H r n
JF-Expert Member
- Oct 3, 2019
- 1,100
- 2,079
Watanzania wengi wanakula kwa ajili ya kushiba, si kwa ajili ya afya. Nimegundua watu wengi huangalia chakula kwa lengo la kushiba tu bila kujali virutubisho au athari zake kiafya. Mara nyingi tunachagua chakula kwa bei nafuu, ladha au wingi wake, lakini si kwa ubora wake kiafya.
Matokeo yake ni kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, presha na unene uliopitiliza. Je, tatizo ni ugumu wa maisha, ukosefu wa elimu ya lishe, au ni mazoea tuliyoyazoea kwa muda mrefu?
Wenzangu, mnaonaje hoja hii?