Je, wapinzani ni wakombozi?


Alah! We are on the same page. I personally I've had it up to here and I want both of them to take place simultaneously (though it may be a tall order)....I just can't stand them anymore....I just want them to go away...
 
Nadhani swali la msingi ambalo bila ya shaka linakuwa wazi katika hoja ya Pundit ni kuwa tuiindoe CCM ili kiwe nini? au tuiondoe CCM alimradi imeondoka halafu tufikirie tufanye nini wakishaondoka?

Kama CCM haitaki kubadili katiba na mambo (institutions) mengine, tuiondoe ili tuweze kufanya hayo mabadiliko maana kuwepo kwao madarakani ni kizingiti cha mabadiliko ambayo baadhi yetu tunayataka na ambayo tuna imani yatakuwa na faida ktk mustakabali wa taifa.
 
Mbona wakoloni tuliwaondoa na hatukuhoji (labda wapo waliohoji) wala kusubiri kubadili institutions walizozijenga? Hatukutaka kusubiri hadi waanze kuzibadilisha wenyewe na wala jitihada hazikulenga ktk kubadili institutions...lakini tukawatimua. Sasa nakubali kuwa baada ya kuwatimua tulitakiwa kuzibadili lakini hatukufanya hivyo. Hilo lilikuwa ni kosa na shame on us tukilirudia tena.
 

I am with you on this, intitutional changes are paramount, either before or parallel with regime change.But lets not kid ourselves that we will achieve much, say with regime change without institutional changes.

Tutabadili chupa wakati mvinyo utakuwa ule ule.
 

That's correct!

Mambo ya kusubiria mpaka institution zijengwe na wale ambao hawako tayari kujenga hizo institution ni kosa la msingi ambalo inabidi lisifanywe tena.
 
You have the option to do a simultaneos effort encompassing the two.
 

Mkuu pundit,

we'll also be just doing the same thing if we wait for ccm to make these institutional changes. Get rid of roadblocks (ccm) on our way and .........
 

Pundit:

Nakubaliana na mawazo yako kimsingi. Lakini si unakumbuka ukiwa mtoto ulivyotaka kuoga maji ya baridi. Kwanza uli-test maji kwa kidole kimoja. Baadaye kwa kiganja. Na mpaka pale mwili uliposisimka ndipo uliweza kujimwagia maji mwili mzima.

Kuna watu waliamini kabisa bila kuwepo Nyerere nchi haiwezi kujiendesha yenyewe. Nchi inajiendesha yenyewe bila kuwepo kiongozi mmoja anayesimama kama kiranja mkuu.

Kuna watu wanaoamini kuwa bila CCM, basi matatizo yaliotokea Rwanda, Uganda au Congo Zaire yatatupata pia. Wao hawawezi kuona mfano wa Zambia au Malawi.

Kwa maoni yangu, taasisi zilizopo zinatosha. Tatizo ni kuwa vyama vya upinzani kwa watanzania wengi ni umande na wanaogopa kuuvaa umande kwenda shule au shamba.
 

Bin Maryam,

I feel you on this. Kuna watu wanasema "be careful what you wish for, you may receive it".Basically I am envisioning watu washaitoa CCM na tuna upinzani kwenye power bila institutional changes. Watakubali kuji clip wings in the interest of government efficiency and integrity au ndiyo tutaona kama mambo aliyoleta Kibaki alipochaguliwa mara ya kwanza?

My fear is that human nature is too unrealiable, that is why we need clear institutional changes at least simultaneously with regime change, if not before.
 
That's correct!

Mambo ya kusubiria mpaka institution zijengwe na wale ambao hawako tayari kujenga hizo institution ni kosa la msingi ambalo inabidi lisifanywe tena.

sio kujenga anamaanisha kama vile kubadili katiba na mfumo wa utawala.
 

Pundit,

Umejaribu kuimagine kile kinachoendelea sasa hivi:

Watoto kufa hospitalini bila dawa au magonjwa yanayotibika wakati richmonduli/dowans pekee wakilipwa billions of dollars kwa sababu zisizoeleweka kabisa!

That is worse to me than a monster under my bed!
 

Things like this make me wanna pull my hair...
 
Tulipowaondoa wakoloni tulifanya wakati huo huo kuingiza watu wapya. Tulifanya hivyo tukiamini kuwa wakoloni ndiyo kizuizi cha maendeleo yetu na hivyo wao wakiondoka tukishika sisi wenyewe basi mambo yatakuwa mazuri.

Matokeo yake ni yapi? Wale tuliowaingiza si walifanya vizuri mwanzo lakini baadaye wameanza kugeuka na kuitwa wakoloni weusi? Na kuna watu wamefikia kudiriki hadi kusema "bora mkoloni"!

