Kwanza namna viumbe vingine tofauti na Binadamu viliumbwa kwa Mungu kutamka tu,yaani neno ndilo lililoumba [Yesu],lakini binadamu aliumbwa au kwa lugha nyingine Mungu mkamilifu [nafsi zote tatu] zilihusika kwenye uumbaji wa mwanadamu na hata alivyoumbwa imeelezwa,kwa maana hiyo basi viumbe vingine vina uhai lakini havina roho
Nasema hivyo kwasababu Mungu ni roho na wakati anamuumba binadamu alisema kabisa "tumuumbe mtu kwa mfano wetu [roho]" lakini wakati anamuumba binadamu hakusema hivyo,kwa maana hiyo kama hakumuumba mbuzi au ng'ombe kwa mfano wake na Mungu ni roho basi hao wengine hawana ule mfanano wa Mungu ambao ni roho
Nikija kwenye hoja yako ya uwepo wa viumbe wengine baada ya maisha haya ni kwamba kwanza haijaelezwa kuwa vitafufuliwa hivi ambavyo leo vinakufa bali imeelezwa vitakuwepo kama hivi,sasa kwa maana hii ni kwamba inawezekana vitaumbwa vingine tofauti na hivi na tutaishi navyo milele bila kuharibika!