Je, wapinzani ni wakombozi?

Je, wapinzani ni wakombozi?

Hivi CCM PAMOJA NA KUWA NA MIAKA 30 TOKA IANZISHWE na kutia ndani mali zote tulizokuwa tukiambiwa ni za Chama cha wananchi wote wakati wa chama kimoja imeacha lini kupata ruzuku toka serikalini?Hivi baina ya CCM na Vyama vingine vya kisiasa ni chama kipi kinapata ruzuku zaidi?Hivi ni chama kipi ambacho kinaendesha Nchi na Kinahusika na mwenendo wa uchumi wetu kupitia ridhaa waliyopewa na wananchi kuongoza Nchi.
 
Mzee Mwanakijiji,

Huyu Ngawaiye sielewi kabisa anachozungumza hapa... Mimi sii mmoja wa wananchama ama mwanzilishi wa chama hiki kipya lakini nitamjibu kwa ustaarabu.
Kwanza kabisa natanguliza maelezo ya kumshukuru kuweza kuweka vipengele vikubwa vinavyo kwamisha maendeleo ya Tanzania na Afrika kwa Ujumla!...
1. Ubinafsi 2. Undugunization 3. Jino kwa Jino strategy 4. Ujuzi wa kujenga uchumi bila kutegemea misaada na mwisho 5. Imani ya dini kutawala sheria za chama.
Kwanza kabisa kaanza na swala la Ubinafsi!...
Hakuna chama nchini na Afrika nzima kwa ujumla kisichokuwa na viongozi wenye Ubinafsi.. hii ikiwa ni pamoja na chama tawala yaani CCM. Kwa hiyo kinachoanzishwa hapa sio jambo jipya kwa wananchi isipokuwa upo uwezekano mkubwa wa kuondoa kipengele hicho kwa sababu ya huu umoja wa vyama hivi. Hii ni hatua ya kwanza ya kimapinduzi na ya msingi kwa viongozi ambao kamwe wasingeweza kufikia hili kama Ubinafsi ungetangulia maslahi ya nchi yetu.
Swala la Pili ni hilo la kupeana madaraka kifamilia...
Hili pia silingekamilika bila muungano huu ambao unajumuisha vyama vyenye makabila mengi zaidi..Hivyo utaratibu wa Chadema kama alivyounukuu hauwezi kufanya kazi ndani ya TLP, CUF ama NCCR-Mageuzi na hata utaratibu wa CUF ama TLP hauwezi kufanya kazi ndani ya vyma vyote vinne vilivyokusanya makabila na dini tofauti.
Undugunization umetumika miaka yote ndani ya CCM na tumeona kila mwaka akiibukuba mtoto wa fulani kushika madaraka. Ni maisha tuliyoyazoea na yawezekana kabisa hawa jamaa wakaleta sura mpya kwani hawa sii ndugu wala hawatoki sehemu moja.
Tatu, hiyo jino kwa jino ni mfumo unaotumika sana kwa viongozi wetu wa vyama tawala kuliko vyama vya Upinzani tofauti ni kwamba vyama tawala kufanya kweli na vya upinzani hutumia maneno haya kama tishio la kupata haki zao. Na jino la chama tawala halina sheria, mwamuzi wala msalie.
Nne, Kama chama tawala kingekuwa na uwezo wa kujenga uchumi leo hii ni miaka 45 hakuna kilichoongezeka zaidi ya kufuga magofu. reli ya kati leo hii inaishia Dodoma, haifiki Dar.. safari ya mabasi mikoani Mungu ndiye anajua..Barabara mbovu kuliko wakati wowote ule. Uchumi wetu unapanda kama pima joto maanake ugonjwa wa umaskini ndio unazidi kila siku..
Mwanza ni safari ya masaa 24, Ukipiti Kenya ni safari ya masaa 30. Kwa ndege nauli ya dollar 200 safari ya saa moja! Umeme ndio kama unavyoona, maji hakuna hata sehemu zilizokuwa na maji miaka ya kujifunga mikanda.
Je, uwezo wa chama tawala ni upi ambao hautegemei ruzuku?...Hivi kutaifisha mali ya Umma na kuifanya mali ya chama tawala ni sifa ya uwezo mzuri wa chama tawala kujijenga!...Je, haiwezekani kuwa hii ndio sababu inayokifanya chama tawala kutoweza kuendesha uchumi wetu kwa sababu inatazama kwanza maslahi ya chama badala ya wananchi na taifa!... Toka lini chama tawala kikafanya biashara za kupangisha majumba ambayo yamejengwa kwa nguvu na mfuko wa wananchi wote.

