Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

Omar,

Acha jaziba na kashfa kwa wanachama wa jamvi hili. Kuna watu makini na wengi wamekuwa wanampa Zitto nafasi ili aeleze kilichomtokea kwenye kamati hizo au kwenye issue ya Dowans.

Huwezi kulazimisha watu kukubaliana nawe. Ukiwa na mpango wa kuwa mwanasiasa, inabidi ujenge ngozi yako ili iwe ngumu kiasi cha kuhimili hoja za watu (wakiwemo wana JF).

Yaani udaku, majungu na cheap spins zimegeuka kuwa hoja. Sidhani kama JF imeishiwa namna hiyo. Hujiulizi kwa nini ninapojadiliana na wengine natumia lugha tofauti na ninadeal na wewe...

Kama unazoendeleza hapa unaona hoja inabidi uelimike zaidi kabla ya kuanza kujitutumua katika ukumbi huu....Samahani nilidhani unajua unachokifanya hapa kuwa ni spining game kumbe unadhani ni kutoa hoja?

omarilyas
 
Vyama vya siasa ni kama ulaji tu Tanzania bado hatujapata chama au wanasiasa wa kuipeleka nchi pale inapotakiwa kuwa.Wengi wamejaa undugu,ukabila au mkondo wa kifisadi na wale ambao kidogo wanakemea mafisadi huenda tu kwavile mvua hazikuwanyeshea au maji hayakuwa kwenye mkondo wake.
 
Duh...kumbe Zitto ndani ya Chadema yupo na Mama yake pia.
MAMA ZIto ni mwanachama wa kawaida,ungeshangaa MTEI na mkwe wake-MBOWE.

NDESAMBURO na Mtoto wake Lucy wote wabunge kupitia chadema.

KOMU mkurugenzi wa chadema na mke wake amepewa ubunge bila kupigiwa kura-Anna Komu. kama alivyopewa Mtoto wa Ndesamburo na wengine.
 
Shughuli ipo,siasa ina mambo mengi!..Wiki hii naona Zito na Mama zito wamepamba media du!..
 
Hapo kwa ufupi CHADEMA wamechemsha! Hata mkiwatetea vipi...inaelekea uongozi wa juu wa hiki chama ni kwa ajili ya watu fulani ndo maana wanarithishana kama usultani. Hii haina tofauti na enzi ya chama kimoja ambapo mgombea alikuwa mmoja kisha fedha kibao zinatumika kwa kinachoitwa "uchaguzi". Kwa mwendo huu CHADEMA haiwezi kushutumu vyama vingine kuwa havizingatii demokrasia. Yaliyotokea CHADEMA si kukuza bali ni kudidimiza demokrasia. Kwa Tanzania bara bado hakuna chama makini cha upinzani...vyote ni ubabaishaji.
 
Mkuu Omar,
kweli mkandara. Inawezekana vyama hivi vinashindwa kutengeneza na kuzisimamia sera zinazoendana na mirengo yao lakini wanayo. CUF wao ni waliberali ingawa ni mabingwa wa siasa za chuki na kukosa uvumilivu. Chadema walikuwa mabwanyeye na sasa wamepunguza makali na kuwa mabepari ingawa ukiangalia sera na misimamo na kauli mbiu zao zimejaa fikira za kijamaa. CCM wao ni wajamaa ingawa sera zao ni za kibepari.
sasa mkuu wangu hapa umesema kitu gani?..yaani madai ya maandishi ktk katiba yasiyofuatwa unayaita ndio mrengo! yaani unataka kunambia Muislaam anaweza kuwa akisali kanisani lakini bado ni Muislaam!..

