Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 1,211
- 233
Hivi CCM PAMOJA NA KUWA NA MIAKA 30 TOKA IANZISHWE na kutia ndani mali zote tulizokuwa tukiambiwa ni za Chama cha wananchi wote wakati wa chama kimoja imeacha lini kupata ruzuku toka serikalini?Hivi baina ya CCM na Vyama vingine vya kisiasa ni chama kipi kinapata ruzuku zaidi?Hivi ni chama kipi ambacho kinaendesha Nchi na Kinahusika na mwenendo wa uchumi wetu kupitia ridhaa waliyopewa na wananchi kuongoza Nchi.
Na Ramadhan Semtawa
JESHI la Polisi limeanza kuwachunguza mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa chama hicho Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa tuhuma za uchochezi.
Tuhuma hizo zinatokana na maneno ambayo wanasiasa hao, wamekuwa wakiyatoa sehemu mbalimbali kabla na katika ziara zao zinazoendelea mikoani hivi sasa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Kamishna Robert Manumba, alilisema uamuzi huo hauna maana ya kuingilia uhuru wa raia kutoa maoni, bali kuhakikisha kuwa sheria za nchi hazikiukwi.
Akifafanua kuhusu tuhuma hizo, Kamishna Manumba alisema Agosti 14, mwaka huu, Kabwe akizungumza katika kituo cha televisheni ya Channel Ten, alisikika akiwashawishi wananchi wayashambulie kwa mawe malori yanayobeba mchanga kutoka machimbo ya Bulyanhulu, mkoani Shinyanga.
Aliongeza kwamba, Septemba 9, mwaka huu, Mbowe akiwa katika ziara ya viongozi wa vyama vya upinzani mjini Tabora, alisikika akiwataka askari wa majeshi yote, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla, kuachana na dhana ya amani na utulivu na kwamba wapo tayari kuwasha moto.
Kutokana na matamshi hayo, kamishna Manumba alisema tayari polisi makao makuu imemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kuanza uchunguzi mara moja.
"Jeshi la Polisi lenye dhamana ya kulinda amani na utulivu nchini, linachukua hatua za kuchunguza matamshi ya viongozi hao kama yamekiuka sheria," alisema na kuongeza:
"Kwa kuanzia, tumemwelekeza Mkuu wa Polisi Mkoa wa Tabora kuanza uchunguzi mara moja kuhusu matamshi ya uchochezi yanayodaiwa kutamkwa na viongozi hao walipokuwa mikoani humo.
"Jeshi la polisi limekuwa likifuatilia kwa makini kauli zinazotolewa na viongozi hao wa kisiasa ili kuhakikisha kuwa malumbano ya kisiasa yanayoendelea hayakiuki sheria za nchi, kwa lengo la kudumisha amani na utulivu nchini."
Kamishna huyo alifafanua kwamba, kama Kabwe na Mbowe wana taarifa zozote zenye mwelekeo wa uhalifu wanapaswa kuzipeleka kwenye vyombo husika ili zifanyiwe kazi.
"Ni mategemeo ya Jeshi la Polisi kwamba viongozi wenye dhamana kama walivyo wao, wangetumia taratibu za kisheria zilizowekwa kushughulikia taarifa za uhalifu walizonazo," alisisitiza na kuongeza:
"Pamoja na uhuru wa kutoa mawazo walionao viongozi wetu wa kisiasa, tunawasihi wajiepushe kutoa kauli au matamshi yenye mwelekeo wa uchochoezi," alitahadharisha Kamishna Manumba.
Tangu kusimamishwa kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge, Kabwe akiwa na viongozi wengine wa vyama vya siasa, wamekuwa wakizunguuka Mikoani kueleza mambo mbalimbali kuhusu nchi.
Kabwe alisimamishwa na Bunge kufuatia hoja yake ya kuliomba Bunge kuunda tume ya kuchunguza mkataba wa mgodi wa Buzwagi ambao ulisaininwa na Waziri wa Nishati na Madini kinyume na maagizo ya Rais Jakaya Kikwete ya kusimamisha mikataba yote mipya hadi hapo sheria ya madini itakapotiwa na kufanyiwa marekebisho
source:
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=1562
Ni wazi kuwa CCM imeanza kuonyesha dalili ya kukataa kuwa chaka la rushwa, ufisadi na hata ukosefu wa maadili miongoni mwa viongozi wake. Ingawa kinachoonekana sasa kinabaki kuwa dalili za zoezi lenyewe na unaweza kusema ni ujanjaujanja wa aina fulani huku kukiwa na manung'uniko ni kuwa kinachendelea ni mikakati ya kushika nguvu za kisiasa ya baadhi ya wanaCCM ama binafsi ama kwa makundi yao ya kimadaraka, lakini ukweli unabaki kuwa kinachoendelea kinasaidia kupunguza kasi ya kuanguka kwa CCM.
