Kwa nchi yetu Tanzania vipigo kwa watoto inaonekana ni jambo la kawaida sana, na huku baadhi wakipongeza jambo hilo kwa kuona ndio msingi bora wa malezi kwa watoto unaowafanya kuwa na maadili, hofu, kusikiliza na kutekeleza maagizo ya wazazi aidha kwa kutaka au kutokutaka kwa kuogopa kuadhibiwa kwa vipigo.
Kuna baadhi wamekuwa wakijisifu kuwa wao hawacheki na watoto kwani wao ni fimbo mkononi huku wakirejea maandiko kutoka kwenye vitabu vya dini kuwa Usimnyime mtoto mapigo na hivyo kuona kaaa walipewa ruksa ya kuwadunda watoto vilivyo kutoka kwa Muumba wao.
Hali hiyo imekuwa ikifanya watu wanaolea watoto bila kuhusisha vipigo kutuhumiwa kuwa wanawaharibu watoto, wanawadekeza na kwamba wanafata utamaduni wa wazungu ambao hauwezi kufanya kazi kwa watoto wa kiafrika hususani Watanzania, Wazazi wa aina hiyo wamekuwa wakituhumiwa kuzalisha watoto watakaokuja kuwa wa ovyo wasio na maadili wenye matendo mabaya.
Je, watu wote wasio na maadili waliopo ni zao la wazazi ambao hawakuwapiga watoto wao?
Je, hakuna watoto waliopigwa na hawakuwa na maadili licha ya vipigo vikali?
Ni kweli kipigo ndio suluhisho la maadili na usikivu kwa watoto?
Ni kweli hakuna watoto wanaolelewa bila vipigo na kuja kuwa watu wema?
Pamoja na yote wanaosifu vipigo kwa watoto huwa hawataki kabisa kuzungumzia athari hasi ya vipigo hivyo kwa watoto, na pengine hawatambui kuwa zipo. Je, hakuna namna ya kuweza kuwalea watoto bila kuhusisha vipigo?
Pia soma:
Je, ni kweli Adhabu ya Viboko inasaidia kuongeza Nidhamu na Uelewa kwa Mtoto?