Anyway, kusema kweli siwezi kuweka ubishi ktk mambo ambayo siyafahamu kwa uhakika isipokuwa nachukulia mawazo ya mtu na mtazamo wake ktk maswala tofauti. Ila tu nitasema kwamba sii CCM, CUF wala Chadema wana mrengo zaidi ya kuvuta sera zozote zionazoweza kuwapa kura..Leo hii siwezi kabisa kusema CCM ni Mabepari au Wajamaa, kwani mabepari siku zote huhifadhi na kulinda mali, tamaduni, Uzawa, serikali ndogo (matumizi madogo), lower taxes kuwa ilani tangulizi za msimamo wao tofauti na kushoto. Na utakuta vyama vyote Tanzania vinaweza kuwa ma majibu sawa ktk maswala yote muhimu yanayojenga mrengo..

Kwa mfano, ukiuliza mwanachama wa CCM, CUF au Chadema kuhusu kutoa mimba majibu utapata tofauti ndani ya chama na yakifanana pande zote, dini utaambiwa nchi haina dini lakini wananchi wake wanaruhusiwa ku express their beliefs hata kama they offend others..wanasema maslahi ya nchi mbele!

Hakuna kitu separation of churches or Mosques and the Government. Hakuna walfare, Education na health care ni privilege or Right kwa wananchi, it all depends na mtu unayemuuliza..
Hivyo huwezi kunambia ati Tanzania tuna Mirengo huu ni uzuhshi mtupu na ndio maana watu wengi wanafikiria kuwa Conservative ni Ubepari na Liberal/Progressive ni Ujamaa ule wa Kikomunist. kifupi nchi yetu ni nchi isofungamana na imani yoyote ya dini wala mrengo ila watu wake pekee.

Kitu kingine umezungumza mengi kuhusu Zitto ambayo nashindwa hata kukuelewa, kwamba yeye sii Conservative ila ni mtu wa kushoto wakati huo huo nukuu ya maelezo yako imejieleza vizuri kuwa mtizamo wako ni kuwa ubepari wala ubwanyenye hauwezi kuwa conservatism. Consevatism kwa Tanzania imejikita katika misingi ya ujamaa na kujitegema kwani hiyo ndiyo iliyounda nchi na jamii ya Tanzania. Hivyo unajigonga mwenyewe ktk kuchanganya mtazamo mzima wa mrengo huu kwa kuchukua ya Ulaya kuwakana watu hawa, hapo hapo unatambua kuwa conservatives wa Ulaya hawawezi kuwa sawa na wa Tanzania kutokana na historia ya nchi yetu. mimi nitaongezea pia Watu na Mazingira ni sababu kubwa sana.


Hata hivyo mkuu nimekusoma na nitashukuru sana kama utanipatia hayo mafanikio ya ndugu yetu Zitto toka ameingia kamati ya madini kwa sababu nachoelewa mimi sheria mbado hazijabadilika Barricks bado wanavuta kama jana hiyo miradi mipya sidhani kama inahusiana na dhahabu labda madini madogo madogo ambayo hayana faida.
 
Last edited:
mengine yote yawezekana kuwa una hoja,...................ila hiyo ya mwisho hapo....mkuu umepotea.......

Hilo la mwisho limeonyesha ni kwa jinsi gani umeishiwa hoja, na una ufinyu mkubwa wa fikra.
 
KOMU mkurugenzi wa chadema na mke wake amepewa ubunge bila kupigiwa kura-Anna Komu. kama alivyopewa Mtoto wa Ndesamburo na wengine.

Acha uzandiki....

Anna Maulida Komu ni mngazija wa Zanzibar aliyeolewa Moshi....Hana mahusiano yoyote na Komu mkurugenzi wa fedha CHADEMA.

Ama kuolewa kunabadili kabila siku hizi. Inaelekea kuna wengi wanaolalamika uchaga humu ambao hawana tofauti na MASIHA FEKI wetu wanaojiita wapambanaji wa ufisadi. Wote ni mafisadi, wakabila na wadini sema tu hapa wanaona wamezidiwa kete na ukabila wa wenzao. Subirini UR TURN TO EAT...

Acheni kujidai mnapambana na ukabila kwa kutumia chuki za ukabila......

