Je, wezi wa Wizara ya fedha wameshafahamu aina ya Rais tuliyenaye?

Hii typicaly ndiyo yalikuwa maisha kipindi cha utawala wa Kikwete. Maofisini watu walikuwa wanatafuta visingizio vya kulipana posho. Mheshimiwa Samia asipokuwa makini na mkali hali inaweza kuwa mbaya hata zaidi ya kipindi cha Kikwete.
Kumbuka tumesha kubaliana tuachie pesa ije mtaani,saa hizi kuna wengine wamepata bahati huko mtaani Mzigo wa Wizara ya fedha nao umewafikia! Kama kuna mafundi Ujenzi au mafundi Magari saa hizi nao wanawapiga pesa Watumishi wezi wa fedha za Umma!!
 
Umetoa mfano mzuri sana, kongole, nadhani hii ingewekwa kama mstari wa utangulizi kwenye magazeti ya kesho, ndugu zangu kule kijijini wangelielewa vizuri kilichotokea
 
Mod., Unawezaje kui-pin thrd hii ili ibaki juu kwa siku kadhaa zijazo? Hawa nyani sasa hawaogopi mlinzi bandia!
 
Ivi izi connection za huko zinapatikanaje NIMEJIONA FALA GHAFLA
 
nashauri wapige haswa tena haswa ...wenye nchi wamesema wana amani kipingi cha magu hawakuwa na hiyo amani hivyo hawana haja na hela yeyote ile kwa hiyo wakwapuaji kazi kwenu
 

Dotto James amekula hii nchi sana kwa miaka mitano ilikuwaje. Na waziri mkuu anasema hapo bado kuhamisha pesa za miradi. Tatizo katibu mkuu alikuwa anapigiwa kifua na Hayati hivyo hakuna aliyesubiri kuhoji Mama Samia tumshukuru kwa kuagiza uchunguzi yaani haya ni machache kwenye uchunguzi 🤔 huu ndiyo tunaita mfumo yaani Hayati hakutaka wizara hii ichunguzwe
 
Kwani mkuu lini wizi uliisha?kama ungekuwa umekwisha ripoti ya CAG, isingekuwa vile ilivyo kwa 2019/2020!sema tu ilikuwa ni marufuku kuu ripoti, kwa kumuogopa jiwe, hivyo watu wakaaminishwa kuwa hakukuwa na pesa ya serikali iliyoibiwa!!sasa awamu ya sita inaamini ktk uwazi ndio maana mtaanza kusema hivyo kuwa hawamuogopi kumbe ni uwazi ambao jiwe hakuupenda!!kinachotakiwa hao wabadhirifu ikibainika kweli wamekula pesa ni adhabu kali sana wapewe.Tena hakuna kipindi ambacho pesa imeliwa kama cha awamu ya tano kwa taarifa yako.yaani ingetokea ikafanyika special audit ya miaka 5, iliyopita watu watazimia kwa kutoamini ubadhirifu mkubwa wa pesa.
 
Sorry! Huyu Katibu mkuu aliingia lini na yule Dotto aliondoka lini? Nauliza kwa kuwa naona upigaji umekuja hadi mwezi huu, Mei. Kama walianza Dotto akiwepo, ina maana yalikuwa mazoea yao kwa miaka yote na nitakuunga mkono kwa nguvu zote.
 
Sorry kuweka kumbukumbu sawa. CAG wakati wa kikwete aliitwa Utoh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…