Hakunaga mtu anayekubali kuumia kwaajili ya Chama, ni namna tu unavyopanga karata zako za maslahi, pia ikumbukwe watu huwa hawapeani tu madaraka, huwa yanatafutwa. Power is not given, Power is taken. Kama Ndugu Lowassa alikuwa anasubiri kupewa madaraka na kikwete kisa alimsaidia kunyakua u Rais basi hakuwa ameiva kwenye kuitafuta nafasi ya u Rais, na ndio maana wanasema kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu inategemea tu kwa wakati husika mwenzio ataamua akuweke kundi gani ili afanikishe maslahi yake.
Tunaweza kufikiri CHADEMA kwa wakati ule walikosea kumteua Lowassa kuwa mgombea badala ya Dr. Slaa ila pale ziliangaliwa namba na nani mwenye influence kwa wakati ule, namba nyingi ya kura inamaanisha maokoto ya ruzuku pia yanakuwa juu bila kujali umeshinda ama umeshindwa, namba alizokuwa nazo Lowassa kwa wakati ule inawezekana Dr. Slaa asingezileta hata nusu.