Je, wapinzani ni wakombozi?

Je, wapinzani ni wakombozi?

hivi ule wimbo wa Kapteni(kada?)john Komba Unaosema "wapinzani tuwalete tuwachanechane tuwatupe" siyo wimbo wa kiuchochezi?
 
manumba bwana! watu walisema angalau hawa Said Mwema na Manumba kumbe ndiyo bure kabisa,hivi wanadhani tumesahau propaganda za Mahita na Mwenzake Adadi waliodai wamekamata Kontena la Visu vya CUF vilivyoletwa kwa ajili ya kuanzisha fujo na vita nchini. Hivi zama hizi za vifaa bora kabisa vya kijeshi ndiyo mtu aagize visu kwa ajili ya kufanyia fujo,sasa Manumba naye anakuja na UNUMBA wake!
 
hivi ule wimbo wa Kapteni(kada?)john Komba Unaosema "wapinzani tuwalete tuwachanechane tuwatupe" siyo wimbo wa kiuchochezi?

Komba anatakiwa akamatwe kwa UCHOCHEZI kwa wimbo wake huu..
 
We kaka,

Nani kukudanyanya CCM imekataa kuwa chaka la rushwa?

Wangekataa kuwa chaka la rushwa si wangeshughulikia RADA, IPTL, RICHMOND, BOT nk katika serikali yao?

Wamekaa vipi wakati rushwa imetolewa nchi nzima kwenye uchaguzi wa CCM kuanzia ngazi ya matawi mpaka wilaya mpaka sasa?

Nawe bwana, unakubali kufanyiwa usanii kwa kutumia tukio la Arusha?

Nyuma ya "Arusha" ni mapambano za rushwa za makundi ndani ya CCM na matokeo yoyote yale lazima kundi moja la rushwa ndio lishinde ati!

CCM ilichokifanya ni kuahirisha mjadala tu kwa sasa mpaka mahakama ifanya uamuzi mpenzi.

Lakini rushwa itadumu. Kidumu CCM

Rushwa ni alama ya ushindi, ilitumika kwenye uchaguzi mkuu kuwashinda wapinzani wa nje, sasa inatumika kuwashinda wapinzani wa ndani.

Wapinzani nao si vyema wakatoa rushwa? Pesa sabuni ya roho


Asha


Bibie kabla ya kukurupuka na mipasho yako soma uelewe mantiki ya posting yangu.

Mengine baadaye,

Tanzanianjema
 
mi nadhani uchochezi linamaanisha kwenda against the interests of watawala hasa wale wabadhirfu kama wa watz na anapotokea mtu kuwaamsha wanancnhi basi huyo anafnya uchochezi na ni hapo kina manumba et al come into picture...in other words CCM wanajitransorm kupia polisi kutisha watu wasiamshwe toka usingizini!!!
 
CCM wajue tusemepo ipo siku watu wataamka na kuelewa efisadi wao, basi wajue watu ndo wameanza kuamka. Kuwabana viongozi wa 'mwamsho'ni sawa na kuzima moto wa petroli kwa maji maana watatokea wengi wapya. Dawa ni serikali ya CCM kueleza kwa uwazi yale yote ambayo wananchi tunayalalamikia km uizi na matumizi mabaya ya ofisi ulofanywa na viongozi wa juu km Mkapa, BOT, nk. CCM wajue hamna atayelala kama maswala hayo hayajawa wazi. Na sana mpaka wananchi waone dalili nzuri za maisha, enzi za kuwaachia mnaiibia nchi mtakavyo imeisha. Kama huko ni kuvuruga amani na utulivu basi na iwe, kwani lengo ni kujiletea mawazo mapya na utendanji mpya ambao tunaamini utaleta amani, utulivu na maendeleo.Kwani nini serikali ikae kimya kwa fununu zote za uizi na ufisadi.
 
Mi nasema hapo kuna hatari langoni mwa CCM mabeki wamechanganyikiwa watajifunga sasa hivi.Subiri tuone hadi mwisho wa mchezo!
 
hii ni hatari tena kubwa kuona kuwa kushughulikia matatizo ni kuigawanya nchi vipande vipande
Kiongozi Upinzani ataka Kigoma ijitenge Tanzania



*Adai mkoa umetelekezwa sana katika maendeleo
*Wa CHADEMA ampinga akisema ni mawazo binafsi

Na Prosper Kwigize, Kigoma

MMOJA wa viongozi wa vyama vya Upinzani nchini, Mwenyekiti wa PPT Maendeleo mkoa wa Kigoma, Bw. Kasongo Ramadhan, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuuacha mkoa wa Kigoma uwe nchi huru kama itafika mwaka 2010 bila maendeleo mkoani hapa.

