Je Watu wameacha kumwogopa Kikwete? Wameamua tu waseme ukweli?

JK aliwahi kuwa Waziri wa maji, Waziri wa Nishati, Waziri wa mambo ya nchi za nje, Waziri wa fedha pia kama sikosei, Rais wa Tanzania na mwenyekiti wa chama. Sasa hata ukimsema yeye anapoteza nini?

Tusimfundishe JK aishi tunavyotaka sisi au aishi Kwa kuiga wengine, umeamua kuitumia style hiyo anayoitumia kudeal na adui zake na ndio ilimfanya afanikiwe, siajabu angetumia style uitakayo asingeweza kuyafikia mafanikio aliyoyafikia.

JK alitumia sarakasi zake mwenyewe kuipata Urais na kukaa kwenye Urais - hiyo ndio tafsiri sahihi ya mwanaume, EL alishindwa kutumia sarakasi zake mwenyewe kuwa Rais akamtegemea JK - tunapata funzo hapa, usimtegemee mwanadamu kufikia mafanikio yako.

Mwisho: Kifua cha JK kimebeba mengi sana ya nchi hii toka zama za JKN mpaka leo zama za. mama
 
Hivi nyie mnaonga'ang'ana kila siku.kwamba lowasa kasalitiwa mlitaka afanyiwe nini?

Huwezi kumpa madaraka mtu mwenye tamaa na madaraka.
Hata akiwa lafiki wa aina gani. Muacheni huyo mzee apumzike sasa.mwenye mamlaka kuu kampenda basi, wengine nao wapo nyuma yake. Kasoro mimi tu.
 

Mpaka mwili wa mzee Lowassa ushushwe mavumbini, mzee Kikwete atakuwa amechoka sana kwa kusemwa wazi wazi. Hapa mzee Lipumba amesema wazi Richmond ilikuwa ya JK. Chegeni naye alisema wazi kanisani kwamba Lowassa alibebeshwa mzigo usio mhusu.

Kibinadamu hata mzee Kikwete ndani yake ana maumivu makali na pengine anajilaumu kwa usaliti, anaona kila mtu anamuona mbaya.
 
Mwanzo walitamba kuwa Jk hawezi kuzuia Mafuriko

akaamua sio tu kuyazuia bali akayakausha kabisa wakaanza kumlaumu eti ana roho mbaya sijui hajui shukran etc

Yaani ukabidhi Nchi kwa mtu kama shukran ?
 
Wacha upumbavu mleta mada, Lowasa ni mjinga kiasi gani akubali kuumia Kwa ajili ya chama chake? Kwani CCM ni mama yake? Tusidanganye.
 
Jamaa alikuwa amehonga hadi makanisani, kuna wakati kwa jeuri na alikuwa na jeuri kweli kuwa wasiompenda kwenye chama waondoke wao, akajidanganya na akina Kingunge, Tibaijuka, Musukuma, Bashe, Malasusa wakati ule alidhani Mr Kutabasamu hatamuweza na kweli Mr Kutabasamu alimshindwa Mr Mamvi kwa bahati mbaya sana Mr Mamvi alimsahau Mzee wa Lupaso, kwa wakati ule Mzee wa Lupaso ndie alikuwa Nyerere, na Mzee Lupaso alikuwa na ugwadu nae kuanzia uchaguzi wa kwanza ambapo ndio timu ''wanamtandao''iliundwa ili kumshida Lupaso, Lupaso akaja okolewa na mzee wa Butiama, bila mzee wa Butiama sijui ingekuwaje kwani lile agano la hao marafiki na baadae maadui sijui lingekuwaje.
 
Mambo ya siasa siyo ya kuyaingilia ....wananeemeka sana hao.Watajuana wenyewe
HUo ndio ukweli ya nini kujitia pressure kwa mambo ya watu kama sio umbea na kupoteza muda, wao na familia zao wameneemeka wewe huku kutwa umbea tu ambao haukusaidii kitu
 
Huyu naye mbona aliwasaliti wenzake UKAWA akaenda kula bata Rwanda na dogo mmoja anadhani watu wanasahau
 
All in all Tibaijuka alishasema ni ngumu kumtangaza mshindi asiyetakiwa na mfumo, yule ambaye angetajwa kugombea na chama chetu basi iwe isiwe hata kwa bunduki angeshindishwa ndiyo tafsiri ya goli la mkono
 
Wanasiasa ndio wanaoichafua siasa ili kufikia malengo yao.

Ila siasa inapaswa kuwa mchezo msafi tu.
Africa maana ya siasa ni fitna fitna na uongo unaofanana na fanana na ukweli !
Ndivyo tulivyojiaminisha !!
 
All in all Tibaijuka alishasema ni ngumu kumtangaza mshindi asiyetakiwa na mfumo, yule ambaye angetajwa kugombea na chama chetu basi iwe isiwe hata kwa bunduki angeshindishwa ndiyo tafsiri ya goli la mkono
You nailed it !
 
Sawa bado Magufuli anakuwa ni SHETANI kwa vile mbali ya kukuchukia ANAKUUA au anakutupa jela.

Usimfananishe Kikwete na SHETANI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…