SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,841
- 1,843
Wanadamu tunaamini katika maisha baada ya kifo, ingawa maisha haya yanapishana kutokana na dini mbalimbali, lakini kwa ujumla common ground ni kuwa tutaishi baada ya kufa. Msingi wa maisha baada yakifo ni imani kuwa mbali na viungo vyoote tulivyonavyo, pia tuna ROHO.
Na nimsingi wa uwepo wa roho (soul) ndo unaojenga nadharia ya maisha baada ya kifo katika dunia mpya. Kumekuwa na dhana na mtizamo tofauti katika wanyama na mimea linapokuja swala la roho. Wanazuoni wanaamini kuwa mimea na wanyama hawana roho na sifa hii ya mwanadamu ni kati ya sifa kuu zinazomtofautisha binadamu na wanyama au mimea.
Swali la kujiuliza ni Je,kama msingi wa imani ya uwepo wa roho kwa wanadamu unajengwa na imani ya maisha baada ya kifo. Na kwa kuwa maisha baada ya kifo ni dhana ya kidini kwa wafuasi wa Mungu mmoja.
Na ni roho ndo inaaminika kuwa huendeleza maisha kwa kwenda mbinguni Je vitabu vya dinivinasemaje kuhusu uwepo wa wanyama na mimea katika dunia ya roho/ mbingu (ntazungumzia biblia, mwenye taarifa nakuran ntaomba achangie mtizamo huo) Isaya 65:25 "mbwa mwitu namwanakondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ngo'ombe, na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka.
Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote" asema Bwana. Nabii isaya anathibitishakuwa mbinguni kutakuwa na wanyama na anatoa mfano wa mbwa mwitu, kondoo, ng'ombe,simba, na nyoka. Ufunuo 19:14 pia Yesu anaonekana akirudi na jeshi lake la mbinguni huku akiwa juu ya FARASI mweupe.
Lakini pia Ufunuo 22:1-3 inaonyesha kuwa mbinguni patakuwa na miti. Je hii ni uthibitisho kuwa wanyama na mimea pia wana roho kamawanadamu, na kila wanyama na mimea wanapopoteza maisha roho zao huishi na pia huenda mbinguni kama wanadamu ili kungojea ile siku kuu ya Dunia mpya ya waliochaguliwa na Mungu pekee.
Karibuni.
CC Ishmael, Eiyer, Punjab Singh, Mkuu wa chuo