Sasa, tunapotamania kuiondoa CCM na utawala wake huku tukitumaini kuwa wale watakaoingia watakuwa bora zaidi. Matumaini hayo yanajiandaa kufeli kama sheria ya pili ya thermodynamic (the law of entropy) of which my esteemed friend Pundit is very familiar with inavyotuhakikishia.

Kwa hiyo naamini tunapanga na kufikiria kuing'oa CCM ni lazima tuwe very focused kuwa hatuing'oi CCM ili tubadilishe tu (cosmetic change) bali tubadilishe kwa kilichobora. Lakini pia hatuna budi kutambua hata hicho kilichobora nacho kitavuruga (the law of entropy). Jukumu letu basi ni kuhakikisha hicho kilichobora kinazuiwa kuvuruka kwa kiasi kikubwa kama wale tuliowatoa.

To me the question is, tunajuaje kilichobora ambacho chapaswa kuchukua nafasi badala ya CCM na viongozi wake? Je tunatafuta chama au watu?
 
Naona wengi tunaelekea katika jibu la matatizo ya maendeleo katika nchi zetu. Tatizo lililopo kubwa sana ni tatizo la kikatiba basi. Tatizo la kikatiba ndilo tatizo linalopelekea hata kuwa na viongozi wenye viburi, viongozi wasiokuwa tayari kubadilika, viongozi wasiokuwa tayari kutenda yale waliohapa kuyatenda.Viozingo MAFISADI nk.

Katika hili suala bila kuwa focused hata wapinzani wakiingia mambo yataendelea kuwa yale yale.

Mnasikia kila siku waziri wa katiba akisema katiba haiwezi kubadilika mpaka sijui kipindi gani. Haya yote ni kwa sababu ameisha onja utamu uliopo akiwa na katiba isiyoweza kufanya viongozi wawajibike kwa umma.

Hivyo hivyo tukiondoa CCM leo watakao ingia bila kuwa na katiba iliyokuwa focused inayoainisha nini kifanyike ujue tumeliwa.

Lakini ikitokea ikaonekana watawala waliopo hawako tayari kukubaliana na matakwa ya wananchi kilichopo ni kutafuta njia ya kusonga mbele lakini ukijua kuwa bado hatujafika mwisho wa mapambano.

Msingi mkuu wa kumletea mwananchi/mtanzania maendeleo utaanzia kwenye sheria mama ambayo ni katiba ya nchi.
 
Wengi wetu hapa tuko ktk ukurasa mmoja ila baadhi ya wenzetu wako ktk aya tofauti. Binafsi sikatai institutional changes kuwa
ni muhimu na lazima zitokee. CCM kama ingekuwa inataka hayo mabadiliko yangekuwa yameshatokea kuanzia serikali ya awamu ya kwanza. Mpaka sasa haijaonyesha nia yoyote ile ya kuongoza mabadiliko hayo na kwa mtizamo wangu imekuwa kizingiti. Sasa kama tunayataka hayo mabadiliko na kuna kizingiti njiani kwa nini tusikiondoe?

Mimi sitaki tena CCM waongoze taifa hata kwa siku moja zaidi kwani hawastahili hata kidogo. No! No! No! God Damn them! They have blood on their hands.

Ningependelea mabadiliko ya kikatiba yaende sambamba na ya kiutawala. Lakini kama hilo haliwezekani basi ni bora waondoke kwanza halafu tutadili na hayo mengine baadae. How much longer do you people want CCM to rule?
 
Nadhani swali la msingi ambalo bila ya shaka linakuwa wazi katika hoja ya Pundit ni kuwa tuiindoe CCM ili kiwe nini? au tuiondoe CCM alimradi imeondoka halafu tufikirie tufanye nini wakishaondoka?

Mguu wenye kansa tunaukata kwanza ili kuepusha kifo. Baada ya hapo ndo tutajua tuweke mguu wa bandia,robot au atembelee magongo.

CCM wamesha-prove kuwa hawana uwezo wa kuongoza kwa sasa.Miaka 46ya madaraka imewalevya. Hivi watanzania tunahitaji nini zaidi!!
 
..."be careful what you wish for, you may receive it".Basically I am envisioning watu washaitoa CCM na tuna upinzani kwenye power bila institutional changes...

Tuseme tumedai regime change tumepata. Halafu hakuna institutional change. Chupa mpya mvinyo ule ule, kama ulivyo sema kwa utaalam mkubwa. Sawa.

Sasa hivi hatujapata institutional change wala hatujapata regime change. Sawa?

Kipi bora, chupa mpya mvinyo ule ule au mvinyo ule ule na chupa zee, lina mi cracks kwenye mdomo huwezi hata kunywa mvinyo ule ule?

Nini ubaya wa kuwa na li Sisiem jipya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…