Je, wewe ni Mzaliwa wa Kigoma? Fanya haya ili uraia wako usitiliwe shaka yoyote na wabaya wako

Je, wewe ni Mzaliwa wa Kigoma? Fanya haya ili uraia wako usitiliwe shaka yoyote na wabaya wako

Mbona sijaishi Kigoma na naona waha wanasumbuliwa hata huku kwetu? akionekana tu anaitwa Ndikumana anaitwa uhamiaji, hata mimi kwetu ni mpakani sn lakini hakuna usumbufu wowote na tuna vuka na kurudi salama

Nenda uhamiaji

Uone hao wahaya wanavopata shida. Dada yangu aliolewa na muhaya wa karagwe hadi leo watoto zake wanasumbuliwa kipata passport
Bashungwa sijui alichomoka vipi


Walee jamaa wengi sio watz

Hawana public figure wengi km waha ndio maana husikii ishu zao
 
Wamasai wa Tz na Kenya wanatofauti gani? umewahi kuona masai anahojiwa uraia wake au mwarabu yoyote? nadhani kuna shida zaidi

Hujui kitu kaaa kimya

Sio kwa sababu husikii means haipo, mbona unakuwa kiazi hivo

Hebu nenda uhamiaji
 
View attachment 2881093

Ukishazaliwa Kigoma au ukiwa na asili ya Kigoma jambo la kwanza unalotakiwa kuwa nalo (kichwani) kabla ya yote unatakiwa kuwa na uelewa mzuri wa maswala ya elimu ya uraia na utaifa. Kwasababu hiyo ndio fitina ya kwanza utakutana nayo pindi tu ukihitaji kujitanua kihimaya. Uraia ndio fimbo ya kwanza utayocharazwa nayo.

Mambo muhimu ni kuhakikisha kwamba makaburi ya wazee wako yanahifadhika kwa pande zote (ubabani na umamani). Hakikisha kwamba nyumba za wazee wako zinahifadhika haziuzwi wala kuvunjwa. Hakikisha kwamba ardhi yenu mnaitunza vyema, kumbukumbu za picha na mabaki ya historia muyahifadhi ipasavyo.

Watoto zenu anzeni kuwafundisha mapema namna ya kukabiliana na kasumba hii ya uraia inayotumiwa kama silaha kuwadhoofisha watu wa Kigoma.

Kwanini tunashauri mambo haya? Ni kwasababu nchi yetu pendwa bado haina njia sahihi ya kufanya verification ya uraia hususan kwa watu walio mipakani. Usumbufu umekithiri mno, na sasa imekua kasumba endelevu.

Sio ajabu tena muhamiaji haramu kuingia nchini, kupata haki zote kinyemela ikiwemo kuajiriwa na kuteuliwa katika nafasi za maamuzi.

Hawa watu wanapataje nguvu hiyo?
...........
Hivyo ni muhimu kwa Serikali kuweka mifumo mizuri kwa watu wa mipakani, hususan huku kwetu Kigoma na watu wenye asili ya Kigoma.

Cha kushangaza katika kasumba hii ya uraia huwakuti Wajaluo, Wamasai, na watu wa Kusini. Kwanini muda wote Kigoma na marachache Kagera. Kwanini wahamiaji haramu wa mkoa wa Kigoma na Kagera wanaogopwa sana, tofauti na Mara, Arusha, Ruvuma na Mtwara?.

Mwaka 2014 Tanzania ilitangazwa kuwapa uraia wakimbizi 162,000 wa Burundi kwa mkupuo.

Idadi ya watu waliopewa uraia ilifikia 200,000, rekodi ambayo haijawahi kutokea mpaka muda huu kwa mujibu wa shirika la wakimbizi wa Umoja wa Mataifa UNHCR.

Kama tunawapa watu uraia kwanini hakuna mifumo mizuri ya utambuzi kwa watu hawa? Kwanini bado wenyeji wenye asili ya Kigoma wanapitia madhila na kasumba ya uraia hadi sasa?

Kasumba hii imepelekea hofu kwa watu wa Kigoma, leo mtu wa Kigoma hawezi kuthubutu kusema kwamba ana ndugu Congo au Burundi.

Ukienda Musoma, wajaluo na wakurya, wengi wamesoma hadi shule za Kenya, wana ndugu zao Kenya na Tanzania na wala hawapati usumbufu au ukakasi wowote.

Ukienda Mtwara, Wamakonde na Wayao wapo pande zote mbili za Msumbiji na Tanzania, wala hakuna shida.

