Je, wewe ni Mzaliwa wa Kigoma? Fanya haya ili uraia wako usitiliwe shaka yoyote na wabaya wako

Je, wewe ni Mzaliwa wa Kigoma? Fanya haya ili uraia wako usitiliwe shaka yoyote na wabaya wako

Sija wafanananisha na hamas , alafu ngoja nikwambie kitu hamas unao waona wewe ni magaidi Kuna watu wanaeaona ni wakombozi wao the same hao unaowaona ni wema kwa kua wameishi miaka na miaka Kuna watu wanawaona sio watanzania na bado wanauzalendo na taifa lao la asili hivyo ni Bora wakakae huko huko kwenye taifa lao la asili

No hate ✌️
Unafikiri kujaza nchi ubaguzi na chuki ndo kutaleta nafuu ya maisha? Tukimaliza kubagua hao who next? Waarabu, wahindi, wasomali au wazenji? Ubaguzi ukiulea hautaishia hapo bali mwishowe utabagua hata watoto wako mwenyewe wa kuwazaa
 
kiukweli nilikuwa sifahamu mpaka nilipo enda kujiridhisha kwa kuangalia ramani. lakini mbona Kagera wapo karibu na Rwanda lakini kagera wana ka unafuu...awasumbuliwi sana kwenye maswala ya uraia.​
Inawezekana wameweka nguvu kubwa sana Kigoma kwa sababu ya muingiliano wake na Kongo ukiangalia Kongo ni taifa kubwa na Lina idadi kubwa sana ya watu wanao ingia Tanzania,Mfano wakimbizi

Ukilinganisha na muingiliano kati ya Kagera na Rwanda
 
Tatizo ni Watusi na sera Yao ya kuleta vita kwa nchi jirani. Wayamiaji wengi ni Wahutu toka Congo na Burundi. Hao wameishi kwa amani sana na wenyeji nanpia Mihutu anafanana sana na Makabila mengine ya Tanzania kama msukuma na Wengine tu. Mihutu Huwa na uhalifu kama uhalifu mwingine unaowwza kufanya n'a mkinga au mgogo.

Tatizo ni Hao Watusi na wengi wao ni kutoka Rwanda.

Watusi wanakuja wakiwa wamejipanga. Na wanapenyezwa kimkakati.
 
View attachment 2881093

Ukishazaliwa Kigoma au ukiwa na asili ya Kigoma jambo la kwanza unalotakiwa kuwa nalo (kichwani) kabla ya yote unatakiwa kuwa na uelewa mzuri wa maswala ya elimu ya uraia na utaifa. Kwasababu hiyo ndio fitina ya kwanza utakutana nayo pindi tu ukihitaji kujitanua kihimaya. Uraia ndio fimbo ya kwanza utayocharazwa nayo.

Mambo muhimu ni kuhakikisha kwamba makaburi ya wazee wako yanahifadhika kwa pande zote (ubabani na umamani). Hakikisha kwamba nyumba za wazee wako zinahifadhika haziuzwi wala kuvunjwa. Hakikisha kwamba ardhi yenu mnaitunza vyema, kumbukumbu za picha na mabaki ya historia muyahifadhi ipasavyo.

Watoto zenu anzeni kuwafundisha mapema namna ya kukabiliana na kasumba hii ya uraia inayotumiwa kama silaha kuwadhoofisha watu wa Kigoma.

Kwanini tunashauri mambo haya? Ni kwasababu nchi yetu pendwa bado haina njia sahihi ya kufanya verification ya uraia hususan kwa watu walio mipakani. Usumbufu umekithiri mno, na sasa imekua kasumba endelevu.

Sio ajabu tena muhamiaji haramu kuingia nchini, kupata haki zote kinyemela ikiwemo kuajiriwa na kuteuliwa katika nafasi za maamuzi.

