Je wanyama na mimea wana roho (do animal and plants have soul)

Je wanyama na mimea wana roho (do animal and plants have soul)

mkuu nipe tafsri yako, kwa sababu ukipitia quote zangu tayari nimeshatolea maelezo ya perfect

Kwa maana ninayoijua mimi ni "ukamilifu",sijaelewa unahusishaje ukamilifu na kutokuumba tena!
 
Kwanza namna viumbe vingine tofauti na Binadamu viliumbwa kwa Mungu kutamka tu,yaani neno ndilo lililoumba [Yesu],lakini binadamu aliumbwa au kwa lugha nyingine Mungu mkamilifu [nafsi zote tatu] zilihusika kwenye uumbaji wa mwanadamu na hata alivyoumbwa imeelezwa,kwa maana hiyo basi viumbe vingine vina uhai lakini havina roho

Nasema hivyo kwasababu Mungu ni roho na wakati anamuumba binadamu alisema kabisa "tumuumbe mtu kwa mfano wetu [roho]" lakini wakati anamuumba binadamu hakusema hivyo,kwa maana hiyo kama hakumuumba mbuzi au ng'ombe kwa mfano wake na Mungu ni roho basi hao wengine hawana ule mfanano wa Mungu ambao ni roho

Nikija kwenye hoja yako ya uwepo wa viumbe wengine baada ya maisha haya ni kwamba kwanza haijaelezwa kuwa vitafufuliwa hivi ambavyo leo vinakufa bali imeelezwa vitakuwepo kama hivi,sasa kwa maana hii ni kwamba inawezekana vitaumbwa vingine tofauti na hivi na tutaishi navyo milele bila kuharibika!

Kwanza lazima tujue tofauti kati ya "soul na spirit" soul ni sehemu tu ya human councious ila spirit ndio roho yenyewe when one has communion with God tunasema ana spiritual strenght.

Na pia binadamu anajamuishwa na vitu vitatu body, soul, and spirit.
 
Kwa maana ninayoijua mimi ni "ukamilifu",sijaelewa unahusishaje ukamilifu na kutokuumba tena!

ukamilifu wa uumbaji ni kwamba vitu vyote vilivyoumbwa vilikuwa vikamilifu kwa vigezo vyote vya kidunia na vya kimbingu. kwa hali hiyo hakuna uumbaji mwingine unless kuna kiumbe ambacho uumbaji wake haukuwa "mkamilifu".

kwa hiyo dhana ya uumbaji mwingine wa wanyama na mimea uta imply kuwa havikuubwa kwa ukamilifu katika uumbaji wa kwanza. so there will be no perfection.
 
Roho ni synonym ya uhai. Tofauti ni kuwa neno Roho limekaa kiimani zaidi na uhai limekaa kisayansi zaidi. Hivo naamini kuwa viumbe vingine vina roho kama binadaam. Ndio maana hata kwenye Bible sikumbuki kifungu gani lakini ni Mwanzo inaelezea jinsi mwanadamu alipotofautishwa na viumbe wengine kwa kuongezewa utashi baaasi. So tuna roho/uhai so as viumbe wengine.
 
Kwanza lazima tujue tofauti kati ya "soul na spirit" soul ni sehemu tu ya human councious ila spirit ndio roho yenyewe when one has communion with God tunasema ana spiritual strenght.

Na pia binadamu anajamuishwa na vitu vitatu body, soul, and spirit.
Soul ni roho
Spirit ni nafsi

Usichanganye hayo mawili ...!!
 
uwepo wa hii roho tunaitambua vipi kama haionekani kwa sababu tunaamini mwili wa binadamu una viungo na organs zinazofanya kazi ili kuweza kuupa mwili nafasi ya kumudu mazingira yanayozunguka. Na kitendo cha kuvuta na kutoa pumzi ni matokeo ya respiration process.

Tunatambua uwepo wa roho kupitia imani ...!!
 
fafanua kidogo utafiti

Umezungumzia wanyama kama wana roho ama la! Wao wote wanazaliwa na wanakufa so kitendo cha kufa ndio hiyo roho imeacha mwili. Wangekua hawana roho wasingekufa kama vile hatujawahi kusikia jiwe limekufa
 
Last edited by a moderator:
ukamilifu wa uumbaji ni kwamba vitu vyote vilivyoumbwa vilikuwa vikamilifu kwa vigezo vyote vya kidunia na vya kimbingu. kwa hali hiyo hakuna uumbaji mwingine unless kuna kiumbe ambacho uumbaji wake haukuwa "mkamilifu".

kwa hiyo dhana ya uumbaji mwingine wa wanyama na mimea uta imply kuwa havikuubwa kwa ukamilifu katika uumbaji wa kwanza. so there will be no perfection.

