Je, Yesu na Paulo wangekuwepo "live" duniani leo, wangecheza au kushabikia mpira?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Enyi Wakristo, leo nimewafuata hukuhuku, najua mpo wengi kwenye jukwaa hili la Sports. Please, naomba kwa dakika moja tuzungumze jambo muhimu kuhusiana na soka.

Soka ni mchezo unaofurahisha na kuwaunganisha watu wengi duniani. Lakini, je, mmewahi kujiuliza kama Bwana wetu Yesu Kristo na mtume Paulo wangekuwepo katika mitaa yetu leo, wangetumia muda wao kila weekend kushabikia mpira?

Yesu alipokuwa duniani hakupoteza muda wake kwenye mambo yasiyo na faida ya milele; alijitoa kufundisha, kuponya na kuhubiri habari njema ya wokovu katika miji na vijiji (Mt 9:35). Hata usiku badala ya kupumzika, alienda mlimani kuomba (Luka 6:12). Mtume Paulo naye, alitangaza wazi kuwa maisha ya dunia hii ni kama kinyesi tu akiyalinganisha na thamani ya kumjua Kristo (Wafilipi 3:8).

Maandiko yanatuambia tuukomboe wakati kwakuwa nyakati hizi ni za uovu. Kwahiyo tutumie muda mwingi zaidi kushabikia mambo ya rohoni. Jiulize ndugu yangu: Je, nguvu unayoitumia kushangilia goli likifungwa, ndiyo nguvu hiyohiyo unayoitumia kushangilia mwenye dhambi mmoja akitubu na kumpokea Kristo? Muda unaoutumia kila Jumamosi na Jumapili kukaa mbele ya screen na kutazama mpira, ndio muda unaoutumia kutimiza agizo kuu la Yesu katika Mt 28:19-20?
 
Mazoezi ni sehemu moja wapo ya kutibu mwili, muulize huyo huyo Paul aliandika kuhusu hiko
 
Mpira wa kulipwa au hata wa kujitolea tu.?
 
Unamfaham Paul Scores
kama yesu angekuwepo basi angekuwa ni straika na assist nyingi kama mzize!
 
Mazoezi ni sehemu moja wapo ya kutibu mwili, muulize huyo huyo Paul aliandika kuhusu hiko
Kuna tofauti kubwa kati ya mazoezi na ushabiki. Ukikaa mbele ya screen unaishabikia Man Utd unafanya mazoezi gani ya kutibu mwili?

Isitoshe Paulo anasema mazoezi ya mwili yanafaa KIDOGO.
1 Timotheo 4:8
Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
 
Enyi Wakristo, leo nimewafuata hukuhuku, najua mpo wengi kwenye jukwaa hili la Sports. Please, naomba kwa dakika moja tuzungumze jambo muhimu kuhusiana na soka.

Soka ni mchezo unaofurahisha na kuwaunganisha watu wengi duniani. Lakini, je, mmewahi kujiuliza kama Bwana wetu Yesu Kristo na mtume Paulo wangekuwepo katika mitaa yetu leo, wangetumia muda wao kila weekend kushabikia mpira?

Yesu alipokuwa duniani hakupoteza muda wake kwenye mambo yasiyo na faida ya milele; alijitoa kufundisha, kuponya na kuhubiri habari njema ya wokovu katika miji na vijiji (Mt 9:35). Hata usiku badala ya kupumzika, alienda mlimani kuomba (Luka 6:12). Mtume Paulo naye, alitangaza wazi kuwa maisha ya dunia hii ni kama kinyesi tu akiyalinganisha na thamani ya kumjua Kristo (Wafilipi 3:8).

