Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Kwa nchi yetu Tanzania vipigo kwa watoto inaonekana ni jambo la kawaida sana, na huku baadhi wakipongeza jambo hilo kwa kuona ndio msingi bora wa malezi kwa watoto unaowafanya kuwa na maadili, hofu, kusikiliza na kutekeleza maagizo ya wazazi aidha kwa kutaka au kutokutaka kwa kuogopa kuadhibiwa kwa vipigo.

Kuna baadhi wamekuwa wakijisifu kuwa wao hawacheki na watoto kwani wao ni fimbo mkononi huku wakirejea maandiko kutoka kwenye vitabu vya dini kuwa Usimnyime mtoto mapigo na hivyo kuona kaaa walipewa ruksa ya kuwadunda watoto vilivyo kutoka kwa Muumba wao.

Hali hiyo imekuwa ikifanya watu wanaolea watoto bila kuhusisha vipigo kutuhumiwa kuwa wanawaharibu watoto, wanawadekeza na kwamba wanafata utamaduni wa wazungu ambao hauwezi kufanya kazi kwa watoto wa kiafrika hususani Watanzania, Wazazi wa aina hiyo wamekuwa wakituhumiwa kuzalisha watoto watakaokuja kuwa wa ovyo wasio na maadili wenye matendo mabaya.

Je, watu wote wasio na maadili waliopo ni zao la wazazi ambao hawakuwapiga watoto wao?
Je, hakuna watoto waliopigwa na hawakuwa na maadili licha ya vipigo vikali?

Ni kweli kipigo ndio suluhisho la maadili na usikivu kwa watoto?
Ni kweli hakuna watoto wanaolelewa bila vipigo na kuja kuwa watu wema?

Pamoja na yote wanaosifu vipigo kwa watoto huwa hawataki kabisa kuzungumzia athari hasi ya vipigo hivyo kwa watoto, na pengine hawatambui kuwa zipo. Je, hakuna namna ya kuweza kuwalea watoto bila kuhusisha vipigo?

Pia soma: Je, ni kweli Adhabu ya Viboko inasaidia kuongeza Nidhamu na Uelewa kwa Mtoto?
 
Sisi wa africa bila kunyukwa hatuendi jamii nyingi tunazotamani kuziiga nao wana mambo yao ya ajabu , sio kitu cha ajabu watoto wakizungu kuwaambia wazazi wao wanavutiwa na mahusiano ya jinsia moja na kwao ni kawaida tu.

Mda mwingne tusipuuze desturi zetu na kuiga za watu ambazo kiundani zina madhara yake pia.
 
Watoto wengi waliolelewa Kwa vipigo hawana maadili . wazazi wale wakali , wazee wakufoka foka wametoka 0-0 hawajafanikiwa kuandaa kizazi bora

Kuna njia za kulea mtoto ambazo zinaweza kumfanya akawa na Utii. Heshima na maadili mazuri.


Mtoto mfanye awe na usikivu mzuri na mpatie na EI
 
Nakukumbusha tu usiisahau asili yako. Maisha yetu Afrika tunayo namna ya kumlea na kumuongoza mtoto katika njia sahihi itakayo msaidia mbele ya safari katika maisha yake yajayo. Kumkanya mtoto kwa kiboko sio jambo baya na halitawahi kuwa baya endapo mzazi anajua namna ifaayo kutoa adhabu.

Leo hiki kizazi cha kina Junior tunaona namna kinavyoumiza kichwa sababu ya wazazi wengi kuacha misingi yetu ya malezi na kuiga kwenye tamthilia za kizungu namna mpya ya malezi. Wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, kama kwako unaona kumpa maonyo mtoto yaambatanayo na kiboko ni malezi mabaya, endelea kufuata hiyo njia yako.

Uzuri kama MUNGU ataendelea kutuweka hai na kila mmoja akashuhudia matunda ya malezi ipo siku tutaongea lugha moja.
 
baba junio hayo si malezi
Hapana Mama Kayumba.

Ni vile tu mtoto unamlea tangu mwanzo, mimi na mwanangu, tutacheza, tutataniana lakini kuna sura flani nikiiweka, ni heshima nyumba nzima mpaka mama yao.

Hata mama yao akikosea, onyo huwa anapewa mbele yao(sio kila kesi) na huwa anaufyata kimyaaaa

Ukikosea zaidi ni adhabu ila sio kunyanyua mkono kukupiga.

Kuna njia nyingi sana za kumuadhibu mtoto, hata mama yao pia unaeza kumuadhibu vile vile ila sio kupiga

Hiyo inawajenga watoto kuwa na heshima.
 
eeeh wewe lea hivohivo ipo siku yako wataenda watazoea hiyo sura utakuja na mbinu gani
 

Mkuu viboko havisaidii chochote Ila vinaleta utulivu wa muda
 
Ahsante Sana kwa mada yako. Ndiyo Iko x usiku kucha jana na inaendelea.

Naongezea; tuna wazee wengi hawatunzwi na watoto wao waliowachapq Sana kwa madai ya kuwatengeneza. Je hii siyo MOJAWAPO ya athari ya mpasuko wa mahusiano ya watoto na Wazee ? Kwamba nguvu kubwa ilitumika kuumiza mwili badala ya ku transform akili ya ndani ya mtoto? Sasa mtoto kawa mkubwa, Tabia zake zilizokandamizwa kwa hofu ya kipigo, sasa zinaanza kushamiri na kumea maana hakuna wa kumpiga tena?

Nini maoni yenu?
 
kwa hyo unataka kuniambia viongozi wa serikali wanaoiba hela za umma hawakuchapwa udogoni? Asilimia 80 ya watanzania maadili yetu ni mabovu licha ya kuchapwa sana fimbo udogoni wengi wetu ni wezi, wachepukaji. Sio wastaarabu na tabia nyinginezo za ovyo

Mi ukiniuliza km fimbo zimetusaidia kwenye suala la maadili ntakujibu zimefeli pakubwa sababu wengi wetu zimetufanya tuwe na nidhamu ya uoga. Tunaonyesha nidhamu mbele ya wazazi ila tukiwa pekee yetu tunafanya mambo ya ajabu
 
Kweli Baba JR viboko Mimi naona havisaidii chochote.
 
sio kua mtoto anapigwa kila dakika au kila kosa, kuna kosa unaona kabisa hapa bila kumkanda huyu hatutasikilizana vizuri ili iwe wakat mwnegine akikosea ukimwambia anaelewa, ukimlea mtoto akakosea ukawa unasema tu ntakupiga ntakuchapa utanitambua huyu anakua anajua huna cha kumfanya zaidi ya maneno matupu kiboko sometimes ni kizuri.
 
Unaweza kutusaidia kupata data iwapo zipo za athari walizopata watoto baada ya malezi ya vipigo?
 
Hizo nchi ambazo watoto hawachapwi zina mmonyoko mkubwa wa maadili pia ,sisi tunajiona hatuna maadili ila ukitembelea kwa wenzetu utaona bado sisi tuna maadili sana😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…