Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

Kupiga mtu yeyote yule(hasa asie na uwezo wa kukurudishia) ni hatua ya juu kabisa ya uonevu.

Jiulize, wewe ukikosea, ni nani huwa anakupiga?
Si kweli.Mimi nilikuwa nabondwa kama wanaua lakini leo sijutii kupigwa kule.Kwa akili zangu ningekuwa nunda sana.Kuna muda kipondo ni muhimu kwa watukutu.Watoto wangu wa kike wote waoga.Wakileta utukutu nikifoka tu wanabadilika.
 
Sijawahi kuwapiga watoto wangu kwa sababu nimepigwa sana na ninaona kuna wakati nilikuwa napigwa hata nikitoka kucheza mpira
Hayo walikuwa wanafanya wazazi kudhani kuwa tutakuwa na nidhamu
Ila wengi waliharibika mpaka kuwa nunda, hata mimi nina watoto wakubwa na wengine wamemaliza vyuo ila wananipa heshima ya hali ya juu na upendo juu
Sina mtoto mwizi wala muongo kwa sababu nimewafundisha kama nilivyofundishwa ila bila fimbo

Najua kuna wazazi humu wanaona kupiga ni njia rahisi ya kumnyamazisha mtoto
Jamani hata mbuzi wadogo huwa wanakimbia kimbia wakiwa wadogo
Watoto wakicheza tushukuru Mungu wana afya njema na wanahitaji michezo
Kuna mwanangu alivunja kikombe alishtuka sana nikamwambia kaa mbali na hapo na ni ajali usijali
Sasa ukute mwingine atapigwa siku nzima na hata baadae haombwi msamaha kwa hasira za kijinga
Kikombe tu unamtoa mpaka damu mtoto daa
Wanangu wanalala wakiwa na furaha na lazima nihakikishe hilo
Na wakitoka shule ni kuwapokea kwa heshima bila maswali mengi hujui wamepata nini huko shule na pia wamechoka

Nakuomba uwaelimishe sana wanaopiga badala yake kuwa karibu na kuwafundisha
Usiishie tu kuandika blah... Blah hapa na kujizolea misifa kwa Hawa wazazi wenzio wa kisasa.

Hebu elezea kinaga ubaga umeweza vipi kuwafanya watoto wako kuwa na hiyo discipline ya Hali ya kujua kiasi kwamba wanajua kwamba hili ni kosa, hivi ni sahihi bila kuchapwa hata mara moja udogoni kwao?

Au which convenient approach did you employ to instill discipline to your children such that today intelligently they have become way better than those ones who were raised under the so-called corporal punishment ??? And furthermore what disciplinary actions were you taking against them everytime they misbehaved?
 
Kuna familia watoto walikua hawaguswi mama ndo alikua house maid..wtt hta glass wakinywea maji wanaacha maam ndo anatoa kisa baba alikuwa anawakingia vifua..hela ipo wtt maisha ya geti kali japo sio kali kiviilee...ndani ya room ya boys wamewekewa kompyuta kwa ajili ya game..

Kilichotokea hapo wtt wamekua wa ajabuuu hakuna mfano baba hana kazi tena amestaafu mtoto wa kiume mmoja anataka ajiue kisa anasikia sauti zinamwambia hivyo..wa kiume mwingine alidisco udsm hajarudi tena...yupo kazalisha binti wtt wawili chap chap...binti mwingine hana socalization kabisa yani hata mgeni uje hatoki kukusalimia kazalia home nasikia baba mtoto ni mpiga debe...sijui hata alimpataje sio kwa kiburi kile...

So nachotaka kusema sisi tuliolelewa kwa viboko tulinyooka na tumenyooka mpk leo..na tupo discplined hata katk maisha ya kawaida...kikubwa kubalance upendo uwepo mkubwa kuliko kichapo...
 
