Sote tunajua kibiolojia wanaume tuna Maisha mafupi (short life span)kuliko wanawake
But kuna jambo katika pitapita zangu maeneo mbalimbali ya nchi hii,kupitia simulizi za watu mbalimbali nikagundua katika familia nyingi zina wanawake wajane,yani waume zao walikwishafariki
Ni familia chache utasikia baba yupo ila mama alifariki.
Hasa wazee wengi wastaafu walishafariki na kuacha wake zao, vijana mbalimbali walishafariki na kuacha wake/wapenzi wao
Najiuliza tatizo nini hasa linalopelekea wanaume wengi kufa mapema katika ndoa zao/mahusiano yao na kuacha wanawake
Je wanawake ndio chanzo kikubwa cha hivyo vifo au ni mipango ya mungu tu.
Je watoto pia ni chanzo au shida iko wapi!!?
unatunza familia yako,ukweni ,nyumbani na mashemeji kitu cha kwanza ni kunywa pombe na cha pili ni presha au kufa na hasa ukipata mke ambaye hakulindi na anakumaliza kabisa
Nikifikiria hili suala sipati jibu.
Nawasilisha.