Zoezi hili kama litafika mbali ni wazi litarudisha imani ya wanaCCM na watanzania wengine ambao wamekuwa mguu nje mguu ndani wakijitahidi kujitoa katika kile wakionacho ni uchafu uliojaa katika kundi lao. Hivyo wanaweza kurudi nyumbani na kuchukua jembe kwenda shambani kuendeleza kazi ya ushindi wa tsunami huko mbeleni.
Wakati hii ni habari njema kwa wanaoamini kuwa TANZANIA NI CCM na CCM NI TANZANIA, wale tuaminiao umuhimu wa upinzani makini na wenye uwezo wa kutoa chaguo tofauti la kisiasa, ni wazi tupo mtegoni. Hii inatokana na ukweli kuwa wakati uchafu wa rushwa,ufisadi na uporomokaji wa maadili yaani unyang'au umejikita ndani ya CCM, upande wa pili ambao ungeliweza kuwa kimbilio la wenye kuthubutu nako ni kama tusemavyo, HAWAVUMI LAKINI WAMO.
Sina haja ya kuwapa ushindi makada vipofu ambao hupenda kufurahia hadi meno 38 kuonekana waonapo wale wadhaniao kuwa maadui zao wakianikwa kweupe. Hivyo sitasema mengi kuhusu kuchipuka kwa unyang'au (rushwa,ufisadi na ukosefu wa maadili) ndani ya kundi la upinzani.
Hoja yangu ni kuwa wakati CCM wanaanza kuonyesha dalili ninyi muonyeshe mfano jinsi zoezi la safishasafisha lifanywavyo ndani ya vyama vyenu.
Tofauti na CCM ambako walitoka enzi za umangimeza hadi uvigogo katika masuala ya unyang'au, kwenu ndugu zangu ndio kwanza kuna tuvijogoo vichache ambavyo kuvitoa kafara hakutawapa matatizo makubwa kama hali inayowasibu wenzenu wa CCM.
Kazi kwenu, jisafisheni haraka ama mtajikuta mnabaki kuwa Vi-NGO kama Mzee Mapesa alivyofanikisha kukigeuza chama chake UDP.
Tanzanianjema
We kaka,
Nani kukudanyanya CCM imekataa kuwa chaka la rushwa?
Wangekataa kuwa chaka la rushwa si wangeshughulikia RADA, IPTL, RICHMOND, BOT nk katika serikali yao?
Wamekaa vipi wakati rushwa imetolewa nchi nzima kwenye uchaguzi wa CCM kuanzia ngazi ya matawi mpaka wilaya mpaka sasa?
Nawe bwana, unakubali kufanyiwa usanii kwa kutumia tukio la Arusha?
Nyuma ya "Arusha" ni mapambano za rushwa za makundi ndani ya CCM na matokeo yoyote yale lazima kundi moja la rushwa ndio lishinde ati!
CCM ilichokifanya ni kuahirisha mjadala tu kwa sasa mpaka mahakama ifanya uamuzi mpenzi.
Lakini rushwa itadumu. Kidumu CCM
Rushwa ni alama ya ushindi, ilitumika kwenye uchaguzi mkuu kuwashinda wapinzani wa nje, sasa inatumika kuwashinda wapinzani wa ndani.
Wapinzani nao si vyema wakatoa rushwa? Pesa sabuni ya roho
Asha
Nadhani TanzaniaNjema ameleta changamoto nzuri sana kwa vyama vya upinzani. Kama nitakuwa nimemuelewa vizuri anachotaka kusema hapa ni kuwa kuna some changes ndani CCM ( Japo ndogo sana) katika suala zima la vita dhidi ya rushwa, kwa mtazamo wake kama wapinzani hawatajipanga vizuri ( na wao kusafisha nyumba zao) CCM itawapiga bao.
La msingi hapa ni kuifanyia kazi changamoto hii, badala ya kuanza kulaumu CCM kuwa ni danganya toto, dharau kama hizi zaweza kuwa na athari kubwa kwa ustawi wa upinzani.
Nadhani TanzaniaNjema ameleta changamoto nzuri sana kwa vyama vya upinzani. Kama nitakuwa nimemuelewa vizuri anachotaka kusema hapa ni kuwa kuna some changes ndani CCM ( Japo ndogo sana) katika suala zima la vita dhidi ya rushwa, kwa mtazamo wake kama wapinzani hawatajipanga vizuri ( na wao kusafisha nyumba zao) CCM itawapiga bao.
La msingi hapa ni kuifanyia kazi changamoto hii, badala ya kuanza kulaumu CCM kuwa ni danganya toto, dharau kama hizi zaweza kuwa na athari kubwa kwa ustawi wa upinzani.