TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

Kufuta kwake uchaguzi alisababisha watu wasio na hatia kupoteza maisha yao hasa kisiwani Pemba, historia itaendelea kumwandika hivyo na familia yake wataishi na tag hiyo, why he went so low katika maamuzi yake ili kuilinda ccm,na make things .more craze eti naye alichukua form ya kuomba Urais thr ccm!
 
Alizawadiwa mjengo wa Maana sana Kisaki ng'ambo ya reli baada ya alichokifanya 2015.

Mzee aliishia maisha kama ya digidigi, alikua anatoka usiku kwa kuotea otea wala hakuna mwanakijiji aliekua na time nae, ila hakuwahi kujiamini au maybe aliekewa masharti namna ya kuishi...

Lakini alikua vizuri upande wa ujasiriamali, tulinunua tilapia kutoka kwenye mabwawa yake. Tutamkumbuka.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) aliyefuta uchaguzi 2015 na kupata umaarufu mkubwa, Jecha Salim Jecha leo amefariki Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na mwili wake utapelekwa Zanzibar kwa maziko.

Jecha Salim Jecha alipata umaarufu mwaka 2015 baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar. Zaidi soma Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Mwaka 2020, Jecha Salim Jecha alichukua fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), jambo ambalo lilizua utata ukizingatia mwaka 2015 alikuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar yenye dhamana ya kusimamia chaguzi zote kisiwani humo. Zaidi soma Zanzibar 2020 - Namba 14: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar. Arejesha fomu hiyo

Mola amsamehe makosa yake alipoteleza.

View attachment 2691725
Jecha Salim Jecha enzi za uhai wake​
Duh....mola amsamehe heh..
 
Watawala wasiotenda haki waelewe maisha haya yanapita tu. umepewa Maisha ya miaka michache hapa dunia itumie vizuri kutenda haki kwa wananchi waliokuchagua otherwise cheo chako kitakuwa laana na si baraka na vilio vya wananchi na haki zao vitakulilia na kukuandama hadi kaburini.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) aliyefuta uchaguzi 2015 na kupata umaarufu mkubwa, Jecha Salim Jecha leo amefariki Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na mwili wake utapelekwa Zanzibar kwa maziko.

Jecha Salim Jecha alipata umaarufu mwaka 2015 baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar. Zaidi soma Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Aprili 17, 2018 Salim Jecha Salim aling'atuka rasmi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kuanzia Mei 4, 2013. Zaidi soma Hatimaye 'mtemi' Jecha Salim Jecha ang'atuka

Mwaka 2020, Jecha Salim Jecha alichukua fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), jambo ambalo lilizua utata ukizingatia mwaka 2015 alikuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar yenye dhamana ya kusimamia chaguzi zote kisiwani humo. Zaidi soma Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar

Mola amsamehe makosa yake alipoteleza.

View attachment 2691725
Jecha Salim Jecha enzi za uhai wake​
Mungu katimiza wajibu wake
 
Waliosaini hii tuendelee na sala
 

Attachments

  • 6E479063-BC4C-484C-8DC9-05B77B33955B.jpeg
    6E479063-BC4C-484C-8DC9-05B77B33955B.jpeg
    75.7 KB · Views: 7
Back
Top Bottom