Kuna tofauti ya kumlea mtoto Kwa kutomchapa na kumdekeza, sisi tunawadekeza watoto.
Kuna familia Moja niliitembelea mwaka Jana, nilikaa pale na wenyeji wangu ambao ni baba na mama wenye mji ule mpaka mida ya usiku.

Sasa Wakati tunapiga nao story waliokuwa wameweka channel ya Katuni ambapo mtoto wao wa kike mwenye umri wa miaka 4 alikuwa Yuko bize anaangalia...

Ilivyofika mida ya taarifa ya habari nikawaambia wabadilishe channel waweke ITV, mara mama mtu akaniambia huyu atatusumbua sana nikamuuliza huyu nani?? Na atatusumbua vipi? Akaniambia mtoto wao yule tuliyekuwa nae pale sebuleni ndio atatusmbua... Kwa maelezo ya mama mtu akasema akiwaga anaangalia Katuni huwa wanamuachia tu mpaka atakaposinzia mwenyewe, wakibadilisha channel huwa analia sana na wanashindwa kumnyamazisha..

Kiukweli nilipatwa na hasara sana ila nikajikaza tu, na of course niliwadharau sana ile familia yaani mtoto wa miaka minne mnamdekeza mpaka anawatawala nyumba nzima mnaishi kwa kufuata matakwa yake.
 
Hawajui kuwa lazima mipaka iwepo.
 
Kuna kliniki za watoto watundu na watukutu. Utakuja umuumize bure na sisi tuje na hii hapa 👇
My dear minister yaani una maanisha kwamba mtoto wangu ametemea mate chakula Cha mgeni aliyekuja kunitembelea, halafu eti Mimi nimchukue nimpeleke kwenye hizo clinics Tena kwa kulipia pesa zangu hili wabaini ni kwanini ametemea mate chakula Cha mgeni??????
 
Hawajui kuwa lazima mipaka iwepo.
Wapuuzi tu na uzungu uchwara walionao.

Wenzetu wa Asia wanawaiga wazungu technology, halafu mambo mengine kama tamaduni zao n.k wanawaachia kiasha Wao wanabaki na tamaduni zao za kiasia.

Njoo kwetu sisi huku ngozi nyeusi Sasa, yaani mambo muhimu kama technology na uchumi tumeshindwa kuwaiga, ila kuchukua tamaduni zao na kuzifanya ziwe zetu ndio tumeona jambo la maana sana licha ya umasikini mkubwa tulionao usioendana kabisa na hizo tamaduni za kizungu.

Eti unakuta mtoto anakataa kwenda shule halafu mzazi ana mbembeleza hapo hata masaa mawili hili akubali kwenda shule si ujinga huo..!!
 
My dear minister yaani una maanisha kwamba mtoto wangu ametemea mate chakula Cha mgeni aliyekuja kunitembelea, halafu eti Mimi nimchukue nimpeleke kwenye hizo clinics Tena kwa kulipia pesa zangu hili wabaini ni kwanini ametemea mate chakula Cha mgeni??????
Huyo Waziri si anaongea hivyo ili mshahara uingie kwenye account yake. Kwenye field mambo ni tofauti.
 
Usiishie tu kuandika blah... Blah hapa na kujizolea misifa kwa Hawa wazazi wenzio wa kisasa.

Hebu elezea kinaga ubaga umeweza vipi kuwafanya watoto wako kuwa na hiyo discipline ya Hali ya kujua kiasi kwamba wanajua kwamba hili ni kosa, hivi ni sahihi bila kuchapwa hata mara moja udogoni kwao?