Kama unazungumzia ukamilifu kwa maana ya kutokuumba tena unakosea kwasababu hadi leo Mungu anaumba

Kama unadhani ukamilifu unamaana ya "kutokuongeza" kiumbe kingine kwa maana ya kuumba kiumbe cha aina nyingine tofauti na vilivyopo unaweza k uwa sahihi labda!
 
Wanadamu tunaamini katika maisha baada ya kifo, ingawa maisha haya yanapishana kutokana na dini mbalimbali, lakini kwa ujumla common ground ni kuwa tutaishi baada ya kufa. Msingi wa maisha baada yakifo ni imani kuwa mbali na viungo vyoote tulivyonavyo, pia tuna ROHO.

Na ni
msingi wa uwepo wa roho (soul) ndo unaojenga nadharia ya maisha baada ya kifo katika dunia mpya.
Kumekuwa na dhana na mtizamo tofauti katika wanyama na mimea linapokuja swala la roho. Wanazuoni wanaamini kuwa mimea na wanyama hawana roho na sifa hii ya mwanadamu ni kati ya sifa kuu zinazomtofautisha binadamu na wanyama au mimea.

Swali la kujiuliza ni Je,kama msingi wa imani ya uwepo wa roho kwa wanadamu unajengwa na imani ya maisha baada ya kifo. Na kwa kuwa maisha baada ya kifo ni dhana ya kidini kwa wafuasi wa Mungu mmoja.

Na ni roho ndo inaaminika kuwa huendeleza maisha kwa kwenda mbinguni
Je vitabu vya dinivinasemaje kuhusu uwepo wa wanyama na mimea katika dunia ya roho/ mbingu (ntazungumzia biblia, mwenye taarifa nakuran ntaomba achangie mtizamo huo) Isaya 65:25 “mbwa mwitu namwanakondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ngo’ombe, na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka.

Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote” asema Bwana.
Nabii isaya anathibitishakuwa mbinguni kutakuwa na wanyama na anatoa mfano wa mbwa mwitu, kondoo, ng’ombe,simba, na nyoka. Ufunuo 19:14 pia Yesu anaonekana akirudi na jeshi lake la mbinguni huku akiwa juu ya FARASI mweupe.

Lakini pia Ufunuo 22:1-3 inaonyesha kuwa mbinguni patakuwa na miti. Je hii ni uthibitisho kuwa wanyama na mimea pia wana roho kamawanadamu, na kila wanyama na mimea wanapopoteza maisha roho zao huishi na pia huenda mbinguni kama wanadamu ili kungojea ile siku kuu ya Dunia mpya ya waliochaguliwa na Mungu pekee.

Karibuni.

CC Ishmael, Eiyer, Punjab Singh, Mkuu wa chuo

Unaanza tena; roho ndio nini?
 
Tunatambua uwepo wa roho kupitia imani ...!!

Kwa hiyo naweza kuamini kwamba hakuna roho ?maana si ni imani pia?.Kwa nn wewe imani yako umeelekeza postively?kwa nn isiwe kinyume?Huoni kwamba unalazimisha kile unachodhani kipo kiwepo?
 
Umezungumzia wanyama kama wana roho ama la! Wao wote wanazaliwa na wanakufa so kitendo cha kufa ndio hiyo roho imeacha mwili. Wangekua hawana roho wasingekufa kama vile hatujawahi kusikia jiwe limekufa

nimekupata mkuu CC Eiyer
 
Last edited by a moderator:
Kama unazungumzia ukamilifu kwa maana ya kutokuumba tena unakosea kwasababu hadi leo Mungu anaumba

Kama unadhani ukamilifu unamaana ya "kutokuongeza" kiumbe kingine kwa maana ya kuumba kiumbe cha aina nyingine tofauti na vilivyopo unaweza k uwa sahihi labda!

thibitisha mkuu
 
Back
Top Bottom