Mwisho ndugu Ngawaiya, chini ya muungano wao swala la Udini ilitapatiwa ufumbuzi mkubwa. Lipumba au Seif Sharrif hawezi kuzungumzia maslahi ya waislaam ama Zanzibar pekee mbele ya Slaa, Mrema na wengineo na wala hao hawawezi kuyaweka maslahi ya dini zao mbele ya kundi hili jipya.

Kujiunga kwa vyama hivi ni tishio kubwa kwa CCM na hizi ni roho mdundo za watu wanaokuwa na hofu. Moja ya somo la Ukachero ktk kumpata mhusika ni pale anapoanza kulopoka na kusema mapungufu ya shahidi/victim kabla hata hajaulizwa nafasi yake yeye mwenyewe. CCM wanaanza kutapatapaa!
Nawapa hongera kubwa sana vyama vya upinzani kwa hatua kubwa ya mwanzo. Kuweka UBINAFSI wenu kando!
Mapungufu mengine yote katika uongozi ni vitu ambavyo vinaweza kuwekwa mezani na kuzungumziwa tofauti na CCM ambao imani hiyo imeisha tengenezewa dini.
 
huyo mzee inaelekea kisha zeeka sana hata kuishiwa maarifa.kweli nyani haoni nanihiiiii yake.
 
Maneno yake na ya Tambwe si ni yale yale lazima waseme wawese kula ?Ngawaiya ni kapu la mjanja.
 
Hivi CCM PAMOJA NA KUWA NA MIAKA 30 TOKA IANZISHWE na kutia ndani mali zote tulizokuwa tukiambiwa ni za Chama cha wananchi wote wakati wa chama kimoja imeacha lini kupata ruzuku toka serikalini?Hivi baina ya CCM na Vyama vingine vya kisiasa ni chama kipi kinapata ruzuku zaidi?Hivi ni chama kipi ambacho kinaendesha Nchi na Kinahusika na mwenendo wa uchumi wetu kupitia ridhaa waliyopewa na wananchi kuongoza Nchi.

Nadhani utoaji wa ruzuku unaenda na idadi ya wabunge chama kilicho nao!!!
 
Kwanza huyu Ngawaiya aliwahi kuiba matairi kwa kutoa cheki hewa kule general tyre Arusha hivyi huyu sio mtu wa kumsikiliza.
Pili huyu si ndio aliwatuma vibaka wakaibe zile taa za magari yake matano aliyoyaagiza kule bandarini na kwenda kuwadai bandari ili aweze kulipwa?na pia ameweza kuisingizia bandari na kuyatoa magari bandarini kwa amri ya mahakama wakati hajawahi kulipia hata ushuru na hivyo ndivyo ilivyokuwa?watu wa vyombo vya dola kupitia jjf naweza kuwapatia ushahidi jinsi ambavyo gari hizo hazijalipiwa ushuru kwani zilitolewa bandarini kwenda kuwa kama ushahidi mahakamani na Gawaiya kafanya ujanja na kukabidhiwa magari bila ushuru huu ni wizi.
Ushahidi hapa naweza kuwapa kei no.then mfuatilie.
 
Halafu kuna hii pia... Ni kweli haiendelei au ndo imesahaulika tu? Kama imefikia tamati nayo tuiweke kulee ------>>>?
 
