Je, Zitto Kabwe alijisahau na kuanza kuung'ata mkono unaomlisha?

Je, Zitto Kabwe alijisahau na kuanza kuung'ata mkono unaomlisha?

Hakuna kitu cha hovyo na kibaya kama kusoma bandiko la lefu la hovyo, propaganda na la kipumbavu halafu asubuhi asubuhi.

Halafu unakuta hili jamaa ni zee lenye mke na watoto.
Kibaya zaidi unakuta katika hao watoto wake wewe ni mmoja wapo tena first born.
 
Hamjawahi kuheshimu Sanduku la Kura nyie.
Chama kilichotoka kwenye ushawishi wa hoja, mpaka kutegemea vyombo vya dola na taasisi zake ili kipate matokeo ni aibu sana.
 
Kilichotokea kwenye uchaguzi huu tumekiona, haukuwa uchaguzi, bali ni maagizo ya rais kuwa nani atangazwe mshindi, usitake kujifanya eti ccm walikuwa wanashindwa kwa sababu ya mpasuko.
Tunaweza kusema pia kuwa kilichotokea uchaguzi huu kinaonesha kuwa nafasi ambazo walizokuwa wanashinda wapinzani huko nyuma ccm walikuwa wanawaachia tu.
 
na huo ndio ubavu wenyewe. Baada ya vita watu huangalia ushindi na si jinsi gani ushindi ulipatikana. Tukubali tukatae CCM ndio imeshika dola na tukiendelea kuichekea itatawala mpaka vitukuu vyetu.
Sasa hivi muda wa kupimishana mabavu umepita maana CCM itashinda tu kwa njia zake zizijuazo zenyewe.
Wa kuitoa CCM madarakani sio wanasiasa kama kina Zitto maana wote wana bei yao, wakilipwa wanaufyata.
Atakaekuja kuitoa CCM madarakani ni mlalahoi wa chini kabisa asiekuwa na jina wala cheo, maana huyo ndio muhanga hasa wa siasa mbovu za CCM zikisaidiwa na hao wanaojiita wapinzani.
Sio wazungu tena ni walalahoi?
 
Jibu ni ndiyo Mimi niliwahi kuandika humu kwamba Kati ya wanasiasa wa nchi hii Zitto ni mchumia tumbo namba moja. Kwamba alikuwa anapiga makelele kwa sababu mianya ya kupiga hela aliyozoea wakati wa serikali ya Kikwete ilikuwa imezibwa.
Zitto kwenye siasa ni "kinyago kilichochongwa na CCM".
 
Mwami Zitto ni one man show, hata wadhifa wake kwenye chama ni KIONGOZI WA CHAMA, ni zaidi ya Mwenyekiti wa Chama.

Zitto ni survival wa siasa za Bongo kwa kipindi kirefu mbeleni.
Zitto amekuwa survival wa siasa nchini sio kwa uwezo wake bali kwa uwezo wa CCM!
 
Kama kweli CCM wanajiona wana ubavu, ilikuaje wanaiba kura kijinga tena mchana kweupe? Nadhani CCM hawana nguvu yeyote, zito amewachapa asubuhi tu na wala hawajashinda.

CCM hawana nguvu then CCM hao hao wamechukua jimbo? Sentence yako inajikanganya.

Asiye na nguvu hawezi kuchukua jimbo. Mwenye nguvu ndo mshindi siku zote mahala popote.
 
Seifu alitamba kwa hasira safari hii Basi yatosha imetosha alipotupiwa mnofu kaona anatosha.
Wazikumbuke pia hata familia zilizomwaga damu Ili wao washibe japo hata kifuta machozi Ili maridhiano yawe na amani. ACT ni sawa na CUF kwisha habari yake.
 
Mwami Zitto ni one man show, hata wadhifa wake kwenye chama ni KIONGOZI WA CHAMA, ni zaidi ya Mwenyekiti wa Chama.
Lakini kubwa ya yote Zitto hana upande,na hiyo ndio siri ya mafanikio yake.
Ndio maana aliungana na Lissu wa Chadema kususia nafasi ya viti maalum vya Chadema akisisitiza Chadema ni sister party, lakini akaja kukubali ACT kuingia serikali ya Mseto Zanzibar.
Huyo Mwami haoni aibu kubadirisha mtizamo au msimamo wake kwa kipindi kifupi,yaliyomkuta Membe yanafurahisha.Membe hakutegemea Zitto atamkana mchana kweupe kuwa sio mgombea wa ACT,bali Lissu wa Chadema tena katikati ya kampeni.
Zitto ni survival wa siasa za Bongo kwa kipindi kirefu mbeleni.

Mkigoma yeyeto usimuamini mbele ya njaa.mwami ni copy na paste
 
Hamjawahi kuheshimu Sanduku la Kura nyie.
Chama kilichotoka kwenye ushawishi wa hoja, mpaka kutegemea vyombo vya dola na taasisi zake ili kipate matokeo ni aibu sana.
Kama chama hakikushawishi wewe haina maana kuwa hakiwashawishi na wengine!

Wizi wa kura ni maneno ambayo sio mageni kwa sababu yamesemwa tokea mwaka 1995!
 
Hakuna kitu cha hovyo na kibaya kama kusoma bandiko la lefu la hovyo, propaganda na la kipumbavu halafu asubuhi asubuhi.

Halafu unakuta hili jamaa ni zee lenye mke na watoto.
Hahahahahahahaahaahaha
 
Maelezo marefu hayana kichwa wala miguu , hivi ccm kutumia dola , usalama wa taifa kushinda ubunge , urais na udiwani nchi nzima Ni jambo la kujivunia ?
Ulitaka CCM wahuzunike wakati malengo makuu ya chama cha siasa makini ni kushika dola!
 
Back
Top Bottom