Yaleyale ya kikundi cha Mashehe wa Shura ya Maimamu wanavyopambana na "udini wa wakatoliki" kwa kumobilize "udini wa waislamu"....Angalao Kakobe ameamua kushindana na wadini wenzake kwa kutumia misingi ya UTANZANIA...

omarilyas

omarilyas
 
KOMU mkurugenzi wa chadema na mke wake amepewa ubunge bila kupigiwa kura-Anna Komu. kama alivyopewa Mtoto wa Ndesamburo na wengine.

Acha uzandiki....

Anna Maulida Komu ni mngazija wa Zanzibar aliyeolewa Moshi....Hana mahusiano yoyote na Komu mkurugenzi wa fedha CHADEMA.

Ama kuolewa kunabadili kabila siku hizi. Inaelekea kuna wengi wanaolalamika uchaga humu ambao hawana tofauti na MASIHA FEKI wetu wanaojiita wapambanaji wa ufisadi. Wote ni mafisadi, wakabila na wadini sema tu hapa wanaona wamezidiwa kete na ukabila wa wenzao. Subirini UR TURN TO EAT...Wenzenu MTANDAO walisubiri THEIR TURN wakaja na RICHMOND etc kwa ARI na KASI MPYA..

Acheni kujidai mnapambana na ukabila kwa kutumia chuki za ukabila......

Yaleyale ya kikundi cha Mashehe wa Shura ya Maimamu wanavyopambana na "udini wa wakatoliki" kwa kumobilize "udini wa waislamu"....Angalao Kakobe ameamua kushindana na wadini wenzake kwa kutumia misingi ya UTANZANIA...

omarilyas

omarilyas
 
..mkubwa wao alitoa maagizo juzi akiwa lindi akizindua barabara inayolipiwa mkopo wake kwa kodi zetu wote ...aliwaambia """ sasa barabara hiyo msimuuzie mtu yeyeto ardhi..."....nikajiuliza kama ni barabara imeanza kujengwa tangu enzi ya nyerere,mwinyi,mkapa,na sasa wanaendelea ...sikupata kumsikia mkapa mfano pamoja na kutokea huko pwani ya mtwara na kujenga sehemu kubwa ya barabara akiwaagiza wakazi wasikaribishe watanzania wenzao....ujinga kabisa..kukaribisha wasomali sawa ..lakini watanzania wenzenu tatizo....

juzi waziri mmoja akiwa bagamoyo ...akawaambia kuwa wanapeleka pale bandari ;;;na EPZ na akawataka watu pale wasimkaribishe mtu kufaidi hayo matunda.....kwa kuuza ardhi...,sasa tunaenda wapi????...hiyo EPZ na BANDARI si inajengwa kwa kodi za wote...kwa nini wazuie watanzania wenye nia ya kutega uchumi pale wasichukue fursa kwa usawa....???.... afteral bandari hiyo na epz hazikuwa na sababu badala yake wangejenga EPZ mtwara au tanga...waunganishe na uganda kwa tanga na malawi na zambia kwa mtwara...hakuna sababu ya kujenga bandari mpya bagamoyo just 30km away the dar es salaam port....
mkuu wale ilibidi kuwastua walikuwa wanauza ardhi yao kijinga kabisa! To be fair ni vyema kuwajulisha ardhi ni mali na wasiuze hovyo wasije kuishia kuwa manamba hukohuko kwao.
Respect
 
MAMA ZIto ni mwanachama wa kawaida,ungeshangaa MTEI na mkwe wake-MBOWE.

NDESAMBURO na Mtoto wake Lucy wote wabunge kupitia chadema.

KOMU mkurugenzi wa chadema na mke wake amepewa ubunge bila kupigiwa kura-Anna Komu. kama alivyopewa Mtoto wa Ndesamburo na wengine.

Hebu tusaidie na analysis ya vyama vingine ili tuone nani zaidi... kama sikosei kuna sehemu hapa tz hata urais wameukwaa baba na mwana, uwaziri n.k

its about quality and not undungu ndiyo inamatter zaidi
 
Mpayukaji kama mwanaye!!! Nyoka ni lazima atotoe nyoka mwenzake!!! Basi akiwa mama Mke huyo, kazi ipo na huyo mwanaye!! Au ndiyo maana ndoa na yule.... mhhhh bado??? Chiriku mno huyu!!

Asante Dr. Slaa kwa kumjibu kwa busara.
 
Mpayukaji kama mwanaye!!! Nyoka ni lazima atotoe nyoka mwenzake!!! Basi akiwa mama Mke huyo, kazi ipo na huyo mwanaye!! Au ndiyo maana ndoa na yule.... mhhhh bado??? Chiriku mno huyu!!

Asante Dr. Slaa kwa kumjibu kwa busara.

.....Maane, Niagize mtoto aniletee Popcorn?? 🙂
 
.....Maane, Niagize mtoto aniletee Popcorn?? 🙂
Zitto akiwa RAISI BASI MAMA YAKE ATAPEWA U BALALI (GAVANA WA BOT) ULAJI UNAENDELEA PALE PALE KAMA CHI CHI EM. MAISHA HAYA NI KUFANYA KAZI SIASA POROJO TUPU
 
Acha uzandiki....

Anna Maulida Komu ni mngazija wa Zanzibar aliyeolewa Moshi....Hana mahusiano yoyote na Komu mkurugenzi wa fedha CHADEMA.

Ama kuolewa kunabadili kabila siku hizi. Inaelekea kuna wengi wanaolalamika uchaga humu ambao hawana tofauti na MASIHA FEKI wetu wanaojiita wapambanaji wa ufisadi. Wote ni mafisadi, wakabila na wadini sema tu hapa wanaona wamezidiwa kete na ukabila wa wenzao. Subirini UR TURN TO EAT...Wenzenu MTANDAO walisubiri THEIR TURN wakaja na RICHMOND etc kwa ARI na KASI MPYA..

Acheni kujidai mnapambana na ukabila kwa kutumia chuki za ukabila......

Yaleyale ya kikundi cha Mashehe wa Shura ya Maimamu wanavyopambana na "udini wa wakatoliki" kwa kumobilize "udini wa waislamu"....Angalao Kakobe ameamua kushindana na wadini wenzake kwa kutumia misingi ya UTANZANIA...

omarilyas

omarilyas

Nashukuru wewe Kibanda alishakupa habari zako kuwa Chadema haikuhusu hata ukijipendekeza kwa mtindo wa kuuma na kupuliza ambao ndio unafiki.unauma humu JF halafu unampigia simu KIBANDA.

ANNA KOMMU hakupigiwa kura na taasisi au jumuiya yeyote ya Chadema kwa taarifa yako 2005 Chadema hawakuwa na baraza la wanawake.majina yaliteuliwa na kundi la wenye chama.wewe na Chacha Wangwe nani anaijua Chadema na mwenye uchungu na Chadema?

Chacha WANGWE alikwishaliweka wazi hili la uchagga wa kina KOMMU. nakuuliza kuna Mngazija anaitwa KOMMU ANNA? kukusaidia sikiliza au fuatilia mahojiano ya Chacha Wanngwe na Mwanakijiji upate habari kamili.nashukuru wenye Chadema wamekushtukia hata ukijipendekeza.
 
..sijui hayo ya "FIRST LADY ".... kama ni kichwa sahihi.....

..........Taratibu tu tutafika.Kumbukeni kuwa kuna upo uwekezaji hata katika SIASA, tushishangae siku hizi ndivyo mambo yalivyo natumaini tutafika tu kama asemavyo mwandishi moja,

..Familia pia inaweza ikawekeza katika siasa, watoto wakubwa wengi na Wabungwe wengine wemepata Uraisi na bado kuna ambao wnategemea kupata Uraisi kurithi viti vya Baba zao kama vile.............

