Mate, Habari.
Kwenye familia zetu kumekua na nadharia inayosema kua watoto ambao ni wa kwanza kuzaliwa hasa watoto wa kiume kwamba hua hawana Akili, ni mapepe,ni watundu na mara nyingi hua hawana mafanikio mazuri kiuchumi (pesa) na kijamii (familia). Ni kweli, Mara nyingi wazaliwa wa kwanza hua
(HASA WA KIUME) hua na maisha Vulnarable hasa katika mafanikio ya pesa,familia zao,elimu,tabia nk. Watu husema kwamba eti kwakua mtoto alikua ni wa kwanza kwenye familia hivyo alidekeshwa sana hadi ikapelekea akili yake kudumaa na kua mjinga,wengine husema kwakua ni mwana wa kwanza hivyo mayai na mbegu yalikua hayajakomaa ipasavyo kutoa mtoto mwenye akili, Wengine huenda mbali zaidi na kusema kwamba watoto wa kwanza akili zao hua hazijatulia kwakua eti wakati wanzaliwa mlango wa uzazi wa mama ulikua haujatanuka hivyo ilipelekea wakati mtoto anatoka tumboni kichwa chake kiligandamizwa na mlango wa uzazi ili kipite hivyo akili ya mtoto nayo ikawa
Compressed, Hence ndio maana watoto wa kwanza hua akili zao hazijatulia na hua hawafanikiwa sana maishani kama wadogo zao….
WRONG!!! Nadharia na dhana hizi zote ni ongo na potof, ni kweli kwenye familia zetu wazaliwa wa kawanza wana matatizo mengi ila mtatizo yao hayasababishwi na chochote nilichoorodhesha hapo juu au chochote unachofikiria wewe. Kuna sababu nyingine kubwa ndio inafanya wazaliwa wa kwanza wawe hivyo mnavyoona walivyo.
GENESISS
Ili tujue sabau kuu ya wazaliwa wa kwanza kua hivyo inabidi turudi nyuma hadi kipindi cha ukombonzi watu kutoka misri, Israel walipokua Sinai Mungu aliongea na Mussa kuhusu wazaliwa wakwanza
Hesabu 3: 13.”Kwakua wazaliwa wa kwanza wote ni wangu, katika siku ile niliyowapiga wazaliwa wote wa kwanza katika nchi ya misri nikajiweka wakfu wazaliwa wa kwanza wote wa Israel, wa wanadamu, na wanyama watakua wangu; mimi ndimi BWANA”.
Pigo la mwisho la Mungu kwaPharaoh lililofanya hadi wana wa Israel kuruhusiwa kuondoka lilikua pigo la kua kila mzaliwa wa kwanza wa watu wa misri, hivyo basi hapo kwenye kifungo hicho mungu alimwambia Musa kwamba kila mtoto, mnyama,mavuno,mapato ya kwanzakatika taifa la Israel yatakua ni mali ya BWANA yaani wanatolewa kumtumikia BWANA maisha yote kama ni mazao au mifugo wanatolewa kama sadaka ya kuteketezwa. Lakini baadae kidogo Mungu alibadirisha sharia(torati) hiyo, aliwachukua watu wa kabila zima la
WALAWI WA KIUME na kuwafanya wao ndio watakaokua wanatoa makuhani na watumishi wa kumtumikia. Alifanya hivyo kwa ajili ya Uaminifu aliouonyesha kuhani wake Aaron (haruni) aliyekua anatoka kabila la Lawi. Lakini akasema kila mzaliwa wa kwanza wa makabila mengine watatakiwa kumnunua kwa kutoa sadaka mbele ya bwana. Aliyasema hayo katika
Hesabu 3:41
Ikimbukwe kwamba Yesu Kristo alikua ni mzaliwa wa kwanza mwanaume katika familia ya Bwana Joseph na Bibi Mariamu, hivyo basi kama ilivyo agizwa katika torati ya Mungu nimeeleza hapo juu Yesu alitakiwa akatolewe kwa Bwana hekaluni ila wazazi wake walitoa sadaka hekaluni. Kwakua familia ya Joseph ilikua maskini hivyo haikuweza kumudu kutoa ng’ombe,mbuzi,kondoo walimtolea Mungu sadaka ya NJIWA WAILI Yesu akarudi katika familia, Refer
Luka 2:22. Swali ni je kwanini anatakiwa mzaliwa wa kwanza tu sio wa mwisho au wapili? Lakini tukumbuke mada yetu inataka tujue kwanini Wazaliwa wa kwanza kwenye familia ndio hua wanaonekana na matatizo. Tuendelee…
