Je, Zitto Kabwe alijisahau na kuanza kuung'ata mkono unaomlisha?

Je, Zitto Kabwe alijisahau na kuanza kuung'ata mkono unaomlisha?

Uchaguzi huu wizi bila akil ndio maana walikataa kuwapa nakala ya matokeo mawakala.chaguzi za nyuma ukiwa na mawakala makini, waadilifu,wazalendo na wapenda demokrasia unapata matokeo yenye unafuu na nakala yako unapata
Yaani kwa sasa mnauweka wizi katika makundi!

Kwa hiyo ule mwingine haukuwa wizi kwa sababu ulifanyika kwa akili!

Kwanza nadhani hujaelewa msingi wa hoja yangu!
 
Zitto kilichombeba miaka hiyo kuanzia 2005 ni urafiki wake na JK, na hicho ndicho kilichosababisha Chadema waanze kumtilia shaka, akafika mbali na kusema JK ni kama baba yake wa pili alipoona kelele zinazidi kuelekezwa kwake.

Hivyo kwa mtazamo wangu usichanganye kati ya urafiki wa JK na Zitto ukadhani ndio CCM wote wenye mtazamo huo, ndio maana Magufuli sasa hivi hana habari na Zitto, mpaka wakamnyan'ganya ushindi Kigoma Mjini kwa lazima, japo nasikia atapewa Ubunge wa kuteuliwa hivi karibuni, hii ni kama ahsante ya CCM kwake kwa kukubali kujiunga SUK kule Zanzibar.

Hapa ndio pangependeza mada yako iegemee zaidi, kwasababu naamini kama Zitto angekuwa na uhusiano na CCM wa moja kwa moja TISS wangemwambia Magufuli asimshughulikie Zitto kwenye ule uchaguzi mkuu uliopita kwa kuwa ni mwenzao, lakini haikuwa hivyo; ila kubwa zaidi, Zitto ni opportunist sana, hiyo ndio tabia yake kubwa, anapenda sana kurukia fursa za kisiasa, ndio maana kakimbilia SUK.
 
Hakuna kitu cha hovyo na kibaya kama kusoma bandiko la lefu la hovyo, propaganda na la kipumbavu halafu asubuhi asubuhi.

Halafu unakuta hili jamaa ni zee lenye mke na watoto.
Kwani umelazimishwa kufungua na kusoma!

Kinachoshangaza zaidi umepata mpaka muda wa kutoa maoni kwenye bandiko lefu la hovyo, propaganda na kipumbavu! Sasa hapa nani ni mpumbavu zaidi!
 
Hakuna sifa yoyote ya maana kwa ccm..

Yoyote yule aliye timamu, anaiona ccm kama kusanyiko la wapumbavu..

Umaarufu wenu ccm kwa sasa dunia nzima inawafahamu kama majambazi ya kura kwenye chaguzi.
Huu ni mtazamo wako ukiwa ndani ya boksi lako la fikra ambalo halina uhalisia!
 
No. Tatizo lenu Mr Mzungu aliwapatieni matarajio makubwa ambayo hata yeye asingeweza kutimiza. "Tutashinda uchaguzi huu kwa Tume hiihii!" ~ Mr Mzungu
Tume hiihii,Kama ingekuwa huru kwa kiwango Cha miaka iliyopita matokeo yangekuwa tofauti sana.nazingatia kwa aliyojili huku kwetu kusini mwa tz.
 
Bila kuiba kura hakuna CCM iliyoko madarakani.
Kwa hiyo badala ya kuisifu CCM iangaze kwa ukweli wake hakisi kuwa iko haoo ilipo kwa uporaji wa maamuzi ya wananchi!
 
Mleta mada, CCM sio chama cha siasa, uchaguzi (uchafuzi) wa mwaka huu wapinzani walipambana na Tiss, polisi, jeshi, wakurugenzi, wakuu wa wilaya/mikoa

Ccm kama ccm kwenye uwanja huru ni wepesi kama karatasi
 
Watanzania ,watanganyika na wazanzibar wanakatishwa tamaa na baadhi ya wanasiasa na maamuzi yao, hivyo wanaamua kuachana na mambo ya kufatilia Siasa!

Niwakumbushe tu ndugu zangu, sukari tunayokorogea Hot beverage ni siasa, mafuta tunayoweka kwenye automobile ni siasa, beer na condom tunazotumia ni siasa!

Tusiache, tuendelee kujadili SIASA, siasa ni maisha.
 
Kwani umelazimishwa kufungua na kusoma!

Kinachoshangaza zaidi umepata mpaka muda wa kutoa maoni kwenye bandiko lefu la hovyo, propaganda na kipumbavu! Sasa hapa nani ni mpumbavu zaidi!
Wewe ni 🍑🍑🍑🍑🍑🍑🍑.

Unajaza public forum your stupidity just for the sake of money
 
Kwa hiyo wakati Zitto anakuwa Mbunge kwa miaka 15, nguvu za CCM za kuiba kura hazikuwepo au miaka hiyo CCM haikuiba kura?

Bila kupinga bandiko lako namba moja maana lina ukweli mwingi tu. Huwa simuamini Zito na sintokaa nimuamini, ila Zito ushindi alioshinda kwa support ya ccm ni baadhi ya kuhitilafiana na cdm. Kabla ya hapo alishinda kwa ushawishi wake binafsi au cdm.

Usitake kuchanganya ukweli na uongo wakati ukweli tunaujua. Kabla ya Magufuli CCM ilikuwa inaiba kura, lakini baada ya Magufuli kuwa rais, anatumia madaraka yake vibaya kushurutisha CCM watangazwe washindi. Jitahidi kutofautisha wizi wa kura na matumizi mabaya ya madaraka.
 
Kwa kifupi wapinzani wengi walikuwa wanashinda audha kwa kuachiwa nafasi na ccm au mpasuko wa ccm kuelekea uchaguzi mkuu..hata lowasa 2015 alipata kura nyingi sababu ya mpasuko ndani ya ccm.

Nani asiyejua kuwa msigwa, lema, sugu na kuna bulaya walipita sababu ya mipasuko na wagombea wa ccm kupita kwa rushwa pasipokukubalika..

Hata jimbo la mtama 2015 nape alitaka kupoteza sababu ya mpasuko..safari hii wakiwa na umoja kapita bila kupingwa.

Kilichotokea kwenye uchaguzi huu tumekiona, haukuwa uchaguzi, bali ni maagizo ya rais kuwa nani atangazwe mshindi, usitake kujifanya eti ccm walikuwa wanashindwa kwa sababu ya mpasuko.
 
Uliiba wewe na sio CCM,
Huwezi shindana na mtu hana miguu kisha umwibie,
Chadema ni nyumbu ambao ukiwaonyesha mto wa maji wanatumbukia woye bila kujua urefu wa mto na mamba kiasi gani wamo.

Kama mmeibiwa basi hata nyie mngefikisha hata milioni 8 hapo ungeweza kulalama, uzidiwe milioni 10 kisha useme umeibiwa?
Nyumbu mna shida sana.

Kwa taarifa yako hata wapiga kura hawakufika hiyo 10m huko vituoni.
 
Back
Top Bottom