Ukienda Mbeya kuna muingiliano mkubwa sana na Wazambia na Wamalawi, wameoleana mno, wafanyabiashara wengi wa Lusaka ni Wakinga na Wanyakyusa, na wanaongea kinyakyusa, kikinga na kiswahili hiki cha kwetu na likizo za mwaka huwa wanarudi na hawafanywi kitu kwasababu wanalipa kodi kule Zambia.

Leo hapa mwanakigoma apite mpakani aseme naenda kusalimu ndugu zangu Burundi au naenda kwa ndugu zangu Congo. Basi na yeye atajumuishwa kuwa ni Mrundi au Mkongo.

Ukienda Moshi kwa Wachagga, na Wameru, sio ajabu majina ya koo kuingiliana pande zote mbili Tanzania na Kenya, nchi ya Kenya kuna eneo na kabila la Wameru.

Ni kawaida sana kumkuta mtu wa Tanga au Zanzibar ana ukoo wa mashangazi na wajomba huko Mombasa Kenya.

Mikoa ya mipakani ni kawaida kuwa na watu wa nchi zote kwasababu watu wanaoleana, wanafanya biashara pamoja, wanazaliana na wengine wanahamia kabisa. Lakini huku kwetu Kigoma mambo yanakua ni tofauti. Dhiki na manyanyaso ya uraia yanazidi.

Je! serikali inasubiri nini kutatua fumbo hili la muda mrefu kwa wakazi wa asili ya Kigoma?

Ukijitambulisha wewe ni mtu wa Kigoma chakwanza kabisa mtu anakufikiria kunako uraia. Kanakwamba watu wa Kigoma ni raia daraja la pili. (Inaumiza sana kihisia na kiakili pindi unapowekewa mashaka).

Kigoma Region Tanzania
Waha:

1. Ni wabishi, wanabishana hata na redio wakati habari ya redio inakuwa imepitia mchakato wa ukusanyaji, utafiti, uhariri ndipo hutangazwa.

2. Waha wanabeba mizigo kama Kombamwiko na msururu wa watoto, waliopishana mwaka na vijibwa na vimbuzi.

3. Wana ardhi nzuri ya kilimo lakini wanaitelekeza na kwenda kulima vibarua Tanga kwenye mashamba ya MO ya katani, walitelekeza mawese kwa ajili ya katani kama Mkwere anavyouza nanasi ili anunue mua atafune.

4. Wanabishana hata na CCM yenye Kamati ya Maadili ambayo ina nguvu kuliko Mahakama ya Rufaa.

5. Jina la utani la "mwisho wa reli" limewafanya kuwa mwisho kikwelikweli katika mambo mengi e.g. SGR, Gridi ya taifa, chuo cha VETA, barabara ya lami, kiwanja cha ndege, ujenzi wa daraja kubwa la kimkakati mto Malagarasi (Kikwete Bridge). Serikali isiwapelekee SGR ya abiria watalazimisha kuingiza vijibwa humo, wapelekewe MGR tu kwa ajili ya abiria.

6. Zitto mbishi, Kabourou mbishi, Machali mbishi, Kafulila mbishi, Mondi mbishi.

7. % kubwa ya watoto wa kiume wanaozaliwa kuanzia 2021 wanawaita "Mpango"

8. Wana uchawi wa kuchukuwa kivuli chako hadi umlipe ela yake vinginevyo anakuondoa kwenye sayari.

9. Wanapenda kubeba mafurushi makubwa na watoto kibao wanaopishana mwaka mmoja tu; na kulazimisha kulipa nauli 1 ya mtu mzima tu bila mizigo na utitiri wa watoto. Mabasi mengi hayaendi huko kwa sababu yao. Wanalazimisha kuingia kwenye gari hata na vijibwa vyao.

10. Makarani wa sensa na wa kuboresha Daftari la Mpigakura hawapendi Kigoma kwa sababu ya ubishi wa Waha.

11. Kiboko ya Muha ni Mmanyema.

12. Makabila mengi ya mipakani yanakuwa na uraia pacha kwa siri kali.
Screenshot_20240124-225912.jpg
 
Nenda uhamiaji

Uone hao wahaya wanavopata shida. Dada yangu aliolewa na muhaya wa karagwe hadi leo watoto zake wanasumbuliwa kipata passport
Bashungwa sijui alichomoka vipi


Walee jamaa wengi sio watz

Hawana public figure wengi km waha ndio maana husikii ishu zao
Wahaya hawana public figure na masifa yao? siyo kweli
 
Just imagine hata VP anatiliwa shaka kuwa ni Mrundi.
 
75% ya wakazi duniani ni wahamiaji unaweza ukajiona si mhamiaji Kwa sababu Babu zako huenda walifika mapema kabla ya wengine.
 
Back
Top Bottom