REASONS
Mtoto wa kwanza anapozaliwa anakua
Endowed ,Entrusted and Blessed with God katika uongozi na uangalizi wa wa familia na watu wanaomzunguka kiroho na kimwili Mungu kamchagua mzaliwa wa kwanza kwakua yeye ndio future na msimamamizi wa familia husiki baada ya wazazi kuishiwa nguvu au kufariki. Kwa sababu hiyo basi mtoto wa kwanza amezaliwa akiwa na Baraka tele maishani pia kapewa extra knowledge na potential kubwa kuliko watoto wengine ili aweze kuongoza familia yake baada ya wazazi. Ndio maana Mungu alipowapiga wamisri pigo la mwisho walisalimu amri wakawaachia waisrael maana pale Mungu alikua ameteteresha future ya familia. Pia alitaka wazaliwa wa kwanza kutoka familia ya waisrael kwakua mtoto wa kwanza ukiwa umempata hua unakua na upendo wa ajabu kwake na Mungu anapenda umtolee kile kitu ambacho ukikitoa kinakuuma sana maana yake kina thamani kubwa sana kwako, ndio maana babu yetu mzee
Ibrahimu anachukua point kua baba wa imani kwakua aliweza kumtoa mwanae wa pekee aliyempata uzeeeni kabisa
Issack .
Kwenye familia zetu wazaliwa wa kwanza hua na akili za kuzaliwa na wana upendo wa hali ya juu kwa wadogo zao, utakuta kaka/dada yupo tayari asisome ili ndugu zake wasome vizuri, hufanya kila kitu kuhakikisha wadogo zao wanasimama vizuri kielimu kwa kuwasomesha na kimaisha kwa kuwapatia mitaji au kuwatafutia connection. Yupo tayari mkewe asiavae nguo kwenye Eid au Xmass ili tu wadogo zake walipiwe ada, ukikuta mzaliwa wa kwanza anayejitambua na kusimamia majukumu yake hufanya kila kitu ili tu ndugu zake wasipitie tabu alizozipita na wazazi wake wakati anazaliwa. Kwa sacrifice zote hizo wazaliwa wa kwanza wanazozitoa ili familia/ukoo usiaibike kiroho na kimwili ndio maana wao utakuta wana maisha magumu kuliko wadogo zao, bahati mbaya wadogo zao wengine wakishafanikiwa hua hawamjali tena kaka/dada yao baadae wanaanza kumuona kama kaka yao Dishi limeyumba kiasi Fulani au ana gundu la maisha au anapenda kuwapiga mizinga…Wanasahau hapo walipo ni kujitoa kwa kaka/dada yao mkubwa kiroho na kimwili. Lakini wazaliwa wakwanza wanaelewa kwamba wazazi watakufa siku moja,yeye atakufa siku moja,na ndugu zake watakufa siku moja ila Legacy that is what lives on..Familly that’s what matter. Ndio maana wanaendelea kupigania ndugu zao wasiamame kabla yao.
Mkubwa ni jalala
Nini kinafanya maisha ya wazaliwa wakwanza kuwa Vulnarable..?
Kuna mwimbaji injili anaimba kwamba “Mungu anafanya kampeni na shetani anafanya kampeni” ni kweli mwisho wa siku kila mmoja anataka apeleke Hesabu zae. Shetani ndio adui mkubwa wa wzaliwa wa kwanza, Shetani unapozaliwa tu anakua ashajua mtoto huyu ana potential gani maishani hivyo mappema sana ataanza kumuwinda mtoto huyo ili amuharibu. Atafanya kila njia kukupata ayafanye maisha yako vibaya. Wakati Mungu anahitaji roho yako ila sio mwili wakoyeye shetani anataka vyote viwili…Anajua kabisa roho yako hawezi kuifikia kwakua ni roh yenye Uungu hivyo atautumia mwili wako zaidi kuua roho yako yenye potential hapa duniani, Akishauharibu mwili roho inabaki haiwezi tena na inakua rahisi kuipeleka roho nje ya kusudi kuu la mungu maana roho inahitaji mwili kutenda. Mwili ukiwavizuri basi roho yako inaweza kutenda yapaswayo kwa uafasaha..lakini pia mwili wako ili utende kazi inahitaji
ROHO ILIYO IMARA.