Akihutubia katika mkutano wa hadhara wa vyama vya upinzani ambao pia ulihudhuriwa na wana CCM kwa wingi, Bw. Ramadhan alisisitiza kuwa kuutelekeza mkoa huo ni kuukana kuwa sehemu ya Tanzania.

Alisema endapo CCM na Serikali yake hawatakuwa wamefanya chochote kuuletea mkoa wa Kigoma maendeleo hususan barabara, umeme na maji pamoja na kuboresha usafiri wa reli, itabidi wakazi wa Kigoma waombe kuwa Jamhuri huru.

“Tunakuomba Rais Kikwete kama utashindwa kuisimamia Serikali yako kutuletea huduma hizo za lazima, uwe tayari kutangaza kuwa sasa Kigoma si sehemu ya Tanzania nasi tuko tayari kujitawala wenyewe, angalau kwa miaka mitano tukimaliza tutakutana kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kigoma ikiwa huru na yenye maendeleo kuliko utung’ang’anie wakati huduma hatupati,” alisisitiza Bw. Kasongo.

Aidha, alisema viongozi wengi wa mkoana wa kitaifa wamekuwa na desturi ya kutoa ahadi zisizotekelezwa na wanapomaliza muda wao huwa hawatoi sababu za kukwama kunakotokea kwa Kigoma tu.

Alidai kuwa mwaka 1985 Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliwaahidi wakazi wa Kigoma kuwaletea mabati baada ya kubomoka kwa nyumba nyingi, lakini hakuna kilichofanyika hadi sasa.

Alisisitiza kuwa ahadi inayotolewa na Rais Kikwete ya kujenga daraja la Mto Malagarasi si ahadi ya awamu ya nne bali tangu Rais mstaafu Benjamin Mkapa, akiomba kuwa Rais wa Tanzania mwaka 1995 naye alitoa ahadi hiyo, lakini kwa miaka yake 10 hakuna alichoufanyia mkoa wa Kigoma.

Hata hivyo, licha ya Bw. Ramadhan kudai uhuru huo, Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Jafary Kaseseko, alikanusha kuwa hayo ni madai binafsi na si ya vyama vya siasa vilivyoandaa maandamano hayo.


Wakati huo huo, Muungano huo ulitoa mwito kwa wananchi wa mkoa huo kuikataa CCM katika uchaguzi ujao kwa kile ulichodai kuwa ni kushindwa kwa chama hicho kuiwajibisha Serikali yake.

Bw. Kaseseko aliitaka serikali itoe huduma muhimu za maji, barabara na umeme mkoani hapa.

Alisisitiza kuwa kutowajibika ipasavyo kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma kunakofanywa na Serikali ni ishara kuwa CCM imeshindwa kuiwajibisha Serikali yake chini ya Rais Kikwete.

Katika maandamano hayo yaliyoanzia katika ofisi ya CHADEMA Ujiji na kumalizikia katika uwanja wa Community Centre, Mwanga, viongozi hao walitaja kukerwa na utendaji kazi wa Serikali na kuwataka wananchi kuendelea kuandamana hadi huduma za maji na umeme zitakapotolewa.

Aidha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa walidai kuwa kutokuwapo kwa huduma za maji, barabara na umeme, sambamba na huduma mbovu ya mawasiliano ya reli kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma, ni moja ya mikakati ya kuutelekeza mkoa huo kiuchumi, kitamaduni na kisiasa.

Aidha katika risara ya vyama hivyo vya CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI na TLP, viongozi wa maandamano waliitaka Serikali mkoani Kigoma kumfukuza kazi Mhandisi wa Barabara wa Mkoa kwa kile walichotaja kuwa barabara ya Kigoma Ujiji inayojengwa na mkandarasi, haikidhi viwango na imesimama bila sababu.

Walimpa mwezi mmoja Mkandarasi wa barabara hiyo, Bw. Peter Mulima, kukamilisha ujenzi na kwamba asipofanya hivyo maandamano mengine dhidi yake yatafanyika kushinikiza ujenzi na ubora wa barabara hiyo.

Zaidi wa waandamanaji 1,000 wakiwa na mabango yaliyoandikwa kero hizo na lawama kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kigoma, waliandamana kwa amani huku wakiimba nyimbo zinazoonesha kilio cha wakazi wa mkoa huo.