Maandiko yanatuambia tuukomboe wakati kwakuwa nyakati hizi ni za uovu. Kwahiyo tutumie muda mwingi zaidi kushabikia mambo ya rohoni. Jiulize ndugu yangu: Je, nguvu unayoitumia kushangilia goli likifungwa, ndiyo nguvu hiyohiyo unayoitumia kushangilia mwenye dhambi mmoja akitubu na kumpokea Kristo? Muda unaoutumia kila Jumamosi na Jumapili kukaa mbele ya screen na kutazama mpira, ndio muda unaoutumia kutimiza agizo kuu la Yesu katika Mt 28:19-20?
Ndugu Setfree; Roho ndio itiayo uzima, mwili haufai kitu (Yn 6:63.)
Yesu angekuwepo hapa duniani zama hizi, bila shaka angetumia technolojia iliyopo e.g. Simu, Mitandao, Vyombo vya moto badala ya punda na hata kufundisha kwake kwa mifano angetumia vile vitu watu wanavijua au kuvitumia mara nyingi ikiwepo mpira, bao, n.k. Sio vyema sana ukamwekea mipaka eti hakupoteza muda. Usisahau kuna mahali aliwaambia wanafunzi wake wapumzike kidogo baada ya kutoa ripoti ya kazi aliyowaagiza. Je, katika kupumzika kwao hao wanafnzi walikuwa wakifanya nini? (sio kulala au kusali) (Marko 6:31.)
 
Asante Iyerdoy kwa kuchangia mada.
Hiyo sura ya 6 ya Marko naomba tuisome tena pamoja kuanzia mstari wa 31 hadi wa 45 halafu uniambie ni mstari wa ngapi wanafunzi walipumzika:
31Akawaambia, Njooni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula. 32 Wakaenda zao faragha mashuani, mahali pasipokuwa na watu. 33Watu wakawaona wakienda zao, na wengi wakatambua, wakaenda huko mbio kwa miguu, toka miji yote, wakatangulia kufika. 34 Naye aliposhuka mashuani, akaona mkutano mkuu, akawahurumia; kwa sababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi. 35 Hata zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa; 36uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula. 37Akajibu, akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakamwambia, Je! Twende tukanunue mikate ya dinari mia mbili ili tuwape kula? 38Akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakasema, Mitano, na samaki wawili. 39Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabichi. 40Wakaketi safu safu, hapa mia hapa hamsini. 41 Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandalie; na wale samaki wawili akawagawia wote. 42Wakala wote wakashiba. 43 Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili; na vipande vya samaki pia. 44Na walioila ile mikate walikuwa wanaume elfu tano. 45 Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande mashuani, watangulie kwenda ng'ambo hata Bethsaida, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. 46Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba.

SOMA KWA MAKINI HAYO MANENO NILIYOYAWEKEA BOLD
Utaona wazi kuwa wanafunzi hawakupumzika.
Ni kweli Yesu aliwaambia wapumzike kidogo. Lakini hata hiyo kidogo hawakupumzika. Kule walikokuwa wanakwenda kupumzika, watu walitangulia kufika kwa miguu. Mkutano wa Injili ukaanza. Zikapita saa nyingi za mchana. Yesu akawaambia wawaketishe watu. Akawaambia wawagawie ile mikate. Wakala, wakaanza kukusanya mabaki...baada ya hapo Yesu hakupumzika, akaenda mlimani kuomba. Busy, busy, busy asubuhi mpaka usiku.
 
Enyi Wakristo, leo nimewafuata hukuhuku, najua mpo wengi kwenye jukwaa hili la Sports. Please, naomba kwa dakika moja tuzungumze jambo muhimu kuhusiana na soka.

Soka ni mchezo unaofurahisha na kuwaunganisha watu wengi duniani. Lakini, je, mmewahi kujiuliza kama Bwana wetu Yesu Kristo na mtume Paulo wangekuwepo katika mitaa yetu leo, wangetumia muda wao kila weekend kushabikia mpira?

Yesu alipokuwa duniani hakupoteza muda wake kwenye mambo yasiyo na faida ya milele; alijitoa kufundisha, kuponya na kuhubiri habari njema ya wokovu katika miji na vijiji (Mt 9:35). Hata usiku badala ya kupumzika, alienda mlimani kuomba (Luka 6:12). Mtume Paulo naye, alitangaza wazi kuwa maisha ya dunia hii ni kama kinyesi tu akiyalinganisha na thamani ya kumjua Kristo (Wafilipi 3:8).

