Je, wewe ni mtoto wa kwanza katika familia: Fahamu jinsi Potential yako inavyowindwa ili uharibike

Je, wewe ni mtoto wa kwanza katika familia: Fahamu jinsi Potential yako inavyowindwa ili uharibike

Naomba niongeze kitu kwenye mada hii
Kuna aina mbili za mzaliwa wa Kwanza
1. Mzaliwa wa kwanza kwa CHEO
2. Mzaliwa wa kwanza kwa HAKI

Mzaliwa wa kwanza kwa CHEO ni yule wa kwanza kuzaliwa, yeye hubeba baraka zote za uzao huo na kusudi la Mungu kwa hiyo Familia. Huyu akisimama vizuri na Mungu huwa na maisha flan hivi Amazing na huwa baraka kwa wadogo zake ma wazazi pia.

Mzaliwa wa Kwanza kwa HAKI
Hii ni pale mzaliwa wa kwanza kwa CHeo anapokorofisha mambo, anapoenda kinyume na sheria ya Mungu. Hapa Mungu huinua mtoto mwingine katika familia ili kufikisha kile Mungu alichokusudia katika hiyo familia. Mzaliwa wa kwanza wa aina hii anaweza kuwa hata mtoto wa mwisho kuzaliwa ili mradi Mungu kampa nafasi hiyo. Huheshimika kuliko watoto wengine kwenye familia, huwa ndie Tegemezi wa Familia.

Ahsante sana Mtoa mada
 
Hapa kuna mambo hujaweka sawa.

Mtoto wa kwanza familia maskini

Mtoto wa kwanza familia inayojimudu

Hawa wote ni watoto wa kwanza ila wana majukumu tofauti sana. Ni wazi na kweli siyo kila mtoto wa kwanza anajitoa kwa ndugu zake hasa watoto wa kiume wengi wana wivu na ni natural kwao sababu kaja wakuchukua nafasi yao kwa mama.

Jambo lingine watoto wanakuwa na majukumu kulingana na wingi wao kwenye familia mfano familia yenye watoto 9 hadi 12 hapa kuna makundi mawili ya watoto kifupi familia hii ina familia mbili ndani yake.

Nitafafanua, kadiri watoto wanavyokuwa wengi ndivyo wanavyogawanyika kulingana na umri waliopishana, watoto wanaopishana umri mdogo huwa wanakuwa pamoja.

Habari ya baraka na mikosi ni nadharia, tuangalie upande wa sayansi pia kwa yanayoonekana.

Watoto wa kwanza wengi na wamwisho pia wengi wa kiume wana matatizo kulingana na jamii inavyowaaminisha kujiona spesho.
 
Nitatofautiana na hii dhana ya ukutaka kuangusha familia uta dili na mzaliwa wa kwanza.

Hii dhana naikataa kwa sababu mzawa wa kwanza ukijaribu kuangalia vizuri utagundua familia haimthamini kama wanaomfuata sasa why utake kuangusha familia kwa asiyethaminiwa??

Kuna mzaliwa ambaye huwa ana nguvu kubwa zaidi ya mzaliwa wa kwanza, na hawa wengi ni wazaliwa wa katikati mfano kwenye watoto watatu mzaliwa wa pili, kwenye watano mzaliwa wa pili na wanne hawa huwa ni kiungo cha familia nzima.

Na hii inatokana na nature kuwafanya wawe na uwezo wakuchangamana tangu utotoni sana sasa hawa wakiwa watu wazima ndio unakuta wana sauti sana na kwa vile wengi ni rahisi kufanikiwa kutokana na asili yao kuchangamana zinakuja dhana za kusaidiwa na wakubwa wao kumbe sivyo ni uwezo wao asili wa kujichanganya na kushawishi ndio unawafanya wafanikiwe. Hii ni sayansi ya kawaida kabisa