Ukitaka kuharibu Jf inatakiwa umpige Max ukimshinda moderator wote watakimbia, ukitaka kuiangusha treni yote anza kuangusha kichwa chake(injini) ndipo mabehewa nayo yataanguka yote ukianza kungusha mabehewa yaliyo nyuma kichwa cha treni kinaweza kuyaweka sawa mabehewa na safari ikaendelea. Ukitaka nyoka afe mapema usijiahangaishe na mgongo piga kichwa nyoka atakufa haraka. Shetani anajua hizi mbinu zotenaye hua hajiahangaishi na mabehewa hua anaanza Injini. Shetani lengo lake ni kuangusha treni (Familia) kiroho,kiuchumi, na kijamii hivyo anachofanya anaangusha kichwa/injini (mzaliwa wa kwanza) kisha mabehewa (ndugu) huanza kuanguka. Kwanza kabisa anaanzakum distract mtoto toka akiwa mdogo kwa magonjwa mbalimbali, akienda shule anamuwekea vikwazo ili tu asisome inavyotakiwa akaja
ku-Retrieve potential yake. Baadae atamletea vikwazo kama kutokujiamini, aibu,kutokuweza kuongea/kujieleza,hofu na uoga. Shetani anaweza hata kutumia hata wazazi,ndugu au majirani ili tu aharibu potential ya mzaliwa wa kwanza coz anajua mtoto akisimama katika njia yake anayotakiwa kuwa basi anaweza iongoza familia kwenye mwangaza mwisho shetani ashindwe kukusanya mapato yake ya kwenda na watu gizani.
Utakuta mtoto wa kwanza ulevi,bangi ,uhuni,ubishoo,kamari,wizi,na mengine mengi mabaya anayo yeye. Unakuta hana future ya maisha yake au akili za shule hana kawa kituko cha familia, hapo ndio watu wanaanzisha ile dhana ya kwamba mzaliwa wa kwanza kwenye familia hua hawana akili aua hawajatulia. Kumbe si kweli! Shetani anakua ameshawin maisha hayo ya mzaliwa kwanza…
Je mzaliwa wa kwanza aiepuke vipi mitego ya shetani..?
- Malezi stahiki kwa mtoto toka kwa wazai
Hope mwajiuliza kama Mungu kaumba mtot akiwa na potential zote hizo kwanini anarusu shetani aje amuharibu kijana? Jibu ni kwamba huko juu nimeeleza kwamba ili mwili uweze kukwepa mitego ya shetani basi mwili unahitaji roho iliyo imala. Roho inaweza kuulinda mwili usishambuliwe na sheani na mwili ukishashambuliwa basi roho inakua haiana uwezo tena. Eg mwili ukishashambuliwa na pombe,bangi na madawa ya kulevya basi hauwezi kufanya yale roho inayotaka kutenda kama vile Kuaishi katika kusudi kuu la binaadamu kuumbwa. Hivyo basi ili mtoto ambae bado yupo kwenye himaya ya wazazi inabidi apate malezi yanayofaa toka kwa wazazi. Kama wazazi wakiwa na imani iliyo thabiti na wanaelewa mtotot wao anatakiwa awekwe vipi ili aishi maisha bora huko baadae basi wanaweza kumuokoa tokakwenye mikono ya shetani. Wazazi inatakiwa watengeneze misingi imara kwa watoto wao ili baadae waje kuongoza familia kama inavyotakiwa. Nyumba iliyojengwa kwenye msingi imara haiwezi tetereshwa na kimbunga wala tetemeko.