Hawa watu wanapataje nguvu hiyo?
...........
Hivyo ni muhimu kwa Serikali kuweka mifumo mizuri kwa watu wa mipakani, hususan huku kwetu Kigoma na watu wenye asili ya Kigoma.

Cha kushangaza katika kasumba hii ya uraia huwakuti Wajaluo, Wamasai, na watu wa Kusini. Kwanini muda wote Kigoma na marachache Kagera. Kwanini wahamiaji haramu wa mkoa wa Kigoma na Kagera wanaogopwa sana, tofauti na Mara, Arusha, Ruvuma na Mtwara?.

Mwaka 2014 Tanzania ilitangazwa kuwapa uraia wakimbizi 162,000 wa Burundi kwa mkupuo.

Idadi ya watu waliopewa uraia ilifikia 200,000, rekodi ambayo haijawahi kutokea mpaka muda huu kwa mujibu wa shirika la wakimbizi wa Umoja wa Mataifa UNHCR.

Kama tunawapa watu uraia kwanini hakuna mifumo mizuri ya utambuzi kwa watu hawa? Kwanini bado wenyeji wenye asili ya Kigoma wanapitia madhila na kasumba ya uraia hadi sasa?

Kasumba hii imepelekea hofu kwa watu wa Kigoma, leo mtu wa Kigoma hawezi kuthubutu kusema kwamba ana ndugu Congo au Burundi.

Ukienda Musoma, wajaluo na wakurya, wengi wamesoma hadi shule za Kenya, wana ndugu zao Kenya na Tanzania na wala hawapati usumbufu au ukakasi wowote.

Ukienda Mtwara, Wamakonde na Wayao wapo pande zote mbili za Msumbiji na Tanzania, wala hakuna shida.

Ukienda Mbeya kuna muingiliano mkubwa sana na Wazambia na Wamalawi, wameoleana mno, wafanyabiashara wengi wa Lusaka ni Wakinga na Wanyakyusa, na wanaongea kinyakyusa, kikinga na kiswahili hiki cha kwetu na likizo za mwaka huwa wanarudi na hawafanywi kitu kwasababu wanalipa kodi kule Zambia.

Leo hapa mwanakigoma apite mpakani aseme naenda kusalimu ndugu zangu Burundi au naenda kwa ndugu zangu Congo. Basi na yeye atajumuishwa kuwa ni Mrundi au Mkongo.

Ukienda Moshi kwa Wachagga, na Wameru, sio ajabu majina ya koo kuingiliana pande zote mbili Tanzania na Kenya, nchi ya Kenya kuna eneo na kabila la Wameru.

Ni kawaida sana kumkuta mtu wa Tanga au Zanzibar ana ukoo wa mashangazi na wajomba huko Mombasa Kenya.

Mikoa ya mipakani ni kawaida kuwa na watu wa nchi zote kwasababu watu wanaoleana, wanafanya biashara pamoja, wanazaliana na wengine wanahamia kabisa. Lakini huku kwetu Kigoma mambo yanakua ni tofauti. Dhiki na manyanyaso ya uraia yanazidi.

Je! serikali inasubiri nini kutatua fumbo hili la muda mrefu kwa wakazi wa asili ya Kigoma?

Ukijitambulisha wewe ni mtu wa Kigoma chakwanza kabisa mtu anakufikiria kunako uraia. Kanakwamba watu wa Kigoma ni raia daraja la pili. (Inaumiza sana kihisia na kiakili pindi unapowekewa mashaka).

Kigoma Region Tanzania
Mm ni mtanzania.Lakin pale Uganda kuna, kabira yetu wengi sana. Haya Mambo Nyerere, aliyakataa. Nyerere mwenyewe alitokea Rwanda na kuja Musoma. Wajita wakawaita vijanaki. Yaan waliokuja na nn. Leo tunaanzisha debate za Kipumbavu.
 
