Kama waliweza kushiri kwenye sherehe mbalimbali hadi kubadili maji kuwa divai why not mpira!
Sherehe alizohudhuria Yesu zilikuwa na msingi wa kiroho, sio burudani. Kwa mfano, Sikukuu ya Pasaka, Vibanda na Hanukkah zilikuwa sherehe zilizoamriwa na Mungu/zilihusiana na historia ya wokovu wa Israeli.
Yesu alienda katika sherehe hizo ili kufundisha, kufunua ukweli na kuonyesha kwamba Yeye ndiye utimilifu wa sherehe hizo.
Yesu hakuwahi kushiriki katika starehe au burudani zisizo na faida ya kiroho. Hakuna mahali tunaona Yesu akipoteza muda wake kwenye michezo, maigizo au starehe za kidunia.
Wakati wake wote ulimwenguni aliutumia kuhubiri, kufundisha, kuponya na kufanya kazi ya Baba aliyemtuma (Yohana 9:4).
Kusudi la Yesu duniani lilikuwa kuleta wokovu, sio kujiburudisha. Yeye mwenyewe alisema:
“Chakula changu ni kufanya mapenzi yake aliyenituma, na kuitimiza kazi yake” (Yohana 4:34).
Hata kwenye arusi ya Kana, hakwenda kushiriki shangwe ya kidunia, bali alitumia tukio lile kufanya ishara yake ya kwanza, ili wanafunzi wake waamini.
Mpira na michezo ya kisasa havina uhusiano na utume wa kiroho.
Sherehe za Wayahudi zilikuwa na maana ya kumkumbuka Mungu na kazi zake, lakini mpira ni burudani ya kibinadamu isiyo na uhusiano na ibada.