Bendera za vyama karibu vyote ikiwamo ya CCM zilipeperushwa na waandamanaji hao kuonesha kuwa katika kero zinazoukabili mkoa wa Kigoma itikadi za vyama hazipewi nafasi zaidi ya wanavyama wote kutoa sauti moja ya kuitaka CCM iiwajibishe Serikali yake kwa kuuacha nyuma mkoa wa Kigoma.
 
Sio ndoto tu bali 'Kasongo yeye...!' nyimbo tu! Huyu Kasongo ana Uraia wa wapi?
 
Nafikiri Ramadhani Kassongo hakuwa akimaanisha kuigawa nchi 'per se', bali alikuwa akisisitiza Serikali ya CCM iuangalie Mkoa wa Kigoma kwa namna ya pekee. Katika maandamano hayo bendera za vyama vyote vya siasa vilivyoko Mkoani Kigoma, ikiwamo CCM, zilipeperushwa. Hii ni dalili tosha kuwa kila mwananchi wa Kigoma, bila kujali itikadi ya chama chake, amechoshwa na maendeleo duni ya Mkoa huo yanayotokana na ahadi hewa zinazotolewa na viongozi wakuu wa Serikali wakati wa kuomba kura. Sidhani kuwa kuna Mtanzania mwenye akili timamu anayeweza kufurahia nchi yake kugawanyika vipande vipande. Ni kweli Mkoa wa Kigoma umetelekezwa kwa muda mrefu, huu ni wakati wa Wanakigoma kusema NO! Shida ya maji, umeme, barabara, na miundombinu kwa ujumla vimeendelea kuwa kero isiyokwisha. Serikali iwajibike kwa hilo. Kigoma ni sehemu ya Tanzania pia.!!
 
Sio ndoto tu bali 'Kasongo yeye...!' nyimbo tu! Huyu Kasongo ana Uraia wa wapi?

Haya majina Kasongo, Nguza si wanatokea nchi jirani hapo mpakani...kazi kweli kweli, anataka iwe republic of Kigoma ama sehemu ya Zaire?

Huenda anaimanisha Kigoma imeachwa nyuma kwenye mtandao wa maendeleo Tanzania
 
Hata hivyo, licha ya Bw. Ramadhan kudai uhuru huo, Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Jafary Kaseseko, alikanusha kuwa hayo ni madai binafsi na si ya vyama vya siasa vilivyoandaa maandamano hayo.

Kumbe CHADEMA hawako kwa ajili ya kuigawa nchi ,kumbe PPT ndio wanafanya hiyo kazi.

Je?hii habari kuandikwa na kuwekwa front page ya majira ?
Je?chama ambacho kina diwani mmoja nchi nzima halafu mweyekiti wake wa mkoa fulani anasema kuhusu kuigawa nchi anawezekana kupewa front page?ama kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia?

Je?ni kuwa wapinzani ama ilipaswa kuwa PPT MAENDELEO.
 
Hata hivyo, licha ya Bw. Ramadhan kudai uhuru huo, Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Jafary Kaseseko, alikanusha kuwa hayo ni madai binafsi na si ya vyama vya siasa vilivyoandaa maandamano hayo.

Kumbe CHADEMA hawako kwa ajili ya kuigawa nchi ,kumbe PPT ndio wanafanya hiyo kazi.
Je?hii habari kuandikwa na kuwekwa front page ya majira ?
Je?chama ambacho kina diwani mmoja nchi nzima halafu mweyekiti wake wa mkoa fulani anasema kuhusu kuigawa nchi anawezekana kupewa front page?ama kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia?

Je?ni kuwa wapinzani ama ilipaswa kuwa PPT MAENDELEO.


Mpaka kieleweke,
Ni kweli mwandishi pengine alikuwa na jenda nyingine ndani yake.. ama kufifisha nia njema ya wanakigoma kwa ujumla kuhusu kilio chao kwa kutokumbukwa, ama hivo hvio nia ya kufifisha upinzani kama kichwa kinavo sema

Ila kwa msomaji makini.. message ya M/Kiti wa mkoa Chadema.. imeondoa sumu yote.. na kun'galisha zaidi muunganiko wa vyama vya ushindani!.. Kwa hapa, huenda amejipiga bao!

Bravo wana Kigoma.. endeleeni kuwaamsha! na pengine watanzania wote wataweza stuka kama nyinyi kwamba tulipo sipo tulipo paswa kuwa, je nani katufikisha?.. tumfanyeje?? 2010 ndiyo jibu!
 