Kuna sehemu nakubaliana na wewe ila ipo sehemu kubwa natofautiana na wewe
 
Akhsante kwa uzi murua ..Hebu liweke sawa hilo la mzaliwa wa kwanza,kuna mkanganyiko maana unaweza kuta mama aliolewa mara mbili na kila mtoto akawa wa kwanza kwa baba yake au baba ana wake wawili na kila make ana mtoto wa kwanza.je hapo tunampataje mzaliwa wa kwanza kwenye familia kama hizo?
Au mzaliwa wa kwanza anatoka kwa baba au mama?
Naomba kuwasilisha
 
client3 ent3 jibu hili swali please
 
Kila mtu kwa Mungu ana hadhi sawa. Tofauti zinazoweza kuwa za vipaji zina lengo la kutajirishana kwa manufaa ya wote.

Hakuna mtu bora kwa maana ya hadhi ya binadamu kwa Mungu.

Mawazo kwamba wazaliwa wa kwanza ni potential au hawafanikiwi katika uchumi nakadhalika hayana ukweli wowote; ni hisia tu.

Mungu amemuumba mtu kwa lengo moja tu, mtu amjua, ampenda na amtumikie.

Kuna vitu vinavyofanya mtu awe potential au kinyume chake. Katika hivyo vitu wazazi wakichukuwa nafasi ya kwanza na jamii ndio huandaa mwelekeo wa mtoto.
Hapa kuna suala la elimu, mafundisho na uelewa wa mambo. Elimu, mafundisho na uelewa mambo ukikosekana watoto huangamia.
Kweli kabisa yote hutokea na namna malezi ya watoto yalivyo....namshukuru Mungu baba yetu alikuwa mtu aliyemtumainia Mungu,alilea watoto katika Imani na kutusaidia kufikia malengo,wote Mungu katuinua,hakuna aliye mzigo kwa mwenzake,mzaliwa wa Kwanza kasimama na YESU hakuna kuteseka bali YESU kawa kiongozi wa familia yetu...nashukuru wazazi wote wawili kusimama na sisi kimwili na kiroho..Amen
 
Kuzaliwa wa kwanza ni lango la baraka yaani utumishi na utajiri na siyo majukukmu ya kulea wazazi na wadogo zako
Na Hilo inategemeana unamtumainia vipi Mungu wako,maana Kama hujamuita asimame na wewe Kama lango Bali lango unaendeshwa na nguvu za giza na tamaa za ulimwengu huo,uzaliwa wa Kwanza wenye nguvu ya Mungu utatoa wapi? Yapo malango au wazaliwa wa Kwanza waliosimama na YESU angalia walivyobarikiwa,hili neno ukilichukulia kiroho utafunguliwa,ukichukulia kimwili utaishia kulalamika katika nafasi yako..
 
Samahani ivi nabii au mitume wa Mungu wana cheo kikubwa kwa Mungu kuliko waamin wengine?
 
FB_IMG_15973396663790159.jpg
 
Mimi Ni mzaliwa wa kwanza Vita ninavyopigana kwenye Hilo life MUNGU tu anajua.

Naamini nitashinda soon maana mimi akili ninayo sio kilaza

Sio mnywaji

sio mlevi

Sijawahi vuta hata kipisi Cha sigara

Ila shida yangu iko pale Kati patamu [emoji2]

Kwakweli MUNGU nipiganie niachane na hij kitu[emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kati ndio ulevi wako wala huwezi kuacha.[emoji1][emoji1]
 
Samahani ivi nabii au mitume wa Mungu wana cheo kikubwa kwa Mungu kuliko waamin wengine?
Hakuna utofauti kabisa isipokuwa wote wanatakiwa kumwabudu Mungu katika roho na kweli.hata hao waamini wengine Kuna kitu ambacho kwa nafasi waliyopo wanasaidia katika kutenda kazi ya Mungu..cha msingi ni Imani iende sanjari na matendo...hicho ndicho kipimo cha mkristo yoyote haijalishi anakazi gani katika shamba la Mungu...
 
Imani iende sanjari na matendo yapi? Na ivi Mungu kusema kuwa katuwekea roho wake ndani yetu na anatuongoza kwa njia ya roho wake, unaelewaje?
 
Back
Top Bottom