Na Ramadhan Semtawa

JESHI la Polisi limeanza kuwachunguza mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa chama hicho Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa tuhuma za uchochezi.

Tuhuma hizo zinatokana na maneno ambayo wanasiasa hao, wamekuwa wakiyatoa sehemu mbalimbali kabla na katika ziara zao zinazoendelea mikoani hivi sasa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Kamishna Robert Manumba, alilisema uamuzi huo hauna maana ya kuingilia uhuru wa raia kutoa maoni, bali kuhakikisha kuwa sheria za nchi hazikiukwi.

Akifafanua kuhusu tuhuma hizo, Kamishna Manumba alisema Agosti 14, mwaka huu, Kabwe akizungumza katika kituo cha televisheni ya Channel Ten, alisikika akiwashawishi wananchi wayashambulie kwa mawe malori yanayobeba mchanga kutoka machimbo ya Bulyanhulu, mkoani Shinyanga.

Aliongeza kwamba, Septemba 9, mwaka huu, Mbowe akiwa katika ziara ya viongozi wa vyama vya upinzani mjini Tabora, alisikika akiwataka askari wa majeshi yote, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla, kuachana na dhana ya amani na utulivu na kwamba wapo tayari kuwasha moto.

Kutokana na matamshi hayo, kamishna Manumba alisema tayari polisi makao makuu imemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kuanza uchunguzi mara moja.

"Jeshi la Polisi lenye dhamana ya kulinda amani na utulivu nchini, linachukua hatua za kuchunguza matamshi ya viongozi hao kama yamekiuka sheria," alisema na kuongeza:

"Kwa kuanzia, tumemwelekeza Mkuu wa Polisi Mkoa wa Tabora kuanza uchunguzi mara moja kuhusu matamshi ya uchochezi yanayodaiwa kutamkwa na viongozi hao walipokuwa mikoani humo.

"Jeshi la polisi limekuwa likifuatilia kwa makini kauli zinazotolewa na viongozi hao wa kisiasa ili kuhakikisha kuwa malumbano ya kisiasa yanayoendelea hayakiuki sheria za nchi, kwa lengo la kudumisha amani na utulivu nchini."

Kamishna huyo alifafanua kwamba, kama Kabwe na Mbowe wana taarifa zozote zenye mwelekeo wa uhalifu wanapaswa kuzipeleka kwenye vyombo husika ili zifanyiwe kazi.

"Ni mategemeo ya Jeshi la Polisi kwamba viongozi wenye dhamana kama walivyo wao, wangetumia taratibu za kisheria zilizowekwa kushughulikia taarifa za uhalifu walizonazo," alisisitiza na kuongeza:

"Pamoja na uhuru wa kutoa mawazo walionao viongozi wetu wa kisiasa, tunawasihi wajiepushe kutoa kauli au matamshi yenye mwelekeo wa uchochoezi," alitahadharisha Kamishna Manumba.

Tangu kusimamishwa kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge, Kabwe akiwa na viongozi wengine wa vyama vya siasa, wamekuwa wakizunguuka Mikoani kueleza mambo mbalimbali kuhusu nchi.

Kabwe alisimamishwa na Bunge kufuatia hoja yake ya kuliomba Bunge kuunda tume ya kuchunguza mkataba wa mgodi wa Buzwagi ambao ulisaininwa na Waziri wa Nishati na Madini kinyume na maagizo ya Rais Jakaya Kikwete ya kusimamisha mikataba yote mipya hadi hapo sheria ya madini itakapotiwa na kufanyiwa marekebisho

source:

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=1562

Jee CCM inataka kutumia askari polisi kumnyamazisha Zitto??
 
CCM inaonekana imeshindwa hoja na sasa wanataka kuwatumia polisi kama ilivyokuwa kawaida yao.

Chadema nawaomba muwe makini na matamshi yenu kwani sasa CCM imeshapata kisingizio na inataka kutumia hazina yao ya dola.
 
