Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

No mkuu nmetolea mfano tu , mmonyoko wa maadili ni mkubwa sana kwa wenzetu tofauti kabisa na kwetu , pia hata wao wanapenda sana jinsi sisi tulivyo naongea kitu ninachokijua na sio nilichosikia mkuu .
Hata huko magharibi kuna wachache wanatamani maisha ya kupiga watoto na wanawake ila ndio hivyo wanazidiwa nguvu na wale waliostaarabika zaidi kwa hiyo wanabaki kutamani wangeishi kama nyie.
 
Mtoto hupewa adhabu akifanya makosa Kwa dhamiri.
Bahati mbaya Watoto wengi HUFANYA Makosa Bila dhamiri yàani Bila kujua ni Makosa.

Hivyo unapompiga inamtengenezea chuki zaidi ya kujifunza.

Kwa Bahati mbaya zaidi Wazazi wengi ni Wabinafsi, wakatili àmbao hujijali waô wènyewe.

Mzazi lazima uwe na Sifa ya Ualimu. Kumpiga Mtoto mara nyingi huleta matokeo Hasi kuliko matokeo chanya.

Fikiria Mtoto chini ya Miaka 14 unampiga mafimbo mengi kisa hajafua nguo Zake. Kumbe Mtoto mwenyewe hajafanya kusudi kutokufua Bali amesahau.

Sasa wewe kama siô chizi ni nini?

Au unampiga Mtoto Kisa kapoteza au kuangusha Pesa uliyomtuma akanunue maandazi. Mtoto hajafanya makusudi.

Kûna namna ya kudili na Makosa ya Mtoto hasa Yale àmbayo hajafanya kusudi.
 
Ukweli mtupu
 
Bila viboko hakuna maadili. Viboko ni baada ya maonyo mengi kwa mtoto, sio kila kosa viboko huo ni unyanyasaji. Kumbuka kumchapa mtoto ni muhimu ila usimpige,kupiga ni kitu kingine.
 
"Mda mwingine tusipuuze desturi zetu na kuiga za watu ambazo kiundani zina madhara yake pia" Kaka umenena vyema 100%.
 
Ninyi mliolelewa kwa vipigo mnajiona mna maadili? Mnataka kusemaje kizazi cha 80’ 90’ mliopigwa kama ngoma si ndio ninyi maadili yenu 0 wazee wa chini kwa chini?

Kinachomtofautisha mtoto aliyezoea kupigwa na yule ambaye hajapigwa ni confidence, Ukipigwa sana ile unayoiona wewe ni confidence si confidence bali ni arrogance, Ambae hajapigwa mara nyingi huwa na confidence iliyo balanced na anakuwa expressive (anaweza kujieleza) Mean while wa vipigo either akose confidence au awe arrogant.

Na most of psychopaths wamelelewa kwenye violence, think .
 
Kwanini tunadiscorage vipigo? ni kwasababu wapigaji (kama mpo mtakiri) Hamna kipimo, sababu ya jazba mnazidisha kipimo.

Wengi wenu hamna uwezo mzuri wa kumatch the child's actual experiences kulingana na umri wake na aina ya adhabu mnayowapatia.

Hata darasani, huwezi mfundisha mtoto wa darasa la 3 mambo ya mwanafunzi wa kidato cha 6, iweje kitoto cha miaka mitano unakipiga kipigo cha mbwa koko?
 
Hizo nchi ambazo watoto hawachapwi zina mmonyoko mkubwa wa maadili pia ,sisi tunajiona hatuna maadili ila ukitembelea kwa wenzetu utaona bado sisi tuna maadili sana😁
Hili huwa mnalipimaje? Maadili yanaendana na ustaarabu , kitu ambacho waafrica ni 0.

Ukiwaondoa wahindi, wathailand, wamexico na wa brazili na mataifa machache. Most of watu weupe wana maadili . Anza na wajapani, wachina na wazungu wenyewe, hapo ondoa black americans maana nao ni kama sisi tu isipokuwa kuna mifumo fulani fulani inawabana inawataka kuact accordingly.
 
Mnataka kuleta maisha ya kizungu mwishoni mitoto inakuwa ma bwabwa
Mtoto lazima umpitishe njia ngumu ngumu ila aje awe strong mbeleni ukimdekeza mwishowe ndio unakuta tatzo kidogo anaona bora ajiue
 
Umeibua hoja moja nzuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…