Je, Watanzania kushangilia vita ya Ukraine na Russia kama mpira wa miguu ni mapungufu ya akili?

Bila shaka wewe unaumwa sonona.
Kuna kufuatilia na kuna kushangilia.
Huko mitandaoni kuna memes nyingi za dhihaka na kushangilia hii vita.
 
Acha ushamba,hata huko G7,G20,story ni Russia vs ucraine war.sasa usijifanye ww ni smarter sanaaaa!! Kuliko hao waliowqchonganisha!!
 
We ndio haupo sawa kabisa.Huo ni utani wa kawaida tu wa maisha.Yaan unataka kutufanya wote tuwe na matatizo ya akili Kama uliyonayo.Yaan watu wasifanye utani kwa kuwa Kuna vita.Ondoka kwenye akili mgando ,utaugua akili si muda mrefu.
 
Mbona mnawasiwasi kwani kushapikia league ya Europe ni upungufu wa akili?? vita vinapiganwa ushabikie usishabikie vinapigwa hivyo acha watu wazungumze kuimarisha afya ya akili
 
Wa TZ ni moja ya watu wa ovyo kabisa kwenye ulimwengu
 
Unaelewa kwamba Rwanda walikuwa wanachinjana wao kwa wao kwa sababu za kijinga kama mmoja ana pua ndefu na mwingine fupi? Umoja wa Africa na Jumuiya ya Africa Mashariki walikuwa wapi wakati ndugu zao weusi kama wao wakichinjana kama kuku mipakani mwao?
Mbona wao walishangilia mauaji ya Kimbari Rwanda, kwa miezi mitatu watu wanachinjwa kama kuku, uliona Mataifa yenye nguvu duniani yakiingilia kuzuia?
 
kama kuna kijana wa kiume umri wako,anafurahia kifo cha jpm!!!unashangaa kufurahia vita ukrain???

kuna vichaa wengi taifa hili.
 
Serikali ya Tanzania haijwahi kuipa uzito unaostahili suala la afya ya akili kwa raia ila ni wakati sasa kuwekeza kwenye eneo hilo kabla hatujageuka kuwa taifa la mzaha na kuchekelea kila kitu kila wakati.
 
Watu wanataniana mpk msibani haswa kwa watani zake sembuse huko nchi za mbali ?

#PuttinAnaupigaMwingi
 
Hata hao wazungu si wanauana wao kwa wao au? Sasa katika nchi za Afrika zinazokosa hata bajeti ya kuwalipa walimu mishahara kuna mtu atatenga bajeti ya kwenda kupiga vita ya ghafla?

Ni tofauti na hizo zinazojiita dunia ya kwanza, ambao waliingia Libya na Iraq kwa mbwembwe.

Hata Iddi Amini alivyotuvamia, uliona nchi yenye nguvu duniani hata 1 ikija kutusaidia? Sana sana walichekelea tu.
 
Kwani umesikia wazungu wakiitaka dunia ya tatu kuingilia kati.
 
Kwani umesikia wazungu wakiitaka dunia ya tatu kuingilia kati.
Kwani nimesema wazungu wanataka tuingilie kati? Nilichosema ni kitendo cha wao kuwa na uwezo wa kuzuia mauaji Rwanda (kijeshi na kiuchumi) lakini bado wakachagua kutofanya hivyo ndio kitendo cha kuchekelea kwenyewe huko. Legeza ubongo kwanza.
 

Pamoja na Potash, Russia anaexport karibu 20%. (Potash facts)

Hakika tutakiona. Tayari Bei za mbolea zilikuwa juu, ongezea na hili la vikwazo tatizo linakuwa kubwa. Wachina watakuja kununua mahindi hapa, subiri uone.
 
Vyombo vya habari vyote Duniani habari ndo hiyo ya Ukreine na Rusia,tena vyombo vingine vikubwa vinatoa habari kishabiki kama Simba na Yanga.sisi nani iwe hajabu kwetu.
 
Ni dalili ya udumavu wa akili😀😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…