..Na mtoto na mama nao wanahaki yao....
 
Zito kweli amepoteza focus,mwanzo focus yake ilikuwa kwenye matatizo ya wananchi lakini mabadiliko yalianza baada kuchaguliwa kwenye tume ya madini..whether kama ni m/kiti wa chadema au sio issue ni kwamba at heart bado anawawazia wanyonge..wanyonge walimtambua kuwa mtetezi wao..lakini sasa mambo ya madaraka yamemside track(kupoteza dira)..akirudi kwenye njia wanyonge amban ndio wengi watamjua mtetezi wao...akiendeleza sera za madaraka na kugombania madaraka atakuwa hana tofauti na viongozi waliopo kwenye government yetu kwa sasa....amenidisappoint sana..hana tofauti na wale..
 
wakuu,huyu mama anatafuta umaarufu tu kupitia mwanae.tumsamehe tu manake hajui hata alichokiongea.asante Mheshimiwa Dr Slaa kwa jibu ulilompa.
 
Erick Ongara,thanx for your post.umefafanua kwa undani hali halisi na natumaini kila mwana JF ambaye anaakili timamu za kufkiria jambo kwa undani atakuwa amekupata.kuna watu hapa ambao wataoa mawazo yao wakilalia zaidi kwenye ushabiki wa mtu mmoja mmoja.mfano kuna watu ambao wanamshabikia zito as a person na sio zito kama CHADEMA.zito kama zito is nothing,he is who he is now kwasababu ya CHADEMA.Mambo yote ambayo amefanya na kumletea umaarufu aliyafanya kichama,i mean CHADEMA walikaa kama chama,wakapanga mikakati then wakagawanya majukumu na vitu vya kuongea public na bungeni kwa wabunge wao(this include slaa,zito,the late chacha wangwe,na wengineo).kwahiyo wakuu lazima muelewe wazi kwamba issue zote ambazo zito alikuwa akizitoa bungeni zilitoka kwenye chama chake na yeye alipewa aziwakilishe bungeni.
Sasa huyu kijana mwenzetu nadhani umaarufu umemlewesha kiasi cha kujisahau kabisa na kumfanya ajione kwamba yeye ni bora kuliko wakubwa zake ambao ndio waliomfikisha hapo alipo leo.Nakubali kuwa Chadema bado ni chama kichanga ambacho kinahitaji muda zaidi kukua na kujiimarisha.Zito ajitahidi kukiimarisha chama na ana nafasi kubwa sana ya kuongoza CHADEMA hata nchi hapo baadae.lakini kama ataanza mapema hii kujidai mjuaji zaidi na kulewa umaarufu ni dhahiri kuwa hatafika mbali kisiasa.atajiua mwenyewe kisiasa na pia kukiuwa chama chake. lazima ajifunze kuheshimu wakubwa zake kama kina mbowe,slaa na wengineo hata pale ambapo hakubaliani nao kimawazo.Naamini kabisa lazima kuna mapungufu ambayo hujitokeza ndani ya CHADEMA kwenye uongozi lakini ni mambo ya kawaidakabisa ambayo hutokea kila mahali.Zito lazima aache ubinafsi na afanye mambo kwa manufaa ya watanzania wote wenye mapenzi na CHADEMA.kwa yeye kama naibu katibu mkuu kuanika mambo ya ndani ya chama sio kwamba ana saidia kukijenga chama bali anakibomoa na anajibomoa mwenyewe kisiasa.
 
Hivi huyu Zitto alivyoenda nje na kuanza kuropoka mambo ya ndani ya chama baada ya kutokubaliana na wenzake maana yake nini,huyu ni fisadi tuu na hana uchungu wowote njaa tupu...kwanini ana magari Landcruisers kama tatu? kapata wapi pesa huyu?
 
Back
Top Bottom