Au which convenient approach did you employ to instill discipline to your children such that today intelligently they have become way better than those ones who were raised under the so-called corporal punishment ??? And furthermore what disciplinary actions were you taking against them everytime they misbehaved?
Asante kwa kuendeleza mjadala ila umeanza na ukali kidogo anyway kwa mimi hainisumbui sana

Unajua kuna disciplined aina nyingi na kupiga ni last option
Kumuadhibu kwa mangumi au makofi ya nguvu au fimbo za hasira yote sio nzuri na hiyo ndio napinga kabisa kwa nguvu zote
Lazima ujue binadamu wote ni tofauti kuna wengine hawajawahi kuwapiga watoto nina maana baina ya wazazi
Unakuta anaewadhibu ni mama na baba hapigi kabisa au kinyume
Kwa mimi siwapigi wanangu bali naongea nao sana
Who wana utundu wa kitoto ambao watoto wote wanafanya lakini nikiwaambia sasa ni mda wa kulala huwa hakuna ubishi na nimejaribu kuwalaza mda huo huo kila siku mpaka wamezoea na ukiwaacha ikifika mda utaona wana sinzia
Kuna wakati natoka nao na kwenda kutembea nao hata say Lisaa limoja na nusu au mawili tukirudi wamechoka
Sioni kitu kikubwa wanachofanya mpaka niwapige kipigo kikubwa hapana
Watoto ni kuwakataza mabaya na kuwafundisha mema kila wakati
Nacheza nao na sio kwamba eti mimi niko serious kila saa hapana
Nawanunulia toys zaidi na vitabu vingi pia rangi za kuchora na hata baiskeli zao kwa kila mmoja na weekend nawapeleka farm ambapo tutakuwa na lunch huko na watacheza na jioni kurudi
Sasa niambie unampiga kwa kosa lipi au mradi nipige tu
Sio waizi, hawatoki nje bila ruhusa na huwezi kuwakuta wanazurura hovyo nje kwa sababu wana vitu vingi vya kufanya na hata kuchezea nyumbani
 
Kuna nchi duniani zimeondokana na adhabu ya kuwachapa watoto iwe shuleni au nyumbani. Yaani ukimchapa mtoto ni at your own peril. Na hii inatokana na studies mbalimbali kwamba kumpiga mtoto ni ku'induce' violence kwenye hisia zake ili na yeye akikua aweze kuwa 'violent'. Ndiyo maana watoto ukiwaacha pamoja utaona baadhi yao ni wapole, lakini wengine ni violent - wanapenda kuwapiga wenzao, kunyakua vitu vyao au kuziharibu bila sababu. Binafsi najiepusha sana kuwapiga watoto wangu, na ikitokea nimewapiga huwa najisikia vibaya sana na hata huwa nawaambia radhi kwa kuwapiga. Kwa kifupi, I hate beating children na nikimwona mtu anayepiga au anayeshabikia kupiga watoto namdharau sana. Kutumia nguvu kunanyesha kutumia akili kidogo na kutumia akili nyingi kunionyesha kutumia nguvu kidogo. Hivyo, mtu anaweza kujipima kuona je katika malezi ya watoto, anatumia akili au nguvu?
Haya ndugu mwelevu naona umetoa maelezo meeengi ambayo hayajagusia hata kiini Cha mada, yaani umeandika ujinga wa kuiga ule ule kama wenzako wanaofanana na wewe kimtazamo.

Sawa hatutakiwi kuchapa watoto wetu hili tusi induce hizo violence kama unavyosema, haya ni njia ipi Bora ya kukabiliana na watoto ambao tayari ni watukutu na wasiokuwa na adabu??? Yaani hapa nazungumzia wale watoto ambao ukiwakataza kitu hawaskii kabisa wakina Brighton sijui Carleen(kama mnavyowaita), njia gani zitumike au ndio tuwapeleke kwenye hizo clinics za malezi wafundishwe adabu na specialists wa watoto kama anavyosema Mhe.Gwajima hapo????
 
