Je, Yanick Bangala Sasa ni Rasmi Yanga?

Je, Yanick Bangala Sasa ni Rasmi Yanga?

Chige

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2008
Posts
13,495
Reaction score
29,872
Wakati Yanga wakielekea kumtambulisha Djuma Shabani pamoja na Jesus Moloko, wakala Mwenye orodha ndefu ya Wachezaji wa DRC, keshatuwekea picha hapo ili simulizi tuandike wenyewe!!

Kama inavyoonekana hapa chini, Faustin Mukandila anatujuza time is loading kabla Yanick Bangala Litombo, hajatangazwa kuhamia klabu inayopiga uzi wa kijani na njano!!

Bangala, ambae umri wa kwenye passport unaonesha ana miaka 27, kwa sasaanakipiga FAR Rabat kama Defender.


Bangala.png



UPDATETS
Finaaly, Wakala wa Djuma Shabani athibitisha DEAL DONE....

Habari chungu namna hii inabidi zimfikie ndugu denooJ popote pale alipo!!


Djuma.png
 
Kila la heri Wananchi. Muhimu tu msirudie makosa ya msimu uliopita. Maana mbumbumbu wanachonga sana.
 
Kila la heri Wananchi. Muhimu tu msirudie makosa ya msimu uliopita. Maana mbumbumbu wanachonga sana.
Binafsi sioni kama ni makosa makubwa sana, kwa sababu ambapo naweza kusema bila shaka kwamba tulipigwa ni kwa Sarpong!

Carlinhos hadi kesho namkubali, sema ndo hivyo tena!!

TK, Mukoko, na Yacouba walikuwa nguzo muhimu kwa timu!!

Saidi Ntibazonkiza bado naamini ni asset!!

Fiston, of course pale vilevile tumepigwa lakini sidhani kama alipata muda wa kuonesha uwezo wake hasa ukizingatia alikotoka ligi ilikuwa imesimama, kaja Bongo ambako watu hatuna muda wa kusubiri mchezaji eti azoee mazingira!!
 
Utopolo shida sana.

Yale maduka yetu naona mmeyatimua, sijui siri kavujisha Dr. H. Manara!

Safari hii Boss Mo anaweza akatususa.
Akisusa atakuwa mjinga, kwa sababu ukiingia kwenye soka lazima ukubali yote!!! Soka ni kama siasa tu... hususani soka ya vilabu vikubwa vinavyomilikiwa na wanachama!! Kote huko, unaweza kuingia wakati unaheshimika kweli kweli mbele ya jamii, lakini ndani ya mwezi mmoja tu, ukaanza kuonekana kama takataka!!

Hata hivyo, lazima niwapongeze kwa kutoendelea zile kansa mbili kwenye ligi yetu 🤣 🤣 🤣 , hususani ile kansa ya Msumbiji manake hakuna kansa iliyokuwa inaninyima raha, kama ile... !!!
 
UPDATES:

Faustin Mukandila, ambae ndie Wakala wa Djuma Shaban, hatimae amethibitisha DEAL DONE kati ya Djuma na Dar Young Africa!!

Djuma.png
 
King Dododoo Labush aisajili timu ya Yanga kwenye umoja wa wacongo wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom