi hawafanyi kazi” anasema Martin Tod, Mkurugenzi Mtendaji wa MHF. “Ripoti yetu inaonyesha kuwa mwanaume ambaye hajaajiriwa anakuwa mgonjwa”

Watafiti mbalimbali wanakubaliana na sababu ya kibaolojia na mabadiliko ya watu kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

“ Ni kweli mitindo ya maisha inachangia lakini haichukuliwi kama jambo ambalo limejikita katika maumbile ya mwanadamu” anasema Tom Kirkwood, mwanafunzi wa Chuo Cha Newcastle nchini Uingereza.

south-africas-history-of-tobacco-control.jpg


Vinasaba Vilivyo katika mwiili wa mwanadamu (DNA) vinatofautiana katika kufanya kazi na kuweza kuhimili mabadiliko ya kimazingira. Inatajwa kuwa mwanamke ana DNA ambayo ina kromosumu X na Y na mwanaume ana X ambayo ikichoka hana nyingine ya kumsaidia ikilinganishwa na mwanamke mwenye mbili ambapo moja ikichoka nyingine huendelea kuhimili mabadiliko ya kiafya kwa muda mrefu.

Mtaalamu wa maabara nchini Ujerumani, Dk James Vaupel anadai kuwa vinasaba huchangia kasi ya kuzeeka kwa asilimia tatu pekee na sehemu kubwa ya visababishi vya kuzeeka haraka hutokana na mtindo wa maisha usiofaa pamoja na lishe duni.

Magonjwa ya moyo yanachangia pia kwasababu ya msongo wa mawazo ambao wanaume wanakutana nao katika majukumu ya kila siku na kuwapunguzia umri wa kuishi. Wanawake hawako katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo kutokana na mfumo wao wa damu ambao kila mwezi hupata hedhi na kuwasaidia kusafisha damu.

Upatikanaji wa huduma za afya, pesa na mabadiliko ya kiuchumi katika familia nayo huchangia wanaume kufa mapema.



Hali ilivyo Afrika Mashariki

Umri wa kuishi kwa wananchi wa Tanzania hautofautiani sana na wananchi wa nchi nyingine za Afrika Mashariki. Kwa Burundi wanawake huishi hadi miaka 62 na wanaume miaka 58, huku Kenya miaka 65 kwa wanawake na wanaume (62).

Kwa upande wa Uganda, wanawake (56), wanaume (54) na Rwanda inakaribiana na Kenya ambapo wanaume huishi kwa wastani wa miaka 58 na wanawake (61).

Licha ya umri wa kuishi kati ya mwanamke na mwanaume kutotofautiana sana kwa wananchi wa Afrika Mashariki, bado kuna watu wanaishi hadi miaka 80 na wakiwa na nguvu wanafika miaka 100.



Mambo ya kuzingatia ili kuishi muda mrefu

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wakazi wa maeneo mbalimbali wanaoishi maisha marefu zaidi duniani kama vile Japani, Italia na Marekani, pamoja na mambo mengine, wanajiepusha na matumizi ya vileo, tumbaku na kupunguza ulaji wa nyama nyekundu.

Nyama yenye shida kubwa ni ile yenye mafuta mengi, nyama choma iliyoungua na ile iliyosindikwa. Nyama ya namna hii huchangia kutokea kwa magonjwa ya moyo, kiharusi, kisukari na saratani ya utumbo. Hii inasababisha uzalishaji wa kemikali zinazodhuru afya.

Pia kuvuta hewa safi ya kutosha na kupata mapumziko ya kutosha baada ya kazi ngumu kila siku. mazoezi na kula chakula asilia cha mimea kama vile mbogamboga na matunda kwa wingi.

Vyakula vya asili vineelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa matokeo ya watu kuishi miaka mingi kuliko wale ambao hawazingatii utaratibu huo.

Wataalamu wa masuala ya afya ya jamii wanaongeza kusema kuwa, uhusiano bora na mtazamo chanya katika maisha huongeza urefu wa maisha kwa miaka saba na nusu.
 
Back
Top Bottom