Asante kwa kuendeleza mjadala ila umeanza na ukali kidogo anyway kwa mimi hainisumbui sana

Unajua kuna disciplined aina nyingi na kupiga ni last option
Kumuadhibu kwa mangumi au makofi ya nguvu au fimbo za hasira yote sio nzuri na hiyo ndio napinga kabisa kwa nguvu zote
Lazima ujue binadamu wote ni tofauti kuna wengine hawajawahi kuwapiga watoto nina maana baina ya wazazi
Unakuta anaewadhibu ni mama na baba hapigi kabisa au kinyume
Kwa mimi siwapigi wanangu bali naongea nao sana
Who wana utundu wa kitoto ambao watoto wote wanafanya lakini nikiwaambia sasa ni mda wa kulala huwa hakuna ubishi na nimejaribu kuwalaza mda huo huo kila siku mpaka wamezoea na ukiwaacha ikifika mda utaona wana sinzia
Kuna wakati natoka nao na kwenda kutembea nao hata say Lisaa limoja na nusu au mawili tukirudi wamechoka
Sioni kitu kikubwa wanachofanya mpaka niwapige kipigo kikubwa hapana
Watoto ni kuwakataza mabaya na kuwafundisha mema kila wakati
Nacheza nao na sio kwamba eti mimi niko serious kila saa hapana
Nawanunulia toys zaidi na vitabu vingi pia rangi za kuchora na hata baiskeli zao kwa kila mmoja na weekend nawapeleka farm ambapo tutakuwa na lunch huko na watacheza na jioni kurudi
Sasa niambie unampiga kwa kosa lipi au mradi nipige tu
Sio waizi, hawatoki nje bila ruhusa na huwezi kuwakuta wanazurura hovyo nje kwa sababu wana vitu vingi vya kufanya na hata kuchezea nyumbani
Nimekuelewa baba Jefferson hongera kwa kujitahidi kusimama kama baba wa kisasa, ila huoni kwamba aina hiyo ya malezi ni exclusive?

Yaani ni wazazi ambao wako njema kwenye suala Zima la financial affordability na hakuna haitaji lolote la mtoto linaloweza kuwasumbua, Kila haitaji kwao linawezekana hili kuwafanya watoto wao wawe bize muda wote kwa kufuata ratiba uliyowapangia.

Na Zaid ya hapo wawe na muda wa kutosha na watoto wao kwa kipindi chote Cha utoto wao, kwa sababu unapokuwa nao mara kwa mara ni rahisi kuwafuatilia patterns zao za ukujaji na kubaini Kila dosari inayojitokeza na kukabiliana nayo bila kutumia nguvu hata kidogo....

Sasa ni wazazi wangapi wa kitanzania wenye uwezo wa kifedha hili kuwapa watoto wao aina hiyo ya malezi? Na pia ni wangapi wenye muda na watoto wao angalau masaa 5 kwa siku?? Wazazi wengi wa kibongo wanategemea daily income waweze kuishi wao na watoto wao.

Na pia vile vile hebu nipe mawazo yako ni Njia ipi rahisi ya mzazi mwenye kipato Cha kawaida kukabiliana na mtoto ambaye tayari ameshakuwa ni mtundu,mkorofi na asiyekuwa na adabu hata kidogo.
 
Mwanamke
Ukizungumzia kina mama hapo nakubaliana na wewe kabisa. Wengi ni wakatili hasa wale waliozalishwa bila kuolewa na kisha kuachwa wahangaike na watoto huwa wana uchungu sana wa kuachwa hasira wanamalizia kwa mtoto.
Mwanamke aliezalishwa na kutelekezwa yeye pamoja na kiumbe wao ni zaidi ya Damaged goods, hata gundi ya mchirizi wa dhahabu haiwezi rekebisha ni rehma za Mungu tu.

Mbaya zaidi jamii yetu haitambui wala kuamini katika kutibu madonda ya roho bali tunaamini katika kuwananga victims na kuwa praise wakosefu.

It's a sad fact lakini Kwa majibu haya ndani ya mada hii tena inayohusu Watoto , it’s a proof beyond any (reasonable?!) doubt kwamba jamii yetu imejaa na kutawaliwa na Narcissists. Sad sad sad.