- Elimu ya kiroho na kimwili itolewe kwa vijana
Waliopewa dhamana ya kuwalea vijana kiroho na kimwili watoe elimu kadri iwezekanavyo, wawafundishe elimu ya utambuzi wajue kusudi la maisha yao na wajue kwanini wapo hapa duniani. Binafsi sijui kama sisi tuliozaliwa miaka hii ya 2000s tunayajua haya masuala ya mzaliwa wa kwanza na kusudi la maisha. Tunajua kuvaa kamatia chini,kuvaa suruali zilizochanika magotini,kupiga picha location na kupata likes Fb ndio kila kitu maishani. Kwa kipindi hiki cha teknolojia na Artificial intelligence inaanza kutumiwa widely na watu wa kawaida sijui kutakua na kizazi cha aina gani kama Elimu ya utambuzi kiroho isipotolewa ipasavyo. Ila yote tutayashindwa kwa imani thabiti maana mtu mdogo anaweza kutoa kivuli kikubwa,
mwanga wa tochi dogo au kibatali unaweza kufukuza giza kubwa ndani ya nyumba. Siku zote Giza haiwezi shindana na mwanga..ila yote hayo yatawezekana kutokana na
imani yako au Uimara wa roho yako.
Sasa kuna wakati wewe mzaliwa wa kwanza unaweza kua umeyafanya mambo mawili niliyoainisha hapo juu au hukuwahi kufanya kabisa maishani mwako na maisha yako yamekua totally miserable huoni pa kutokea maisha yako yamejaa giza ila unatamani kutoka huko ulipo utembee katika njia ya kusudi lako, Fear not God got you coverd!
Mwalimu Mkuu/lecture (
Yesu Kristo) ni mzaliwa wa kwanza katika familia ya BWwana Joseph na Bibi Mariamu, yeye ndio kiongozi wa wazaliwa wa kwanza wote hapa duniani. Anajua kamba Yule mwovu anawatafuta kwa kila hali ili msiweze ku-pursue kusudi lenu, baada ya kumaliza mkataba wake wa kufundisha hapa Darasani(
Duniani) akaondoka zake kwenda kuandaa mataji na vyeti (kupaa mbinguni) kwa wote ambao watakaofaulu masomo yake alijua kabisa hawa wanafunzi wangu wanakumbukumbu hafifu na wakiona mwalimu hayupo hawajisomei tena (
kuishi katika maagizo ya Kristo) wanabaki kupiga fujo darasani. Hivyo alipofika huko alipoenda alimtuma
Tutorial Assistance wake (
Roho mtakatifu) aje kutukumbusha na kutufundisha maagizo ya Kristo kwa wale ambao tulikuja muhula ambao kristo hayupo.
Tutorial Assistance alitufundisha kitu kipya kwa sisi tulioingia muhula mpya mwalimu mkuu akiwa hayupo, Alitufundisha kitu kinaitwa deliverance kwa Kiswahili rahisi ni kupokelewa Upya. Wewe mzaliwa wa kwanza Ukishafika ile sehemu tunaita
the point of no Return maisha yako yamejaa taabu na mahangaiko Yesu kristo kupitia roho mtakatifu anatoa huduma hiyo ya kuwapokea upya wale wote ambao wamepote maana yeye ni mchungaji mwema kondoo wake mmoja akipotea atahakikisha anamtafuta na kumrudisha kundini…Hivyo Yesu kristo kupitia Roho mtakatifu amewaagiza watumishi wake kuwa na siku maalumu au vituo mbalimbali vya kupokea wale wote waliopotea. Ukienda hapo wataformat
Had Disk Drive yako (roho) na kufuta
cockies na caches (roho za giza) zote zisiweze kukufuata tana.
Ukitoka hapo unakua mtu mpya na unaweza kuishi katika kusudi lako kama mzaliwa wa kwanza ila kamwe usisahau Uimara wa Roho yako ndio unaohitajika kuweza kuishi katika Kusudi lako kama mzaliwa wa kwanza.
The End…
[Comment, Like and Share)
~Da’Vinci
El maestro.
Nimeona.
Ni mchango mzuri na kuna neno.
Japo umetumia nasaha za kujinasibu na vyanzo vya 'kidini' na 'imani' -- maudhui yako kwa ujumla yana kusudi jema.
Umeleta kisa cha Musa na maisha ya Waisraeli wakati mmoja, kulingana na simulizi zinazopatikana kwenye vitabu vya Biblia -- japo mimi kama mtu si 'muumini', lakini ninapenda kusoma chochote na kujifunza kutoka popote na ninaona kuna neno la kutilia maanani kuhusiana na kisa cha Musa na Waisraeli kwa mujibu wa simulizi na muktadha wa somo lako.
Musa alikuwa ni Kiongozi wa Jamii ya watu; alikuwa akipata msaada kutoka kwa 'Mungu' -- mungu wa Waisraeli... Ukiwa ni mtu wa visomo, hili litakuja kuwa bayana, kila jamii hapa duniani imepata kuwa na 'misingi ya imani' na 'taratibu' zenye kushikiza mila, tamaduni, desturi na stawi zao. Ukija kuwa na bidii ya visomo utakuja kubaini si kweli hasa kudai 'sura ya mungu' katika jamii moja ni sawa sawa na jamii ingine... Kwanza kabisa, kwa kadri kabisa ya sayansi ya kijamii, mapokeo na 'harakati za jamii kutafuta ufunuo' si lazima 'imani' ya jamii, kabila, watu fulani wa makazi ya pamoja iwe ya namna moja, kufanana kwa hapa na pale kunaweza kuwepo -- lakini si lazima kwa kila kitu. Na hapana shaka, gurudumu la 'harakati za jamii kutafuta ufunuo' ni endelevu. Kama vile stawi na staarabu huinuka na kuanguka, ndivyo hivyo hata imani na mapokeo yanaweza kuja na kwenda... Kwa maana tunachodhania kukifahamu kwa misingi ya kufaa kheri na utangamano wa leo, kesho tunaweza kuja kujua ilivyo bora zaidi na basi kuja kuchukua sura ya ustawi na ustaarabu bora zaidi. Utamaduni wa mtu, makundi ya watu na hata Taifa hauko kusimama tu -- ni wenye kutembea kwenda mbele panapo mazingira bora ya kustawi na maendeleo. Kwa hivyo, si tu kawaida ya leo -- kwa kesho inaweza kuwa ni batili ama bure tu, hata sheria za leo -- kwa esho inaweza kuwa ni batili... Tunaishi kutafuta muafaka kati ya 'upeo na vina vya tafsiri kwa mambo yetu' na 'mapana ya elimu, ujuzi na kujua ilivyo bora' -- kama mtu mmoja mmoja, tunaofanya makundi ya watu, makundi ya watu yanayo zifanya taasisi , na basi tuseme -- kadiri ya 'Taifa' kwa ujumla...
Sisi kama taifa, tunahistoria, nasibu na mustakabari inayoweza kutohitaji kufananishwa na Kisa cha Musa -- tuseme Musa na Waisraeli siku za zamani. Kwa mfano, Tanzania, kama taifa changa, ni jamii inayofanyika kutokana na muunganiko na mchanganyiko wa watu wanatokea katika mila, desturi, tamaduni na imani tofauti tofauti; hili linaleta changamoto nyingi katika mbinu za kileo -- za kuunganisha 'sauti' na 'nguvu' za watu kwa misingi ya taasisi za kidemokrasia -- ili kuwanasibu watu na maendeleo, ustawi na ustaarabu... Je, Unakumbuka usemi, unaotokana na mawaidha ya Uyunani ya Zamani, siku za Plato, kukadirisha kudai '
Ili Nchi Iendelee, inahitaji Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora' (?)
Umoja wa Kinchi katika siku za leo, unasigana na harakati za makundi ya watu kupendelea kujipambanua kwa misingi ya udini, ukabila, ukanda na mengine mengi ya namna hii. Tunapenda kujivunia mazuri na makuu ya waliotutangulia na kurithishwa kwetu; lakini haya yanaweza kuwa vikwazo katika utekelezaji wa demokrasia, uhuru, ustawi na maendeleo. Hali kadhalika, huwezi kusema 'watu ni wamoja' na kumbe hao hao 'kila mtu anaamini chake' mintarafu 'jaala ya maisha yake' na 'hatma ya harakati/pilika zake'. Hili ndilo linaleta swali makini kwa wanazuoni wa kwa mfano siasa na maendeleo... Je, demokrasia ni jambo linaloweza kusanifika na kutekelezwa duniani? Kwa sasa na dunia nzima, kuna ukomo wa utumikivu wa dhana, nadharia na tafsiri za 'demokrasia' -- jambo linalojidhihirisha kwa migogoro mingi ya harakati na 'siasa za uwakilishi' katika mataifa na nchi -- ugumu katika utekelezaji wa demokrasia za kiliberali...