Maandiko yanatuambia tuukomboe wakati kwakuwa nyakati hizi ni za uovu. Kwahiyo tutumie muda mwingi zaidi kushabikia mambo ya rohoni. Jiulize ndugu yangu: Je, nguvu unayoitumia kushangilia goli likifungwa, ndiyo nguvu hiyohiyo unayoitumia kushangilia mwenye dhambi mmoja akitubu na kumpokea Kristo? Muda unaoutumia kila Jumamosi na Jumapili kukaa mbele ya screen na kutazama mpira, ndio muda unaoutumia kutimiza agizo kuu la Yesu katika Mt 28:19-20?
Mambo ya mpira ungeachana nayo.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya mazoezi na ushabiki. Ukikaa mbele ya screen unaishabikia Man Utd unafanya mazoezi gani ya kutibu mwili?

Isitoshe Paulo anasema mazoezi ya mwili yanafaa KIDOGO.
1 Timotheo 4:8
Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
Asante kwa sababu umejaribu kukubaliana na hiii

Kwa kuwa michezo ni sehemu ya kufanya mazoezi ya mwili na mtume Paulo kazungumza hilo, Je, mazoezi ya kucheza mpira ni dhambi?

Kuwaangalia wanaofanya mazoezi kuna makosa kimaandiko?
 
Asante Iyerdoy kwa kuchangia mada.
Hiyo sura ya 6 ya Marko naomba tuisome tena pamoja kuanzia mstari wa 31 hadi wa 45 halafu uniambie ni mstari wa ngapi wanafunzi walipumzika:
31Akawaambia, Njooni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula. 32 Wakaenda zao faragha mashuani, mahali pasipokuwa na watu. 33Watu wakawaona wakienda zao, na wengi wakatambua, wakaenda huko mbio kwa miguu, toka miji yote, wakatangulia kufika. 34 Naye aliposhuka mashuani, akaona mkutano mkuu, akawahurumia; kwa sababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi. 35 Hata zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa; 36uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula. 37Akajibu, akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakamwambia, Je! Twende tukanunue mikate ya dinari mia mbili ili tuwape kula? 38Akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakasema, Mitano, na samaki wawili. 39Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabichi. 40Wakaketi safu safu, hapa mia hapa hamsini. 41 Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandalie; na wale samaki wawili akawagawia wote. 42Wakala wote wakashiba. 43 Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili; na vipande vya samaki pia. 44Na walioila ile mikate walikuwa wanaume elfu tano. 45 Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande mashuani, watangulie kwenda ng'ambo hata Bethsaida, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. 46Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba.

SOMA KWA MAKINI HAYO MANENO NILIYOYAWEKEA BOLD
Utaona wazi kuwa wanafunzi hawakupumzika.
Ni kweli Yesu aliwaambia wapumzike kidogo. Lakini hata hiyo kidogo hawakupumzika. Kule walikokuwa wanakwenda kupumzika, watu walitangulia kufika kwa miguu. Mkutano wa Injili ukaanza. Zikapita saa nyingi za mchana. Yesu akawaambia wawaketishe watu. Akawaambia wawagawie ile mikate. Wakala, wakaanza kukusanya mabaki...baada ya hapo Yesu hakupumzika, akaenda mlimani kuomba. Busy, busy, busy asubuhi mpaka usiku.
Mkuu; maisha ya mwanadamu yeyote(Akiwemo Yesu) haitokaa itokee kwamba mtu hapumziki (to relax) kwa mfano ukienda chooni kukata gogo uta-relax, ukiketi mezani kula chakula uta-relax n.k. Huwezi kujilazimisha kufanya kazi wakati unaumwa -ni lazima uta-relax. ukienda kusali, kuna kipindi uta-relax na kusikiliza Hotuba au Mafundisho(Homilia). Hayo yote Yesu aliyapitia kama mwanadamu wa kawaida sana na ndo mana Wayahudi walimkebehi kwa kusema: Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda? ...(Mathayo 13:55) Maana yake alikuwa ni mtu wa kawaida sana kwa mtazamo wa kimwili i.e. alizaliwa, alilelewa, alivikwa pampas na mama yake, alibeba tofali na mbao - kazi ya useremala), alikunya, aliugua, alikasirika, aligombezwa na wazazi (ref Luka 2:48), alinusurika kutekwa (Yohana 7:44), alilia ....... alikamatwa na kuwekwa lock-up na hatimaye umauti ulimkuta kama inavyokuwa kwa binadamu wote.
Itoshe tu kusema kwamba Mengi yamhusuyo Yesu hayakuwa na sababu ya kuandikwa kwani hayakuwa na umuhimu zaidi sana kwa ajili ya UKOMBOZI wetu mm na ww. Zingatia tu kwamba Yesu ni rafiki yako na unapoongea naye kiroho(Sala) ongea kama inavyokuwa unaongea na rafiki yako wa karibu (Mshikaji)na sio kwa makelele, maamrisho, kumtaka atende jambo fulani (unampiga vizinga Yesu) n.k. n.k. yani ww unaposali hebu fanya kana kwamba una-chat na Yesu na hiyo ndo sala iliyo bora zaidi.
Ni katika muktadha huo ndo mana nikasema Paulo na Yesu wangeliishi sawa na tunavyoishi leo na wangetumia Technolojia zilizopo.
 
Kumbe unamjua hadi Scholes insinekana ulikuwa na wewe mshabiki mkubwa
Ndio, nilipokuwa gizani nilikuwa shabiki sana. Lakini baada ya kuiona nuru ya Yesu, nikatambua kuwa imetupasa kuukomboa wakati kwakuwa nyakati hizi ni za uovu (Efe 5:16-17) Kukaa kwenye screen na kushabikia mpira, ni matumizi mabaya sana ya muda.
 
Enyi Wakristo, leo nimewafuata hukuhuku, najua mpo wengi kwenye jukwaa hili la Sports. Please, naomba kwa dakika moja tuzungumze jambo muhimu kuhusiana na soka.

Soka ni mchezo unaofurahisha na kuwaunganisha watu wengi duniani. Lakini, je, mmewahi kujiuliza kama Bwana wetu Yesu Kristo na mtume Paulo wangekuwepo katika mitaa yetu leo, wangetumia muda wao kila weekend kushabikia mpira?

Yesu alipokuwa duniani hakupoteza muda wake kwenye mambo yasiyo na faida ya milele; alijitoa kufundisha, kuponya na kuhubiri habari njema ya wokovu katika miji na vijiji (Mt 9:35). Hata usiku badala ya kupumzika, alienda mlimani kuomba (Luka 6:12). Mtume Paulo naye, alitangaza wazi kuwa maisha ya dunia hii ni kama kinyesi tu akiyalinganisha na thamani ya kumjua Kristo (Wafilipi 3:8).

Maandiko yanatuambia tuukomboe wakati kwakuwa nyakati hizi ni za uovu. Kwahiyo tutumie muda mwingi zaidi kushabikia mambo ya rohoni. Jiulize ndugu yangu: Je, nguvu unayoitumia kushangilia goli likifungwa, ndiyo nguvu hiyohiyo unayoitumia kushangilia mwenye dhambi mmoja akitubu na kumpokea Kristo? Muda unaoutumia kila Jumamosi na Jumapili kukaa mbele ya screen na kutazama mpira, ndio muda unaoutumia kutimiza agizo kuu la Yesu katika Mt 28:19-20?
Kama waliweza kushiri kwenye sherehe mbalimbali hadi kubadili maji kuwa divai why not mpira!
 
1 Yohana 2:15
[15]Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
Love not the world, neither the things that are in the world. If any man love the world, the love of the Father is not in him.
 