Nani ataukata huu mnyororo wa kishenzi, urithi na matunda ya maumivu ya mababu na bibi zetu?!? Pakikucha itakuwaje?!
 
Haya ndugu mwelevu naona umetoa maelezo meeengi ambayo hayajagusia hata kiini Cha mada, yaani umeandika ujinga wa kuiga ule ule kama wenzako wanaofanana na wewe kimtazamo.

Sawa hatutakiwi kuchapa watoto wetu hili tusi induce hizo violence kama unavyosema, haya ni njia ipi Bora ya kukabiliana na watoto ambao tayari ni watukutu na wasiokuwa na adabu??? Yaani hapa nazungumzia wale watoto ambao ukiwakataza kitu hawaskii kabisa wakina Brighton sijui Carleen(kama mnavyowaita), njia gani zitumike au ndio tuwapeleke kwenye hizo clinics za malezi wafundishwe adabu na specialists wa watoto kama anavyosema Mhe.Gwajima hapo????
Mimi mwenyewe sikuchapwa na wazazi wangu na nilisoma shule ambayo ni marufuku kumchapa mwanafunzi, na mimi kwa nini niwachape watoto wangu, wakati kuna njia nyingi za kumlea mtoto? Naamini kuna njia nyingi za kuwalea watoto zaidi ya idadi ya watu duniani (there are as many ways to raise children as there are people in the world).

Njia ya viboko siyo effective, na kama ingekuwa effective, basi watoto wote waliolelewa kwa kuchapwa wangekuwa na superior bahaviour. Labda tukubaliane kwamba kila mtu anatenda kulingana na jinsi alivyolelewa. Aliyelelewa kwa mabavu/kwa viboko, naye atalea kwa mabavu/kwa viboko, kwa sababu ndivyo alivyolelewa. Na aliyelelewa kwa malezi yasiyohusisha viboko naye atalea kwa namna hiyo pia. Hii ndiyo tofauti yangu na wewe.
 
Acha kabisa, mimi kuna dogo mzee wake alikuwa kaimu pale TPA miaka ya 1990s ile. Jamaa alikuwa na mawe sana yani af maza alikuwa business woman. Ogopa dogo anasoma chekechea za ada laki 6 miaka ile. Mpaka kufikia 2003 story ikaflip back. Maza alidanja late 2001 na mshua 2002 kesi ikiwa ni umeme. Kama unavyojua kilovolt za miaka ile ilikuwa ni miez 6 tu watu wanafunga hesabu.

Sahizi dogo anauza sumu ya panya mende kunguni sisimizi kiroboto. Dogo alisomaga Tugusako badae Happy skillful kabisa ila game imechange.
Mazee hii story yako imenikumbusha familia ya Masubo, jamaa alikuwa ni maarufu sana pale Mwanza maana ni miongoni mwa wale Madon wa kwanza kwanza kabisa kufungua maduka ya simu pale Mwanza mjini miaka hiyo ya late 90s.

Huyo jamaa kwanza watoto wake walikuwaga wanasoma Uganda, na wakija likizo hamuwaoni, muda wote wanatembelea kwenye magari tu na hawana muda wa kuchanganyikana na watoto wenzie wa pale mitaani... Yaani walikuwa wanaishi maisha Fulani hivi Yale ya upper-class, yaani maisha ambayo kwa miaka ile sisi wengine tulikuwa tunayaona kwenye runinga tu.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000s ukaanza uvumi kwamba Masubo tayari ameshaukwaa na pia ana cancer ya damu na Kila bada ya miezi minne alikuwa anaenda kubadilishiwa/kuongezewa Damu huko bondeni kwa Madiba... Wala hata hakuchukua round akakata moto kwenye 2005 hapo na msiba wake uliudhuriwa na watu Kibao mpaka wabunge akina Diaollo(kwa wakati huo).