Mimi ni mtanzania. Lakini pale Uganda kuna, kabira yetu wengi sana. Haya Mambo Nyerere, aliyakataa. Nyerere mwenyewe alitokea Rwanda na kuja Musoma. Wajita wakawaita vijanaki. Yaan waliokuja na nn. Leo tunaanzisha debate za Kipumbavu.
Kwahiyo kama Nyerere alikua mnyarwanda hiyo inatosha kuruhusu wanyarwanda waingie nchini bila utaratibu, tatizo la wstusi ni kutaka kutawala na kuua wenyeji wao.
 
Ati wamepewa uraia watu zaidi ya 200,000? Huo ni uraia hewa ndugu yangu kutengwa kupo pale pale miaka ya 70's watusi waliokuwepo kagera hasa kambi ya kimuli walipewa uraia na nyerere basi wakaishi mpaka wakazeeka na kufia hapo kagera sasa mwaka 2006 vizazi vyao vilivyobaki vikasombwa na kupelekwa Rwanda kwamba ni wahamiaji haramu wanarudishwa kwao, wengi wao hajui hata lugha ya kinyarwanda hawana ndugu huko ila ikabidi wapekwe tu
Hahahah...
Mambo ya ajabu sana haya!

Nadhani hii ya kutoaminika watu wa huko inachangiwa na ile hulka ya warundi na wanyarwanda walio nchini Tz kupenda kufanya uhalifu mkubwa, mfano kutumia silaha nzito za vita kuteka magari ya abiria na mizigo na kupora.

Kuna wakati magari yalikuwa hayawezi kukatiza baadhi ya mapori ya huko bila kusindikizwa na askari wenye silaha.
 
Mbeya, Songwe, Mara na Kilimanjaro nazo zimepakana na nchi jirani na kuoa na kuolewa ni jambo la kawaida sn, mbona hakuna usumbufu wowote?
Nchi jirani na maeneo hayo zipo stable na raia wake hata kama ataingia wengi wao wanarudi walipotoka na wana mahusiano ya kindugu mfano Wakurya wa Tz/Wakurya wa Kenya, Wajaluo wa Tz/Wajaluo wa Kenya, Wamasai wa Tz/Wamasai, Wanyambo wa Karagwe / Wanyankore wa Uganda huwa Kuna vi-favor visivyo rasmi kutokana na mahusiano ya moja Kwa moja ya kiutamaduni kabla na baada ya Uhuru hasa ukizingatia tulikuwa chini ya koloni la Uingereza lakini Kuna watu wanakuwa Wana vinasaba vya karibu tangu enzi na enzi
 
Nchi jirani na maeneo hayo zipo stable na raia wake hata kama ataingia wengi wao wanarudi walipotoka na wana mahusiano ya kindugu mfano Wakurya wa Tz/Wakurya wa Kenya, Wajaluo wa Tz/Wajaluo wa Kenya, Wamasai wa Tz/Wamasai, Wanyambo wa Karagwe / Wanyankore wa Uganda huwa Kuna vi-favor visivyo rasmi kutokana na mahusiano ya moja Kwa moja ya kiutamaduni kabla na baada ya Uhuru hasa ukizingatia tulikuwa chini ya koloni la Uingereza lakini Kuna watu wanakuwa Wana vinasaba vya karibu tangu enzi na enzi
Ok
 
Wamejazana Mno Mishamo Huko, Nambuka Jiwe Aliwakataa Kuwapa Uraia Akawaambia Wazi Mnamiliki Mpaka Silaha Tutawanyoosha Hakuna Uraia View attachment 2881102View attachment 2881104
Mbona wale wa Katumba Katavi wamepewa Uraia wakati hawana tofauti na wa Mishamo,tena hawa wa Katumba ni Magufuli mwenyewe ndio aliwapa uraia. Mwaka jana Uhamiaji ilipitisha fagio kwa wale Waha wauza maziwa na wakopesha bidhaa mitaani kuanzia Tegeta mpaka Temeke wengi walitokea Mishamo katavi ambapo kiukweli si RAIA wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom