Je Zanzibar Inahitaji Truth & Reconciliation Comm。Kuponya Makovu ya Mapinduzi, ili Upinzani Ukishinda,Upewe?。Sis & Bro,Can You Please Do The Needfu?。

Kwa attitude za Wanzanzibar wengi kuhusu watanganyika, sishauri serikali ifanye maridhiano hivi karibuni.

Upinzani ukishika Zanzibar Hapana Shaka Muungano utavunjika
 
Mkuu Pascal
Mimi naona kitu cha kufutwa ni msamiati wa mapinduzi, mfano leo hii kuita serikali ya mapinduzi Zanzibar si sawa. SUK imejumuisha CCM na ACT, na walienda kwenye sanduku la kura, right? Sasa kuna justification gani kuiita serikali ya mapinduzi? CCM na ACT wamempindua nani na lini?

Hili neno linatumiwa na wahafidhina walioko CCM ambao hawako tayari kwa uchaguzi huru na haki Zanzibar. Wanajua waliingia madarakani kwa kupindua na kwenye uchaguzi huru hawawezi shinda. Nakubaliana nawe bila reconciliation hakuna amani ya kweli Zanzibar, maana hata huu uchaguzi ujao uwezekano wa ACT kushinda ni mkubwa ila kama enzi za Jecha watatangazwa CCM. Hii itakuwa hadi lini?

Naunga mkono hoja
 
Hapa tofauti ni nini?
 
Naunga mkono hoja.....

Zanzibar wanahitaji mno tume ya ukweli na maridhiano hasa kuhusu kilichotokea 12/1/ 1964.
 
Hapa tofauti ni nini?
Tofauti ni kwamba Sultan alirejeshewa na Waingereza control ya Zanzibar na kuifanya kuwa constitutional monarchy. Kumbuka, baada ya Oman Arab Rule na Zanzibar kuwa British Protectorate, Sultan hakufungasha virago vyake. Aliendelea kutumiwa na Waingereza kama colonial administrator hadi aliporejeshewa control. Sultan hakuwa Mzanzibar. Alikuwa mkoloni. Period!
 
Kwa hiyo ilipinduliwa serikali ya mkoloni wa uingereza?
 
Paskali haoni kama Sultan alikuwa mkoloni.
Siyo kwa sababu kwa muda ambao Sultani na jamii yake walikaa Zanzibar walichanganyika na watu wa asili ya Zanzibar ndio maana kwa hoja ya Pascal kuwa reconciliation ni muhimu kwani kuna wazanzibari wengi ambao huwezi kuwanyang'anya uzanzibari wao lakini wana asili ya alikotoka Sultani. Mfano uchaguzi wa 2015 matokeo yake, je unaona ufumbuzi wake ni nini? Waendelee kumtumia Jecha?
 
Sultan alikuwa mtawala wa kiarabu mwenye hadhi ya kifalme; hakuna Mzanzibar (hata mwenye asili ya kiarabu) aliyekuwa na authority ya kumuweka au kumuondoa Sultan madarakani.

So, ukimng’oa dictator wa kikoloni, kuna sababu gani ya kufanya reconciliation?
 
Kumbuka kwenye Moja ya vitu tunavyo jihusia sisi Watanzania Kwa ujumla wetu na kumbumbusha mtu anae elekea njia isiyo sahihi: nikwamba
Vita sio kitu kizuri
Mshindi na mshidwa lazima watapoteza vijana wao
Mifano mingi tumeiishi
"Mlengwa mkuu WA vita ni mtu"
Taifa limeamua kusherehekea ushindi japo damu ilitumwagika
tunao mashujaa wakuwaenzi
 
Kwa nini Jecha alihusika kufuta uchaguzi baada ya CUF kushinda? Wakoloni walikuja kupiga kura kuwakataa wanamapinduzi?
 
Kwa nini Jecha alihusika kufuta uchaguzi baada ya CUF kushinda? Wakoloni walikuja kupiga kura kuwakataa wanamapinduzi?
Hata bara hilo linaweza kutokea. In fact, zipo sehemu nyingi wapinzani wamewahi kuenguliwa kwa technicalities ambazo hazina mashiko!
 
Hata bara hilo linaweza kutokea. In fact, zipo sehemu nyingi wapinzani wamewahi kuenguliwa kwa technicalities ambazo hazina mashiko!
Swala siyo kuenguliwa, majority ya wapiga kura wanaokipigia kura ACT, CUF na kabla ya hapo umma party wana asili moja na inajulikana, mostly wapemba na wenye asili ya kiarabu. Au utawanyang'anya uzanzibari wao?
 
Kaka Paskali,
Ninachokishangaa sana kwenye reconciliation za hapa kwetu TZ;
Mkuu Ngali, Ngalikihinja, kwanza asante kutembelea uzi huu, maswali yako ni maswali ya msingi sana.
1. Hakusemwagwi watu wanatakiwa au wana-reconcile kwenye nini
Ni kweli hili halisemwi, kwenye yale Mapinduzi na baada ya Mapinduzi, kuna damu zilimwagika, wenye fursa na uwezo walikimbia Zanzibar akiwemo Sultan na familia yake ya watu 46. Wasio na uwezo walibaki Zanzibar na mpaka leo wanaishi na makovu ya mapinduzi!.

Kuna mambo mabaya maovu yalitokea baada ya mapinduzi miongoni mwake ni yale yaliyosababisha kifo cha Karume, yasemwe wazi watu wa vent, yaishe!.
2. Hakusemwagwi nani na nani wanatakiwa wali-reconcile
Waliopindua wa reconcile na waliopinduliwa!.
3. Hukusemwagwi wamekoseana nini hao wanaotakiwa ku-reconcile
Kwenye truth and reconciliation, maovu yaliyofanywa na mapinduzi yanatajwa, waliopindua wanasema lengo lilikuwa kupindua na sii kumwaga damu, wanaomba msamaha kwa damu zilizomwagika, wanawafuta jasho wana mapinduzi walio sahaulika, wanawafuta machozi walio lia. Wanasoma kisomo cha wote, they bury the hatchet and start afresh.
Reconciliation zetu zipo very blind..!!
Its true, kwasababu Kiafrika hatuna utamaduni wa ku reconcile, mimi mwenyewe yalinikuta.

Nilioa nikiwa young at 25 wife 21, classmate TSJ, from college straight altareni!.

Mwenzangu akapata scholaship ya 4 years US, nikamsindikiza, we have our two kids ni US subjects, mimi nikarejea Bongo, si unajua tena Usukuma, Uafrika, Uswahili, si nika jiachia!.
Niliporudi US nikawa mkweli kwa wife!, kumbe kuwa mkweli sana kosa!. Wife mpaka leo kagomea US, hivyo mimi ikanibidi kuendeleza Usukuma na Auafrika, ila kukitokea zile ajali za magoli ya mipira ya kona na mechi za ugenini, unakomaa na kukausha kau kau.

Huyu mtu ndie mgombea urais wa Zanzibar 2025 kupitia ACT, angalia hapa nilisema nini kuhusu mtu huyu. Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Kisha angalia hapa nilishauri nini Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu

Msikize anasema nini kuhusu muungano Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?
P
 
Swala siyo kuenguliwa, majority ya wapiga kura wanaokipigia kura ACT, CUF na kabla ya hapo umma party wana asili moja na inajulikana, mostly wapemba na wenye asili ya kiarabu. Au utawanyang'anya uzanzibari wao?
Hawapokwi ushindi kwa sababu wana asili ya kiarabu bali ni kwa sababu wao ni wapinzani. Hata bara CCM ikishindwa uchaguzi, itafanya yale yale inayofanya Zanzibar. Kwa mtazamo wangu, solution ya issue ya Zanzibar sio kufanya reconciliation ya mapinduzi bali ni kufuata sheria za uchaguzi. Chaguzi lazima ziwe free and fair.
 
Teh teh teh 😃 😃 😃 kwa hiyo na wewe unahitaji 'reconciliation' Ili mkeo arejee kwako ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…