Wapinzani kupambana na ufisadi zaidi - Zitto

na Irene Mark, Karatu
Tanzania Daima

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, amesema kuanzia mwaka ujao kasi ya kuwashughulikia mafisadi itakuwa kubwa kuliko mwaka huu, hivyo ni lazima Rais Jakaya Kikwete awawajibishe.
Zitto alisema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Karatu, mkoani Arusha.

Alisema kwamba hivi sasa kambi ya upinzani imepata silaha za kutosha kuangamiza mafisadi wa CCM, hasa katika sekta ya madini aliyoteuliwa kuwa mjumbe wa kamati hiyo.

Kuhusu ukuaji wa uchumi, Zitto alisema unakuwa katika sekta mbili - utalii na madini - huku akifafanua kuwa sekta hizo hazina manufaa kwa wananchi wa kawaida.

“Hivi sasa kambi ya upinzani imepata makambora ya kutosha kuwaumbua mafisadi wote,” alisema Zitto.

Zitto alibainisha idadi ya mikataba anayoifahamu hadi sasa kuwa ni sita, tofauti na awali kambi ya upinzani ilipokuwa ikifahamu mkataba mmoja tu.

Alisema hadi sasa amefanikiwa kuona mikataba sita ambayo hata hivyo awali hakuwahi kuiona.
 
FFU wasambaratisha kwa mabonu mkutano wa Wangwe

Na Samson Chacha, Tarime

ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wameusambaratisha kwa mabomu ya machozi mkutano uliokuwa umeandaliwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chacha Wangwe na kusababisha tafrani kubwa kwa wafanyabiashara na wateja waliokuwa wakifanya shughuli zao sokoni mjini hapa.

Tukio hilo lilitokea jana saa 8:00 mchana katika Uwanja wa Sabasaba mjini Tarime baada ya Wangwe ambaye pia ni Mbunge wa Tarime (Chadema) kutaka kuhutubia wananchi wa jimbo lake licha awali Jeshi la Polisi kuupiga marufuku mkutano huo.

Kutokana na tukio hilo, wafanyabiashara na wateja waliokuwa katika soko la mjini hapa, walikimbia ovyo na kutelekeza bidhaa walizokuwa wakiuza na walizonunua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, David Saibulu alimwambia mwandishi wa Mwananchi muda mfupi baada ya tukio hilo kuwa walilazimika kuchukua hatua hiyo kwa sababu za kiusalama.

Saibulu alisema hivi sasa nchi jirani ya Kenya inakabiliwa na machafuko, hivyo jeshi hilo haliwezi kuruhusu maandamano wala mikutano ya hadhara ili kuepusha yanayotokea humo kutohamia nchini hapa.

Awali, polisi hao walimzuia Wangwe kuhutubia mjini Musoma, hatua ambayo ililaaniwa vikali na Wangwe huku akidai kuwa lazima wafanye mkutano huo vinginevyo atalishtaki jeshi hilo kwa kuwatia hasara kutokana na gharama zilizotumika kuuandaa na kukiuka Katiba ya nchi inyaowapa wananchi uhuru wa kujieleza, kutoa na kupata habari bila kizuizi.

Hata hivyo, habari za awali zilieleza kuwa Wangwe katika mkutano huo alikusudia kuzungumzia kuhusu Sh25 milioni zilizotolewa na mgodi wa madini ya dhahabu wa North Mara kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi.

Katika fedha hizo ilielezwa kuwa kila kata ilipewa mgao wa Sh7 milioni za awali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza pekee, ambazo zimeanza kutumika.

Pia alikusudia kuzungumzia kuhusu vigogo wanane wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugawiwa uwanja wa michezo uliopo Tarime kujenga nyumba badala ya vibanda vya maduka kwa wananchi, kitendo ambacho kimezua mgogoro kwa wakazi wa eneo hilo na mchango wa Sh10,000 kila kaya kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.

Kabla ya tukio hilo, Wangwe aliwapongeza wanafunzi wa elimu ya juu kwa kufanikisha maandamano ya amani ya kupinga wizi wa kura na kulaani mauaji ya wananchi wananchi wasio na hatia nchini Kenya.

Akizungumza na umati mkubwa wa wananchi wa mji mdogo wa Sirari ulioko mpakani mwa Tanzania na Kenya waliokwenda kumpokea jana, Wangwe alisema maandamano hayo yanadhihirisha kuwa wapo pamoja na wananchi na vyama vya upinzani katika dhamira ya kukemea maovu yanayopinga demokrasia na haki za binadamu.

Wangwe alilaani hatua ya polisi ya kumzuia kufanya mkutano mjini Musoma akisema kwamba, kitendo hicho ni cha kuwanyima wananchi uhuru wa kuwasikiliza viongozi wao na kupata habari.
 
Nadhani kuna haja ya kuwapeleka mapolisi wetu shule ili wajue maana ya demokrasia. Mambo ya Wangwe yanahusiana vipi na yale ya Kenya?
 
Hawa askari sisi wananchi tunaweza tukawa tunawalaumu bure, let us look on the otherside of the coin.....hawa ni watu wanao amriwa kufanya jambo...hata kama hawapendi..amri inapotoka ni sharti watekeleze kama ilivyoamriwa..Sasa basi kuna vyanzo vyake ambavyo...ni baadhi ya vigogo waliopo madarakani ndo hasa hutoa order ili kuvuruga mipango ya wanasiasa wengine ili wao waendeleee kufaidi
 
Suluhu yanukia mgogoro wa ardhi Kawe
Na Mwandishi Wetu


MWELEKEO wa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ardhi ya shule iliyoko Kawe, jijini Dar es Salaam, umeanza kuonekana, baada ya Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Halima Mdee, kufanikiwa kuwashawishi wakazi hao kukubali kukutana na wapinzani wao kujadili suala hilo.


Wakazi hao walifikia hatua hiyo siku moja baada ya Mbunge huyo ambaye amejitolea kuushughulikia mgogoro huo, kukamatwa na kushikiliwa na polisi wa kituo cha Kawe kwa saa kadhaa Jumatano wiki iliyopita baada ya kuzuka mapigano ya kurushiana mawe kati ya makundi mawili ya wananchi wanaogombea ardhi hiyo.


Kati ya makundi hayo, moja linadaiwa kutumiwa na kigogo mmoja katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni anayetuhumiwa kumega sehemu ya ardhi hiyo ambako kumejengwa Shule ya Msingi ya Kawe ?B? na Shule ya Sekondari ya Ukwamani na kuwa uzia baadhi ya wafanyabiashara kinyume cha sheria.


Habari kutoka katika eneo hilo zinaeleza kuwa wakazi hao walikubali kukutana na wapinzani wao kwenye kikao maalum kati yao na mbunge huyo, kilichofanyika katika eneo hilo, Ijumaa wiki iliyopita.


Alipoulizwa na mwandishi wa Mwananchi mwishoni mwa wiki iliyopita, Mdee alithibitisha kuwa wakazi hao wamekubali kukutana na wapinzani wao.


"Kwa kweli mambo si mabaya. Tulikuwa na kikao cha pamoja jana (Ijumaa wiki iliyopita), tumekubaliana mambo kadhaa, ikiwamo kukutana na wavamizi na kuleta wapimaji, hivyo tunasubiri kuwasikiliza," alisema Mdee.


Mdee alisema wanatarajia kukutana na upande wa pili wa mgogoro Alhamisi wiki hii, huku wapimaji wakitarajiwa kufanya kazi hiyo leo.


Hata hivyo, wakati matumaini ya kupatiwa ufumbuzi mgogoro huo yakianza kuonekana, Mdee alisema jana kuwa anazo taarifa za kigogo huyo kuandaa baadhi ya vijana katika misikiti mbalimbali kwenda kufanya fujo katika kikao cha Alhamisi kwa madai kwamba mbunge huyo anatumiwa na viongozi Kikristo na Waislamu wasio na msimamo mkali kushughulikia mgogoro huo.


"Ni vitu vya ajabu kabisa. Hata hivyo, sitaacha kuwatetea wananchi wanyonge," alisema Mdee.
 
Ina maana kwa vile kwa jirani zetu kenye kuna vurugu, basi sisi tusifanye jambo lolote?

Nadhani muundo wa jeshi la polisi inabdi ubadilishwe, waingize wasomi zaidi na pia wapewe nafasi ya kutumia akili kuchambua mambo badala ya msuli kwa kila jambo!

Walichotakiwa ni kutoa ulinzi si kuwapiga mabomu! na hapo hawajui wanamuongezea umaarufu Wangwe wakidhani wana mmaliza!
 
Hii ni aibu kabisa na hawa polisi bado wako kwenye fikira kuwa wao ni walinzi wa mkoloni (mbwa wa bosi kama wakoloni walivyowaita).

Yaani polisi badala ya kulinda maslahi ya wananchi wao kila mara wamejiandaa na mabomu ya machozi tu kupiga wananchi wenzao!
 
Back
Top Bottom