Haya, yawekwe hapa ili kutusaidia kubaini kuwa kila kizazi katika nyakati kinachangaoto zake. Ni wajibu wa jamii husika kutafuta muafaka wa ustawi na maendeleo kwa misingi ya mbinu kama elimu za visomo... Tukifanya mbinu na visomo juu ya hatma za maendeleo na ustawi wetu basi tutajinasibu na hata kuweza kuona, zamani ilikuwa ni rahisi 'kushikilizisha' dola, jamii ama kabila ukiweza kutaasisha imani iliyomoja kwa wote -- juu ya mambo kama vile 'mungu', 'miungu', 'Mizimu','Mababu', 'Wahenga' n.k... Katika ulimwengu wa leo, makundi mengi kwa ujumla yanajinasibu 'kujiondoa' na 'usadikifu pofu wa kimakundi' -- hili si la kushangaza, kwa kuwa haya pia ni matokeo ya kuongezeka kwa maarifa na elimu... Lakini, kwa mtu yoyote wa kisomo na visomo hasa -- si rahisi kukwepa kuchunguza na kumulika kila kitu...Hata muafaka wa 'Pengo la Mungu' katika kubayanisha ukweli 'uliowazi' ama 'kujificha' -- kule kuliko ni nyuma ya hatma za watu, ustawi na mamendeleo. Huu '
uko pale pale kutafutwa'.... Kushuku, labda 'maarifa' na' visomo' vyetu vya leo bado 'si kamili hasa'...
Mbadala wa siasa na harakati zake kwa maisha ya leo upo katika jitahada za '
Mipango na Ushirikishwaji' kwa maendeleo ya jamii na kujichagulia. Kwa Tanzania kwa mfano, kama taifa tumekuwa tukijifunza na tunaendelea kujifunza ni namna gani tutapata muafaka wa kukabiliana na maadui wakuu watatu --- Umaskini, Maradhi na Ujinga. Kutoka katika uwanja siasa na sera, tumejipambanua kutoka kwenye 'Siasa za Ujamaa na Kujitegemea' hadi kuwa 'Wanabidii katika Ulimwengu wa Leo wa Utandawazi'--kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025... Katikati ya haya mawili, kuanzia
mnamo miaka ya 80, Tulitekeleza maboresho ya kimfumo na taasisi, kutoka '
Ukati' wa Serikali Kuu hadi '
Ugatuzi' wa Mamlaka kwa Serikali Ndogo Ndogo za eneo moja hadi jingine. Kutoka ngazi moja ya mipango, maamuzi na utekelezaji hadi ingine -- kuanzia vitongoji/Mitaa, Kata, Wilaya. Mkoa mpaka Taifa/Serikali Kuu. Azma kuu ya hili ikiwa ni kuongeza tija katika kuibua mahitaji, kusuka na kutekeleza mipango kwa mbinu shirikishi ili kusaidiana na serikali kuu katika kutekeleza makusudi makuu ya Kitaifa kama vile maendeleo kwa watu wote --- na sura ya maendeleo tunayoitafuta ni yale ya watu --- si vitu. Japo katika maendeleo ya watu kuna ya vitu humo humo, mambo yanasohusiana na ukuaji wa uchumi...