Mkuu; maisha ya mwanadamu yeyote(Akiwemo Yesu) haitokaa itokee kwamba mtu hapumziki (to relax) kwa mfano ukienda chooni kukata gogo uta-relax, ukiketi mezani kula chakula uta-relax n.k. Huwezi kujilazimisha kufanya kazi wakati unaumwa -ni lazima uta-relax. ukienda kusali, kuna kipindi uta-relax na kusikiliza Hotuba au Mafundisho(Homilia). Hayo yote Yesu aliyapitia kama mwanadamu wa kawaida sana na ndo mana Wayahudi walimkebehi kwa kusema: Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda? ...(Mathayo 13:55) Maana yake alikuwa ni mtu wa kawaida sana kwa mtazamo wa kimwili i.e. alizaliwa, alilelewa, alivikwa pampas na mama yake, alibeba tofali na mbao - kazi ya useremala), alikunya, aliugua, alikasirika, aligombezwa na wazazi (ref Luka 2:48), alinusurika kutekwa (Yohana 7:44), alilia ....... alikamatwa na kuwekwa lock-up na hatimaye umauti ulimkuta kama inavyokuwa kwa binadamu wote.
Itoshe tu kusema kwamba Mengi yamhusuyo Yesu hayakuwa na sababu ya kuandikwa kwani hayakuwa na umuhimu zaidi sana kwa ajili ya UKOMBOZI wetu mm na ww. Zingatia tu kwamba Yesu ni rafiki yako na unapoongea naye kiroho(Sala) ongea kama inavyokuwa unaongea na rafiki yako wa karibu (Mshikaji)na sio kwa makelele, maamrisho, kumtaka atende jambo fulani (unampiga vizinga Yesu) n.k. n.k. yani ww unaposali hebu fanya kana kwamba una-chat na Yesu na hiyo ndo sala iliyo bora zaidi.
Ni katika muktadha huo ndo mana nikasema Paulo na Yesu wangeliishi sawa na tunavyoishi leo na wangetumia Technolojia zilizopo.
Kupumzika na kurelax sio dhambi. Tatizo linakuja pale ambapo “kurelax” kunageuka kuwa kipaumbele kuliko mambo muhimu ya rohoni au tunapowekeza muda mwingi kupita kiasi kwenye mpira, na kusahau agizo kuu tulilopewa na Yesu(Mt 28:19-20).

Halafu kumbuka kwamba Mungu aliumba usiku ili uwe ndio muda wa kupumzika. Ukilala saa 12 jioni ukaamka saa 12 asubuhi hapo utakuwa bado tu huja-relax?

Sikiliza Paulo anavyosema katika 1 Wakorintho 6:12
“Vitu vyote ni halali kwangu lakini si vitu vyote vyenye faida. Vitu vyote ni halali kwangu lakini sitatawaliwa na kitu chochote.

Kuna watu ushabiki wa mpira umewatawala kiasi kwamba wako radhi wakose vipindi vya maombi kanisani kuliko kukosa kutazama mpira!

Hebu jiulize: je muda unaoutumia ku-relax kwa kushabikia mpira na muda unaoutumia kwa maombi, kusoma Neno na kuhubiri, ni sawa? Kama muda unaoutumia kila weekend kutazama mpira ni mwingi kuliko muda unaoutumia kufanya kazi ya Mungu, basi tambua kuwa hujajua kwanini upo duniani.

Umewahi kutafakari andiko hili:
Kol 3:17
"Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye."

Unapoanza kushabikia mpira huwa unaanza kwa maombi katika Jina la Yesu? Na je, timu yako ikifungwa, huwa unamshukuru Mungu katika Jina la Yesu? Kama sivyo, hiyo ni dalili kwamba ushabiki wa mpira ni jambo lisilo na thamani kiroho.
 
Umsema ukweli.
1. Kurelax kuliko pitiliza ni Uvivu. Na uvivu ni mama wa dhambi.
2.Paulo hapjuuamesema vizuri. Vitu vyote ni halali.. LAKINI si vyote vyenye faida. Hapo ni mhusika atumie akili yake kupambanua na kufanya maamuzi anataka kipi?
3. Hapo kwenye mpira ni kweli hata mm nawashangaa sana mashabiki wa mpira. Mtu analipia kuangalia mpira lakini nyumbani hali ya familia ni tete, miradi, biashara au mipango yake haijasimamiwa ipasavyo-inadorora yy anaona ni sawa tu na wala hashtuki. Inasikitisha zaidi wakati akitenda hayo yote anasahau Yupo aliyemwumba na anampenda ila yeye (Shabiki) amemtelekeza ila siku akipata changamoto esp.tatizo la kuugua au ajali utamsikia " Ee Mungu wangu.............." ndipo anamkumbuka muumba wake.
 
Back
Top Bottom