Je, Watanzania kushangilia vita ya Ukraine na Russia kama mpira wa miguu ni mapungufu ya akili?

Je, Watanzania kushangilia vita ya Ukraine na Russia kama mpira wa miguu ni mapungufu ya akili?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Ukipita Facebook, Twitter, Instagram au kwenye usafiri wa umma utakuta watu wako wanabishana nani atakuwa mshindi na kufurahia kipigo anachokipata Mrusi au Ukrainian.

Je, ni umaskini wa akili au mali ndio hupelekea watu kushangilia mauaji?

Kuna uwezekano kama mbongo angemiliki nyuklia dunia ingepotezwa ghafla.
 
Ukupita Facebook, Twitter, Instagram au kwenye usafiri wa umma utakuta watu wako wanabishana nani atakuwa mshindi na kufurahia kipigo anachokipata Mrusi au Ukrainian.
Je, ni umaskini wa akili au mali ndio hupelekea watu kushangilia mauaji?
Kuna uwezekano kama mbongo angemiliki nyuklia dunia ingepotezwa ghafla.
Ehee wewe upande wako unasema gani???? Mbona hulii Wala hucheki Nini mbaya
 
Stori TU za kawaida mbona niko hapa na matajiri wenzangu ila tunajadili pamoja..nadhani dunia nzima watu wanajadili kwa sababu ndo trending stor kwa Sasa ukizingatia hatuna la uhakika lipi litatokea masaa 24 yajayo...au hujui km watu Wana nuclear la kuilipua dunia nzima tukose wote [emoji3]
 
Binafsi vita vile vinanisikitisha sana, kwani vitatuadhiri sana sisi raia wa Nchi maskini. Sitegemei kupungua bei ya mbolea 'inorganic' kwani Russia ndio mzalishaji mkuu wa ammonium duniani, na amesitisha kuuza nje, lakini chumi za Nchi tajiri zikiyumba adhari ipo kwenye mazao yetu kupata bei ndogo!
 
Hapo kinachoitesa Dunia ni uchumi tu...hakuna lingine.

Mnona hujasikia kelele za mamia wanaokufa Yemen,Syria,Palestina ,Nigeria nk

Eti raia wasio.na hatia Hao was Yemen wanak7fa sio watu!
 
Sio watanzania tu. Saivi ndio habari ya town dunia nzima. We jifanye tu uko dunia ya pekee yako wala hamna shida...!
 
Haya mambo ya ushabiki hayajaanza leo

Vita zote wabongo huwa wanashabikia+ U-team ndani

Ova
 
Mnazijadili Urusi na Ukraine kama timu za mpira wa miguu au kama watu wazima wenye akili timamu?
Stori TU za kawaida mbona niko hapa na matajiri wenzangu ila tunajadili pamoja..nadhani dunia nzima watu wanajadili kwa sababu ndo trending stor kwa Sasa ukizingatia hatuna la uhakika lipi litatokea masaa 24 yajayo...au hujui km watu Wana nuclear la kuilipua dunia nzima tukose wote [emoji3]
 
Ukupita Facebook, Twitter, Instagram au kwenye usafiri wa umma utakuta watu wako wanabishana nani atakuwa mshindi na kufurahia kipigo anachokipata Mrusi au Ukrainian.

Je, ni umaskini wa akili au mali ndio hupelekea watu kushangilia mauaji?

Kuna uwezekano kama mbongo angemiliki nyuklia dunia ingepotezwa ghafla.
Nafikiri ww ndio mjinga na mpumbafu wa akili.Watanzania sio kwamba wanashangilia hiyo vita,Bali wanafuatilia tu kwa ukaribu.

Utakumbuka hata vita yetu na Uganda ,namkumbuka baba na ndugu zangu wakubwa walikuwa wanafuatilia kupitia redio mkulima.

Utasikia BBC na sauti ya ujerumani wakiongea kwa mbwembwe.Kwamba leo vikosi vya Tanzania vikiwa na vifaru vyenye mizinga vimeiteka Entebe.Mwaka 1990 Sadam Hussein alipoivamia Kuwait taarifa za BBC na VOA na Sauti ya ujerumani zilikuwa nyingi pia.

Mwaka 2003 pia vita ya USA na Iraque ilikuwa gumzo.Kabla ya hapo vita ya Iran na Iraque pia ilikuwa gumzo duniani.Vita ya siraha za sumu.Vita ilipiganwa miaka nane.Bomu linapigwa mtu anaoza dak moja.Vita ya USA na Libya pia ilikuwa moto.

Wewe unasema wanashangilia au wanafuatilia kujua mshindo ni yupi.Inaonekana haujui kabisa Mambo ya vita.
 
Kufanya ushabiki kama wa Simba na Yanga au comedy kuhusu raia wanaouwa vitani ni upumbavu.
Haya mambo ya ushabiki hayajaanza leo

Vita zote wabongo huwa wanashabikia+ U-team ndani

Ova
 
Ukupita Facebook, Twitter, Instagram au kwenye usafiri wa umma utakuta watu wako wanabishana nani atakuwa mshindi na kufurahia kipigo anachokipata Mrusi au Ukrainian.

Je, ni umaskini wa akili au mali ndio hupelekea watu kushangilia mauaji?

Kuna uwezekano kama mbongo angemiliki nyuklia dunia ingepotezwa ghafla.
Mbona wao walishangilia mauaji ya Kimbari Rwanda, kwa miezi mitatu watu wanachinjwa kama kuku, uliona Mataifa yenye nguvu duniani yakiingilia kuzuia?
 
Back
Top Bottom