Mfa maji hakosi kutapatapa,hakuna anayechochea watu kufanya fujo,hizo ni propaganda tu za serikali.WEmbe ni ule ule,hata wakati wa kudai uhuru wanaharakati na wanasiasa walikamatwa kuwa wanachochea jamii kufanya fujo.
 
Ni wazi kuwa CCM imeanza kuonyesha dalili ya kukataa kuwa chaka la rushwa, ufisadi na hata ukosefu wa maadili miongoni mwa viongozi wake. Ingawa kinachoonekana sasa kinabaki kuwa dalili za zoezi lenyewe na unaweza kusema ni ujanjaujanja wa aina fulani huku kukiwa na manung'uniko ni kuwa kinachendelea ni mikakati ya kushika nguvu za kisiasa ya baadhi ya wanaCCM ama binafsi ama kwa makundi yao ya kimadaraka, lakini ukweli unabaki kuwa kinachoendelea kinasaidia kupunguza kasi ya kuanguka kwa CCM.

Zoezi hili kama litafika mbali ni wazi litarudisha imani ya wanaCCM na watanzania wengine ambao wamekuwa mguu nje mguu ndani wakijitahidi kujitoa katika kile wakionacho ni uchafu uliojaa katika kundi lao. Hivyo wanaweza kurudi nyumbani na kuchukua jembe kwenda shambani kuendeleza kazi ya ushindi wa tsunami huko mbeleni.

Wakati hii ni habari njema kwa wanaoamini kuwa TANZANIA NI CCM na CCM NI TANZANIA, wale tuaminiao umuhimu wa upinzani makini na wenye uwezo wa kutoa chaguo tofauti la kisiasa, ni wazi tupo mtegoni. Hii inatokana na ukweli kuwa wakati uchafu wa rushwa,ufisadi na uporomokaji wa maadili yaani unyang'au umejikita ndani ya CCM, upande wa pili ambao ungeliweza kuwa kimbilio la wenye kuthubutu nako ni kama tusemavyo, HAWAVUMI LAKINI WAMO.

Sina haja ya kuwapa ushindi makada vipofu ambao hupenda kufurahia hadi meno 38 kuonekana waonapo wale wadhaniao kuwa maadui zao wakianikwa kweupe. Hivyo sitasema mengi kuhusu kuchipuka kwa unyang'au (rushwa,ufisadi na ukosefu wa maadili) ndani ya kundi la upinzani.

Hoja yangu ni kuwa wakati CCM wanaanza kuonyesha dalili ninyi muonyeshe mfano jinsi zoezi la safishasafisha lifanywavyo ndani ya vyama vyenu.

Tofauti na CCM ambako walitoka enzi za umangimeza hadi uvigogo katika masuala ya unyang'au, kwenu ndugu zangu ndio kwanza kuna tuvijogoo vichache ambavyo kuvitoa kafara hakutawapa matatizo makubwa kama hali inayowasibu wenzenu wa CCM.

Kazi kwenu, jisafisheni haraka ama mtajikuta mnabaki kuwa Vi-NGO kama Mzee Mapesa alivyofanikisha kukigeuza chama chake UDP.

Tanzanianjema
 
We kaka,

Nani kukudanyanya CCM imekataa kuwa chaka la rushwa?

Wangekataa kuwa chaka la rushwa si wangeshughulikia RADA, IPTL, RICHMOND, BOT nk katika serikali yao?

Wamekaa vipi wakati rushwa imetolewa nchi nzima kwenye uchaguzi wa CCM kuanzia ngazi ya matawi mpaka wilaya mpaka sasa?

Nawe bwana, unakubali kufanyiwa usanii kwa kutumia tukio la Arusha?

Nyuma ya "Arusha" ni mapambano za rushwa za makundi ndani ya CCM na matokeo yoyote yale lazima kundi moja la rushwa ndio lishinde ati!

CCM ilichokifanya ni kuahirisha mjadala tu kwa sasa mpaka mahakama ifanya uamuzi mpenzi.

Lakini rushwa itadumu. Kidumu CCM

Rushwa ni alama ya ushindi, ilitumika kwenye uchaguzi mkuu kuwashinda wapinzani wa nje, sasa inatumika kuwashinda wapinzani wa ndani.

Wapinzani nao si vyema wakatoa rushwa? Pesa sabuni ya roho

Asha
 
Asha,

Kwa hiyo unamaanisha kwamba CCM hawewezi kujifunza kutokana na mambo yaliyofanyika,,, do you mean CCM watakuwa hivyo milele... mimi siamini hivyo asilani,,, maana hata azimio la arusha walipiga teke,,, wakiaaminisha CCM ya leo sio TANU ya 1967!

CCM ya Nyerere, ya Mwinyi, ya Mkapa sio ya JK as well....

Asha Abdallah wa 1990 sio Asha Abdallah wa 2007 ... huo ndio ukweli... wanasikia vilio vya wananchi, wengine wataweka pamba masikioni lakini wengine hawatakuwa hivyo (watasikiliza), usijekudhani CCM wengine hawakerwi na hali hii, wanakerwa mmojawapo ni JK mwenyewe!

Upinzani, Mrema wa 1995, alikuwa hataki kushirikiana na wapinzani wengine, Mrema wa 2007 ndiye kinara wa kupenda kushirikiana na wengine...

CUF ya 1995/2000 ilikuwa ya fujo tupo, CUF ya sasa inapenda maridhiano...

Jifunze Mama kidogo kidogo alafu weka ushabiki kidogo nyuma ili utumui uwezo wako aliyekujalia mola to the fullest capacity
 
Binafsi naona upinzani ujisafishe kivyao vyao tu,bali siyo kwa kuiga usafi ulioanzishwa hivi karibuni na ccm,japo bado ni chafu 99.9999%.Bado ccm haijafikia hatua ya kuweza kuigwa,kwa lipi zuri?Ni uvundo kila kona,hakuna cha kuweza kujifunza ndani ya ccm,utapeli,ufisadi,udikteta,umangimeza,ubeberu,ukiritimba,unyounyo,uchawi,udini,ukabila,uwana mitandao,majigambo,dharau,sasa lipi zuri la kuigwa?Nakubali upinzani wana udhaifu wao,na wanastahili kusafisha timu yao,wajipange vizuri,watoke kivyao tu,tena nawashauri watumie sera za Mwl Nyerere,ambazo ccm imeamua kuzizika,lakini wasiige mambo ya ccm,watoke kivyao kama alivyotoka Bwana Misosi.Ni kweli kuna baadhi ya viongozi wazuri ndani ya ccm,lakini tunawahitaji watuonyeshe kwa vitendo,na wapinge baadhi ya mambo hadharani,si kujisemea chini chini,huo ni unafiki.
 
Nadhani TanzaniaNjema ameleta changamoto nzuri sana kwa vyama vya upinzani. Kama nitakuwa nimemuelewa vizuri anachotaka kusema hapa ni kuwa kuna some changes ndani CCM ( Japo ndogo sana) katika suala zima la vita dhidi ya rushwa, kwa mtazamo wake kama wapinzani hawatajipanga vizuri ( na wao kusafisha nyumba zao) CCM itawapiga bao.

La msingi hapa ni kuifanyia kazi changamoto hii, badala ya kuanza kulaumu CCM kuwa ni danganya toto, dharau kama hizi zaweza kuwa na athari kubwa kwa ustawi wa upinzani.
 
Asiye wajua CCm ndo ataamini kwamba si danganya toto!

Juzi (kwenye NIPASHE) nilishangaa jamaa Mniri(samahani kama nimekosea jina) alitoa taarifa kwamba CCM safi anashangaa vyombo vya habari vinavyo kichafua chama kwamba kuna rushwa?

Katibu makamba naye arikaliliwa akisema uchaguzi safi hakuna shida yoyote!

Huu ni mchezo wa siasa tu, asiye wajua CCM ndo aamini kwamba wana jisafisha. hapa ni kutafuta kudraw attention ya jamii tu lakini hamna lolote kwamba wanajisafisha, sana sana wanaandaa pesa kwa ajili ya rushwa itakayo wapa ushindi wa kishindo 2010 period.

No wonder kigugumizi cha upotevu wa mabilioni ya BOT na woga wa JK na serikali yake kuzungumzia mabilioni hayo yaliko elekea! Usikute yaliishia TAKRIMA!
 
Nadhani TanzaniaNjema ameleta changamoto nzuri sana kwa vyama vya upinzani. Kama nitakuwa nimemuelewa vizuri anachotaka kusema hapa ni kuwa kuna some changes ndani CCM ( Japo ndogo sana) katika suala zima la vita dhidi ya rushwa, kwa mtazamo wake kama wapinzani hawatajipanga vizuri ( na wao kusafisha nyumba zao) CCM itawapiga bao.

La msingi hapa ni kuifanyia kazi changamoto hii, badala ya kuanza kulaumu CCM kuwa ni danganya toto, dharau kama hizi zaweza kuwa na athari kubwa kwa ustawi wa upinzani.

We Masatu

Acha kunizulia mambo ati. Tanzania Njema amesema CCM inajisafisha kwa kuondokana na rushwa; mimi nisema katu asilani CCM ni ile ile yenye kukumbatia rushwa. Waanzie wapi kujisafisha ili hali wameingia kwa rushwa? Waanze wapi kujisafisha chamani wakati serikalini wanajichafua kwa rushwa? Waanze wapi kujisafisha chamani wakati chaguzi za chama mwaka huu toka chini zilikuwa na rushwa? Lakini wasema upinzani ujisafishe; lini upinzani umejichafua kwa rushwa kama CCM ili ujisafishe?

Msinitie vidole vya macho Asha mie. Nataka tu mnieleze nielewe, na mnanijua humu-nikielezwa nikaelewa huwa nakubali kuelewa.

Hivi Masatu nawewe CCM? Nishawishi basi nami nijiunge. CCM ya Kikwete ina lipi jipya?

Asha
 
jamani ebu nipeni tofauti ya UCHOCHEZI na KUHAMASISHA wananchi KUTETEA rasilimali zao,hawa kina manumba wametumwa na nani?

naona ni yale yale ya kina Nyerere na wakoloni,yaani hizi harakati za kina mbowe zinaleta woga na wasiwasi kwa ccm kama enzi zile za kudai uhuru na ccm sasa wanajiandaa kutumia silaha "YAO" ambayo wanacnhi WOTE huwa tunailipia kodi;POLISI
 
kama JK "ANAKERWA" na rushwa atueleze atafanya nini juu ya Kiwira,Buzwagi,BoT,radar,etc...kama yeye kaweza kuwanunua kina RAI na kina shoo et al na pia wakaweza kuwachafua wapinzani nwa ndani 2005,leo useme JK ANAKERWA na rushwa?Muungwana kwa sasa naona amebanwa kwenye cul-de-sac na HAJUI ajinasue vipi,kulia mtandano,kushoto TAKRIMA (sio rushwa) ndani ya ccm,mbele Buzwagi na karamagi,nyuma madai ya mishahara BORA ya wafanyakzi,chini BoT na balali,juu madai ya waislamu-BAKWATA-Manji...ah mengine mtamalizia...kwikwikwikwi!!!!
 
Alichosema Mwanri ni wajinga tu ambao wanaweza kuamini. Rushwa ndani ya CCM imeota mizizi, hiyo issue ya Arusha lazima itakuwa ni internal tussles za CCM, na kama ingekuwa ni CCM vs CHADEMA, sidhani kama ingeenda kokote. Kuonesheana vidole wenyewe kumesaidia kuthibitisha kuwa wanatoa na kupokea milungula.
Huu ni wakati mzuri wa opposition ku-capitalise kwenye issue hiyo.
 
Back
Top Bottom