Aidha, kwa ujumla, matumizi bora ya Rasilmali, yanaweza kutatua kadhia zetu za umasikini na maradhi pale ambapo tunajitahidi misingi ya
maendeleo endelevu kwa kuzingatia 'utawala bora', 'ukuaji wa Uchumi', 'Maboresho ya Huduma za Kijamii' na 'Uhifadhi wa Mazingira'. Na ikumbukwe, kuzungumzia 'utawala bora' ni kuzungumzia kujenga uwezo wa 'jamii ndogo ndogo kujitawala zenyewe' kwa kuhakikisha kuna uwazi katika mabadilishano ya taarifa, kuna uwakikilishi na Ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ya wenyeji na wadau katika kuandaa na kutathmini muktadha wowote wa mipango, mkakati na utekelezaji wake. Ukuaji wa Uchumi unaakisi ongozeko katika ufikiaji wa mahitaji ya karibu na mbali kuhusiana na riziki, fanaka, uzalishaji na huduma... Maboresho ya huduma yanabeba mambo kama vile miundobinu muhimu kama upatikaji wa umeme/maji, Upangaji wa Matumizi bora ya ardhi, ujenzi wa vituo vya Afya na Elimu na mengine mengi ya namna hii. Katika haya manne ya nguzo za maendeleo endelevu --- Suala la Mazingira ndilo Mama wa yote, kutunasibu wanadamu wa leo kung'amua 'Mungu' katika ulimwengu wa leo anaingia katika eneo gani la 'visomo, uweza, mstahiilisho wa yote'... JInsi gani, kutokujali, kukosa umakini, kufanya mambo kiholela kunaweza kuwa 'laana' na 'kukosa baraka' juu ya hatma ya matendo yetu. Jinsi gani sisi kama watu duniani tunaweza kujiangamiza wenyewe ikiwa tunakosa maarifa, busara na 'moyo wa mapenzi' mema kati yetu na viumbe vyote vilivyomo sayarini mwetu...
Kwa kueleza haya, ikidhi kuonesha hata leo hii tuna akina 'Musa'... Unaweza usiwaone ubayana wao kwa kuwa tunaishi nyakati tofauti na matendo yetu yanabeba sura mpya na tofauti na zamani. Unapokuwa na kiongozi na mwanataasisi kama Rais Magufuli John, anayekazana kusimamia na ujenzi wa miundombinu muhimu -- analolifanya lina mengi ya manufaa kuliko hasara katika jamii. Kujitahdi kuimarisha misingi ya utawala bora -- wengi labda wanadhani ile 'tafsiri ya kisiasa' itajapwo 'utawala bora' ina mapekeleo muhimu, lakini ukweli halisi ni kuwa: mapambano dhidi ya rushwa ndipo penye 'mzizi wa fitina' hasa-- silika ya makusudio yenye kuharibika upesi katika mtu, ni kati ya sumu mbaya kwa ustawi wa jamii...Ugatuzi wa mamlaka kwa mfano, huongeza uwanja wa mawezekano ya rushwa kubwa na ndogo katika kila nafasi na ngazi za maamuzi na utekelezaji wa haki -- na hili lina uwezekano wa madhara makubwa kuliko kuingilia kati mgawanyo wa matunda nchi ili kupendelea miradi yenye kunufaisha sura pana ya ustawi wa taifa... Kinyume na inavyodhaniwa na wengi, maendeleo kwa sehemu kubwa ni uimarishaji wa taasisi na 'si siasa' hasa.... Na hata ikibidi tumulikie siasa na umadhubuti wake katika 'kuwaunganisha' watu, Chama kama Chama Cha Mapinduzi kina mtaji bora wa kuweza kujisuka kimkakati na kujipanga ili kuithibiti siasa -- mpaka pale ulimwengu wa harakati za kisiasa utakapomaliza pumzi yake.... Hili linaweza jambo la kimtego sana kulibaini ukweli wake, lakini linaweza kudadavuliwa vile vile ukweli wake....
Sasa, naona mada inahusu 'Mtoto wa Kwanza' lakini, 'nimeteka nyara' maudhui na basi kulingania 'Maarifa ya Ujamhuri' wa leo. Nimefanya hivi, kumaliza nguvu mashauri ya 'Musa' na 'Israeli'... Lakini hii ni nusu ya kisa...
