Wewe ndiye uache uwongo. Sensa ilikuwa inachukua siku moja tu tangia mwanzo. Ilikuwa inafanyika siku ya jumapili, wananchi wakiwa mapumuziko. Enzi za Ngoswe walitumika wanafunzi wa sekondari wakiambatana na mabalozi wa nyumba kumi. Baadaye hadi 2012 wakawa wanatumika waalimu wakiambatana na mabalozi wa nyumba kumi. Ya mwaka huu wametumia vijana waliokosa ajira (jobless) wakiwa peke yao wakitumia vishikwambi, wametumia siku saba lakini mamilioni ya watanzania wameshindwa kuhesabiwa. Tulitegemea hivyo vishikwambi (digital) vingaliwezesha kazi hiyo kufanyiwa faster lakini matokeo yake imekuwa mwendo wa konokono.
Usitake kubisha. Mimi nilikuwa karani wa sensa enzi hizo za Ngoswe na Mazoea, nayafahamu sana mambo haya. Hata mama Makinda anayajua vizuri kwani naye alikuwepo enzi hizo.