Sasa sikilizia watoto wake walivyoanza kuishi kwa kutaabika baada ya kifo Chake.... Picha linaanza madogo wote wakarudishwa kusoma shule za hapa hapa bongo Tena zile private schools za bei nafuu..

Kabla mzee wao hajafa walikuwaga hawali chakula kilicholala, lakini baada ya mzee kudanja wakaanza kula mpaka dagaa, tukaanza kuwaona wanapanda na Dala Dala ***** zao.

Maisha yaliwapiga sana wale watoto na walikuwa ni mandina kweli kweli maana ujanja ujanja wa mitaani hawakuwa nao, kwa sababu walielewa maisha ya geti Kali Yale ya kudekezwa dekezwa.

Kwa ufupisho tu mara ya mwisho niliskia mtoto wake mmoja wa kike ni Malaya wa kutupwa anauza uchi mgodini huko Geita na mwingine wa kiume ni fundi simu... Siku hizi nyumba yao imekuwa kama jengo la makuumbusho imechoka kweli.

Haya matoto yanayolelewa kimayai mayai wazazi wao wakiondoka huwa wanateseka na kuishi maisha ya ovyo sana, ya kuonewa kupuuzwa.
 
Mimi mwenyewe sikuchapwa na wazazi wangu na nilisoma shule ambayo ni marufuku kumchapa mwanafunzi, na mimi kwa nini niwachape watoto wangu, wakati kuna njia nyingi za kumlea mtoto? Naamini kuna njia nyingi za kuwalea watoto zaidi ya idadi ya watu duniani (there are as many ways to raise children as there are people in the world). Njia ya viboko siyo effective, na kama ingekuwa effective, basi watoto wote waliolelewa kwa kuchapwa wangekuwa na superior bahaviour. Labda tukubaliane kwamba kila mtu anatenda kulingana na jinsi alivyolelewa. Aliyelelewa kwa mabavu/kwa viboko, naye atalea kwa mabavu/kwa viboko, kwa sababu ndivyo alivyolelewa. Na aliyelelewa kwa malezi yasiyohusisha viboko naye atalea kwa namna hiyo pia. Hii ndiyo tofauti yangu na wewe.
Hivi umenilewa lakini swali langu nililokuuliza?? au umekimbilia kunijibu tu Tena kwa maelezo yako Yale Yale ambayo nimeshakwambia hayana mantiki yoyote?

Ngoja nijaribu kukuuliza kwa mara nyingine Tena kwa lugha ambayo pengine ndio walioitumia wazazi wako kukulea.

Aside spanking and taming what are other possible measures which are more corrective and effective can be taken in enforcing discipline to stubborn kids??? I need a very reasonable answer which doesn't only flow with your progressive ideas but it also align with reality of life of an average tanzanian parents.
 
"Shut up Daddy"
...and let me watching my favorite movie.

na wewe baba mtu unakaa kimyaa kweli, halafu ukija huku mitandaoni unatuona sisi wengine ni wajima wakati huo wewe uko civilized wakati kihalisia wewe na mwanao wote wajinga tu msiojua nini maana ya adabu.
 
nadhani waafrica hatutaki kutoka nje ya box kifikra kufikiria njia mbadala za malezi isiwe lazima fimbo pekee yake. Halafu
Mpaka Sasa hivi nyie ambao pro-western culture akiwemo na Waziri mwenyewe Bado hamjanipa maelezo yanye mantiki hili kunibadili mtazamo wangu kuhusu viboko.

Haya na wewe hapa hebu tuambie hizo njia mbadala za malezi ni kama zipi?
 
Kupiga mtu yeyote yule(hasa asie na uwezo wa kukurudishia) ni hatua ya juu kabisa ya uonevu.

Jiulize, wewe ukikosea, ni nani huwa anakupiga?
Mithali 23:13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Mithali 22:15 Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
 
Back
Top Bottom