Mkuu Omar,
kweli mkandara. Inawezekana vyama hivi vinashindwa kutengeneza na kuzisimamia sera zinazoendana na mirengo yao lakini wanayo. CUF wao ni waliberali ingawa ni mabingwa wa siasa za chuki na kukosa uvumilivu. Chadema walikuwa mabwanyeye na sasa wamepunguza makali na kuwa mabepari ingawa ukiangalia sera na misimamo na kauli mbiu zao zimejaa fikira za kijamaa. CCM wao ni wajamaa ingawa sera zao ni za kibepari.
sasa mkuu wangu hapa umesema kitu gani?..yaani madai ya maandishi ktk katiba yasiyofuatwa unayaita ndio mrengo! yaani unataka kunambia Muislaam anaweza kuwa akisali kanisani lakini bado ni Muislaam!..
Anyway, kusema kweli siwezi kuweka ubishi ktk mambo ambayo siyafahamu kwa uhakika isipokuwa nachukulia mawazo ya mtu na mtazamo wake ktk maswala tofauti. Ila tu nitasema kwamba sii CCM, CUF wala Chadema wana mrengo zaidi ya kuvuta sera zozote zionazoweza kuwapa kura..Leo hii siwezi kabisa kusema CCM ni Mabepari au Wajamaa, kwani mabepari siku zote huhifadhi na kulinda mali, tamaduni, Uzawa, serikali ndogo (matumizi madogo), lower taxes kuwa ilani tangulizi za msimamo wao tofauti na kushoto. Na utakuta vyama vyote Tanzania vinaweza kuwa ma majibu sawa ktk maswala yote muhimu yanayojenga mrengo..
Kwa mfano, ukiuliza mwanachama wa CCM, CUF au Chadema kuhusu kutoa mimba majibu utapata tofauti ndani ya chama na yakifanana pande zote, dini utaambiwa nchi haina dini lakini wananchi wake wanaruhusiwa ku express their beliefs hata kama they offend others..wanasema maslahi ya nchi mbele!
Hakuna kitu separation of churches or Mosques and the Government. Hakuna walfare, Education na health care ni privilege or Right kwa wananchi, it all depends na mtu unayemuuliza..
Hivyo huwezi kunambia ati Tanzania tuna Mirengo huu ni uzuhshi mtupu na ndio maana watu wengi wanafikiria kuwa Conservative ni Ubepari na Liberal/Progressive ni Ujamaa ule wa Kikomunist. kifupi nchi yetu ni nchi isofungamana na imani yoyote ya dini wala mrengo ila watu wake pekee.
Kitu kingine umezungumza mengi kuhusu Zitto ambayo nashindwa hata kukuelewa, kwamba yeye sii Conservative ila ni mtu wa kushoto wakati huo huo nukuu ya maelezo yako imejieleza vizuri kuwa mtizamo wako ni kuwa ubepari wala ubwanyenye hauwezi kuwa conservatism.
Consevatism kwa Tanzania imejikita katika misingi ya ujamaa na kujitegema kwani hiyo ndiyo iliyounda nchi na jamii ya Tanzania. Hivyo unajigonga mwenyewe ktk kuchanganya mtazamo mzima wa mrengo huu kwa kuchukua ya Ulaya kuwakana watu hawa, hapo hapo unatambua kuwa conservatives wa Ulaya hawawezi kuwa sawa na wa Tanzania kutokana na historia ya nchi yetu. mimi nitaongezea pia Watu na Mazingira ni sababu kubwa sana.
Hata hivyo mkuu nimekusoma na nitashukuru sana kama utanipatia hayo mafanikio ya ndugu yetu Zitto toka ameingia kamati ya madini kwa sababu nachoelewa mimi sheria mbado hazijabadilika Barricks bado wanavuta kama jana hiyo miradi mipya sidhani kama inahusiana na dhahabu labda madini madogo madogo ambayo hayana faida.