Mbali kupitiliza haya yote mpaka hapa, ni mchango wangu kama mtu, kunasibu maendeleo na stawi za watu ziachane na 'vikomo vya utumikivu' wa mifumo ya leo. Nikiwa ni mwenyekujua wazi yaliyopo, yanayoendelea na mawezekano ya kesho, nitafanya muingiliano muono wangu kama mwanataifa na visomo vya kitaasisi ili kunasibu maendeleo ya siku zijazo --- yenye kupitiliza 'usadikifu pofu wa kimakundi' -- kuelekea liberiti kamili. Sehemu ya maono na tafsiri ya haya unaweza kuyapitia katika
uzi huu.
Kuna uwezekano, miaka michache inayofuatia kuanzia sasa, dunia yote itapitia kipindi kigumu... Uchumi wa dunia kwa sehemu kubwa unakwenda kuathirika na kadhia kama ya hili janga la ugonjwa wa virusi vya korona... SI kuwa mimi kama mtu ninakubaliana na yanayosemwa huko nje ya nchi kuhusiana na hili 'jangaa', la hasha. Mawaidha yangu kama mtu yapo katika
uzi huu. Kuna mambo mengi nyuma ya pazia katika tawala za dunia. Sisi kama taifa tunaweza kuathirika na kukongoroka/kudorora kwa uchumi katika nchi za 'dunia ya kwanza' kunakonukia. Mfumo wa leo uchumi wa dunia na mategemeano ya 'biashara za kimataifa' ni 'si endelevu'. Tunavyoweza kujiandaa na kipindi hichi cha mpito, kuna uwezekano wa kuleta 'Uhandisi Kamili wa Kijamii'... Katika huo, usijekushangaa wazo lako la 'Mtoto wa Kwanza kuzaliwa' litachukua sura ipi...
Katika jamhuri iliyotaamulika ya watu wa kesho, mtoto wa kwanza atachukua majukuu muhimu sana ya 'kutunza' na 'kuendeleza' nasaba za wanajamii wake. Kwa mfano, kutakuwa na uhuru wa watoto wa kike kuchagua wazae na nani na wazae wakati upi. Lakini, tutapendelea ama tuliweke hivi -- watoto wa kike wataombwa na kusititizwa kwamba mtoto wa kwanza wa kuzaliwa awe wa jamii yake ya karibu... Tuseme, kama ni kabila, mtoto wa kwanza awe kazaa na mwanakabila mwenzake... Wanaofuatia, wanawake watakuwa na uhuru wa kuzaa hata nje ya mbari zao... Muafrika atapenda kuzaa na Mzungu, Mhindi, Mjapu, Mchina n.k Vivyo kwa hao. Lakini dunia haitapoteza 'vinasaba' watu kulingana na mchangamano wa watu na usasa, busara itatumika iliyo ni zaidi na nasibu za 'chuki na ubaguzi' wa sura zote. Ni ulimwengu shujaa sana wa kesho, lakini ukifungua moyo na akili yako -- utakirimika kuyajua haya hata leo na sasa... Ulimwengu wa kesho hakutakua na 'ndoa'... Watu watakuwa wanakaa pamoja na kutunza watoto na kaya zao kwa makundi kulingana na shughuli, mapenzi na mapendeleo yao... Wanawake katika ulimwengu wa kesho watakuwa ndiyo nguzo hasa ya 'utawala bora'; wanaume wanakuwa watu wa 'kuweka picha' kupitia visomo na vina vya upeo wa mambo, na wanawake watakuwa ndiyo wenye kubadili 'sura mbegu za kiustawi' kuwa 'stawi halisi.'.. Tendo la kujiaminana katika jamii litakuwa ni jambo linaloangaliwa kwa jicho bora na akili zaidi... Labda wakati mwingine, ningependa nishiriki hili kwa mapana ili kuelimisha...
Basi lije kuwa ni mwendelezo wa shauri la 'Mtoto wa Kwanza'.... Kwa kuwa unapenda mifano ya Israeli, tafiti '
Kibbutzi' --Je, ni jambo gani? Ulimwengu wa kesho utakuwa kama 'kibbutzi', lakini itakuwa bora zaidi... Si kama jaribio letu la '
vijiji vya ujamaa' lilvyobuma... Lakini Mwalimu Nyerere, alikuwa na 'magutu kwa mambo ya kesho'... Tutakuja kujua siku moja, undani wa maisha na wito wake katika kutumikia 'Taifa Changa' ulitokea wapi hasa...
Hmmm