Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Shalom wana jamvi!

Nimetafakari mwenyewe naona kama majibu hayakuji, au kuna maandiko pengine yanasema mwanaume atakufa mapema kuliko mwanamke? Kuna wengine nimepata kusikia wanasema eti mwanaume akipiga bao moja anapoteza dakika 3 za kuishi na wanasema hiyo ni kisayansi naamini humu wanasayansi wapo wengi watanitoa tongo tongo.

Ukitazama katika jamii wanawake waliofiwa na waume zao ni wengi kuliko wanaume waliofiwa na wake zao, hiyo imekuwa kama kawaida hivi hata wanawake katika kusisitiza waume zao kuwekeza katika assets huwa wanatumia msemo wa "Baba chanja kuna Leo na kesho usijetuacha tukawa tunateseka". Sasa hebu tuambiane ni kisayansi, kimaandiko au ni mazingira yanapelekea mwanaume anakufa mapema kuliko Mwanamke????
Karibuni kwa hoja
 
kuanzia pesa,kujenga familia,mapenzi na kazalika kila kitu ni wewe.nani mwanaume kwa nini usife mapema
alafu ukiongeza na mchepuko duuu
 
Ni kwa sababu mwanaume anachepuka sana, so anajitengenezea sumu bila kujijua
Kuchepuka ndo kunamfanya mwanaume afe mapema? Unamaanisha kila wanaume anayekufa basi mchepuko umemfanya atangulie??
 
Wapo lakini ni wachache mkuu, na hufanya kwa siri sana
 
Risk taker..
angalia kazi tuzifanyazo wanaume nyingi ni risk,kazi ngumu.. maisha yetu yanakuwa kwenye hatihati ktk pilika za utafutaji wa maisha tupo mstari wa mbele,pia ktk kukabiliana na hatari(mazingira ya hatari) sisi tunahusika sana.. pamoja na tabia wanaume huwa tuna tabia fulani za ubishi,utawala ikitokea umedharauliwa basi vurugu linaanza hivyo lolote laweza tokea.. baada ya kufanya kazi ngumu utapita bar kupiga mbili tatu,sigara kazaa(unaharibu mapafu),huku ukiwa umelewa utaendesha gari,pikipiki n.k ukiteleza kidogo kwaheri..
kiujumla wanaume ni watu tunaokuwa kwenye risk kubwa kushinda wanawake.
 
Back
Top Bottom