Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

Sisi wa africa bila kunyukwa hatuendi jamii nyingi tunazotamani kuziiga nao wana mambo yao ya ajabu , sio kitu cha ajabu watoto wakizungu kuwaambia wazazi wao wanavutiwa na mahusiano ya jinsia moja na kwao ni kawaida tu.

Mda mwingne tusipuuze desturi zetu na kuiga za watu ambazo kiundani zina madhara yake pia.
'Bila Kunyukwa'😀 ishakuwa Imani tena. Nahisi tunahitaji huduma ya ushauri nasihi
 
Mambo ya daddy ,mammy ,junior ni hatari. kwa lyfe style za kibongo unless uwe na Mtonyo wa kwenda.
Hawa watoto wanaolelewa hivi ndio mwisho wazazi wakipata ajali ghafla wakafa huishia kutaabika sana na dunia
 
Kupiga mtoto at first hand naona haijakaa sawa isipokuwa tu kwenye attempts za uzembe. Mtoto alishafanya kosa hilo hilo mara mbili au zaidi hizo ni signs of negligence of which sio tabia nzuri kwa mtoto kukua nazo. Mara zote ulishamkanya ila anakuwa mzito kuelewa ni lazma umshtue kidogo.

Africa genetically tuna hizo element za kufanya mambo ya uzembe ikiwa hakutakuwa na gharama za maumivu kwa namna fulani.

Wazungu wao wana condition watoto in another way round. Hawa impose physical disturbance ila psychologically kama ku deny mtoto kufanya michezo flani kama way of punishment. Hawaruhusiwi kupiga ila adhabu wanatoa.
Na hayo yote yazingatie 👇
 

Attachments

  • IMG-20241020-WA0006.jpg
    IMG-20241020-WA0006.jpg
    94.3 KB · Views: 1
Nashukuru mzee wangu kwa kunipa kipondo kilali pale nilipotoka nje ya mstari. Bila hivyo leo hii ningekuwa pusha au teja.
Ulitusumbua sana kijana mshukuru mungu mzee Ndomba alikupeleka kikamanda.
 
Watoto wengi waliolelewa Kwa vipigo hawana maadili . wazazi wale wakali , wazee wakufoka foka wametoka 0-0 hawajafanikiwa kuandaa kizazi bora

Kuna njia za kulea mtoto ambazo zinaweza kumfanya akawa na Utii. Heshima na maadili mazuri.


Mtoto mfanye awe na usikivu mzuri na mpatie na EI
Zipi zitaje kwa manufaa ya wengi
 
Ahsante Sana kwa mada yako. Ndiyo Iko x usiku kucha jana na inaendelea.

Naongezea; tuna wazee wengi hawatunzwi na watoto wao waliowachapq Sana kwa madai ya kuwatengeneza. Je hii siyo MOJAWAPO ya athari ya mpasuko wa mahusiano ya watoto na Wazee ? Kwamba nguvu kubwa ilitumika kuumiza mwili badala ya ku transform akili ya ndani ya mtoto? Sasa mtoto kawa mkubwa, Tabia zake zilizokandamizwa kwa hofu ya kipigo, sasa zinaanza kushamiri na kumea maana hakuna wa kumpiga tena?

Nini maoni yenu?
Amini nakuambia...mzee aliekuchapa katika njia ya kukuelekeza uishi kwenye miiko na ukaja fanikiwa lazima utarudisha fadhila kwa kumtunz vzur...labda kama huyo mtt hajitambui..vivyo hivyo kwa mwalimu aliekuwa mnoko lkn alikuwa na nia njema kwako
 
Ni kweli mkuu wengi hawakubali na kusema ooh tunawadekeza hell no
Mtoto kuonywa na kupigwa kidogo ni sawa ila sio mpaka unamchoma moto mikono kisa kadokoa nyama au kaiba mia
Kuna wazazi washenzi mkuu na hao ndio sikubaliani nao kabisa

Unamfunga kamba mtoto masaa na kumfungia chumbani siku nzima
Mkuu kuna ukatili wa watoto we acha tu
Hata humu unaweza kukuta watu wanapiga hivyo
Tuendelee kutoa darasa ili nao wabadilike
Mzazi hata siku moja hutembei barabarani na mwanao bali kuwakunjia uso tu
Akikuomba buku unamtukana
.aisee tunaona mengi sana mitaani
Wengine wanasema wazungu hawapigi sio kweli wakiwa wadogo wanawapiga kwa kuwafundisha ingawa wanajua wanaweza kunyang"anywa watoto
Ila nidhamu ipo
Kina mama kwa afrika ndio wanaongoza kwa ukatili wa watoto sasa sijui kisa mimba za nje ya ndoa sijui
Ukizungumzia kina mama hapo nakubaliana na wewe kabisa. Wengi ni wakatili hasa wale waliozalishwa bila kuolewa na kisha kuachwa wahangaike na watoto huwa wana uchungu sana wa kuachwa hasira wanamalizia kwa mtoto.
 
Sisi huku watoto siyo wanachapwa, wanapigwa na kupigana na wazazi wao. Ngumi, mateke, wengine wanafungwa kwenye miti, wengine wamwagiwe maji ya moto, sad... Halafu mtu huyu anasifiwa na jamii....

Wanasahau kuna kliniki za malezi na makuzi na 👇
Hakika, umesema vyema waziri.
 
Naona wameanzisha sijui programs zao za child protection..ila ukiziangalia kwa jicho la tatu ni kutaja kutuaribia tu hiki kizazi....wanapitia sijui mashuleni na kuwaambia watt kuwa hairuhuisiwi kuadhibiwa kwa namna yyte ile ..huko huko wanapitisha na ajenda zao za ushoga....serikali inatakiwa uwe makinii sanaa na Hawa wanajileta kama NGO's
 
Nunua vitu vya jumla weka ndani acha kumtuma mtoto vitu rejaja dukani mara sukari robo, mara kiberiti kimoja, mara chumvi pakiti moja n.k
Mkuu hapa ndo unakosea...uchumi haulingani kwa wote...na haya ndo yanaleta makuzi tofaut ktk jamii
 
Mkuu hivyi unadhani ulivyo wewe namimi tunalingana kiuchumi?

Hujui Kuna familia Kila siku hununua mafuta 300 na sabuni ya kufulia na kuogea ndo hiyo hiyo? Kwa comment Yako inaonyesha wazi hujui hata uchumi wa watanzania walio wengi
Uko sahihi...pia hata hiyo kumtuma mtoto inamjengea hali ya kuish maziringira yyte ya kudekezwa na kupiga kazi pia
 
Jibu ni ndio. Ila tunajua ajenda iliyoko nyuma ya pazia mnataka tuishi kama ulaya Kwa sababu akili Zenu pamoja na kusoma kwenu hakujawahi wasaidia kabisa. Kila kitu lazima mabwana Zenu wa waambie Cha kufanya kuacha akiri yenu tu itatue vitu vidogo kama Hivi hamuwezi.

Hivi mlisomea utahira? Tuacheni sisi tulee Watoto wetu tunavyoona inafaa. Sio kutupangia
 
'Bila Kunyukwa'😀 ishakuwa Imani tena. Nahisi tunahitaji huduma ya ushauri nasihi
Tufanye Hivi muheshimiwa ninyi waleeni Watoto wenu kama Yai vile mbona inafaa nasisi tuwalee vile tunaona inafaa. Elimu Zenu Bado hajawahi kutusadia wa Africa Kila kitu mnafanya Kwa ku copy then mna paste. Akili Zenu zimedumaa na kukaririshwa na WA magharibi eti Kila wanachofanya wao ni sahihi tu.
 
Naona wameanzisha sijui programs zao za child protection..ila ukiziangalia kwa jicho la tatu ni kutaja kutuaribia tu hiki kizazi....wanapitia sijui mashuleni na kuwaambia watt kuwa hairuhuisiwi kuadhibiwa kwa namna yyte ile ..huko huko wanapitisha na ajenda zao za ushoga....serikali inatakiwa uwe makinii sanaa na Hawa wanajileta kama NGO's
Nashangaa sana sijui ni lini tutaanza kujiamlia na sisi mawazo yetu. Kama na kuleta napo tufundishwe Nini maana ya kuwa mzazi sasa.
 
Mimi nishapigwa tayari na wazazi wangu,ni zamu yao sasa
Kupiga mtu yeyote yule(hasa asie na uwezo wa kukurudishia) ni hatua ya juu kabisa ya uonevu.

Jiulize, wewe ukikosea, ni nani huwa anakupiga?
 
Mlete kwenye huduma ya marekebisho ya tabia
Hiyo clinic ni Kubwa kiasi gani?
Kama Kuna muongozo wa malezi Kwa watoto TZ yote (kama vile Hakuna kuguswa na fimbo Kwa kosa lolote lile). Hiyo clinic itatosha kujaza watoto watukutu TZ yote?
 
Ndo matoto yenu ya siku hizi changamoto kidogo anaanza kulia mara aseme ana depression, mitoto inakua milaini laini hadi unakua baba mzembe mzembe,

Malezi ni Tamaduni ukianza kuiga malezi ya watu wengine unapoteza utamaduni wako.
 
Back
Top Bottom