Jee, duniani kuna nchi inayoendeshwa vibaya zaidi kuliko Tanzania

Hii nchi ni mismanaged,there is no doubt about that.Na hili swala la viongozi kusema ,'' Nchi hii ni ya amani,siyo kama Somalia,siyo kama Libya'',hii ni makosa. Mtu anataka kujikosha kwa kuwachafua watu wengine. Inakuwa kama watu wengine hawana ruhusa kuwa na amani kwa sababu amani ni hati miliki ya Tanzania.
It is interesting to note kwamba siku moja kabla ya milipuko ya mabomu Mbagala,Rais Mwinyi alikuwa anasema,'' Tanzania ni nchi safi kabisa. Badala ya kuzalisha wakimbizi,yenyewe inapokea wakimbizi,inawapa hifadhi wakimbizi.'' Kesho yake Tanzania ilikuwa na wakimbizi elfu kadhaa,wamekwenda Uhuru Stadium. Halafu yule yule Waziri mhusika hakuulizwa swali lolote,badale yake nadhani amekuwa promoted,yupo sasa katika Kamati Kuu ya CCM. Ndiyo haya mambo yanayolete maandamano katika Nchi nyingi duniani. The Governments are not self-regulating themselves,wanasubiri mpaka watu waandamane. Ndiyo maana response to those demonstrations is very sluggish by the international community,kwa sababu those governments are suppossed to regulate themselves.
Marehemu Abdulrahaman Babu alihawai kusema[wakati alipokuwa hayupo Serikalini,wakati alipokuwa anaishi Ulaya na Marekani],kwamba,''Kama Tanzania haina vita, maendeleo yake yako wapi?''

Nimependa mtazamo wako... Lakini vita si suluhusho, tumeona nchi jirani ambazo zipo katika civil wars na they are not improving nor looking forward to improve.... Pia swala lakusema Tanzania ina amani hilo ni kweli kua kuna amani saaana compared na nchi nyingine hata wageni wana acknowledge hilo... Hio ya kusema Mwinyi aliongea na the next day kukawa na milipuko at least haikuwa deliberate kama nchi zingine... Kwanza tuache kujifananisha na nchi zingine kihali na viongozi, nafikiri imefika wakati wa GT kuanza kufananisha wanajamii wa nchi za wenzetu na wanajamii sisi.... Labda walau twaweza pata majibu ya kusuluhisha matatizo at least kama first stage...
 
bahati mbaya sijawahi kufika somalia na kushuhudia hayo mnayoyasema, ila nchi kama lesotho na swaziland pamoja na udogo wake, msumbiji pamoja na uasi na vita vyake vya misituni vya enzi hizo, malawi pamoja na kutawaliwa na raisa wa maisha banda kwa miongo mingi bila demokrasia, etc lakini wanatushinda mbali karibu kwa kila kitu!!

ila jamani kama na sonalia nao wanatuzidi maendeleo yanayoonekana, basi this must be too low for our government!!
 
Nadhani inabidi nifafanue zaidi mada yangu. Nimepigia mfano maisha ya wananchi na si maendeleo mengine ambayo yaelekea wengi hapa, hasa wale wanaofaidi, huona ndiyo maendeleo: kama vile miji, magari nk. Inapokuja katika maisha ya binadamu, mtu, mwanadamu, sijaona nchi binadamu wengi wanaishi maisha duni na ya kudhalilisha kama Bongo. Hii ni pamoja na nchi kama Somalia, Sudan na Chad. Hizi ni nchi nilizozitembelea, na ingawa ni kweli wana matatizo, na mengine hata yanashinda ya Tanzania-vita- ila maisha ya binadamu ni bora maradufu. Hiki ndicho ninachokizungumzia. Kuna watu wengi hapa wanadakia dakia tu bila ya kufahamu mada hii. Ngoja niwape mfano: Sudan, Somalia mtu wa kawaida kabisa anamudu kupikia kwa gesi, na anamudu kuwa na umeme, hadi vijijini. Angalia Tanzania: hata gesi ni ya mtu tajiri na aghalabu anayeishi mjini. Mtungi mmoja wa gesi nakumbuka mwezi Machi kule Moshi ulikuwa unauzwa shs 55,000. Niambie, watu wangapi Tanzania wanaweza kutumia gesi, ambayo, ironically, inatoka Tanzania?
 
Kwa kiasi fulani ninakubaliana na wewe lakini jua nchi zote masikini dunia hii zina matatizo ya kuendeswa kwa kiasi fulani vibaya nyingine zinazidi na nyingine ni bora zaidi. Nchi yeyote yenye vita na misukosuko hiyo imeendeshwa vibaya zaidi ya Tanzania kimtazamo wangu siye bado hatujafikia hapo. Nikitaka kuzitaja ni msururu ni nyingi kimtazamo wango nikipewa uraia wao bora mie nibakie bongo. Kwa mfano tuseme kenya, nimekaa kenya miaka mitatu wakenya wanajisifu sana na nchi yao uchumi mkubwa na majengo na mabarabara mazuri kushinda yetu. Lakini matajiri wakubwa huko ni wahindi na watuwengine kutoka manchi ya nje ndo wanaendeleza huo uchumi. watu wa chini nairobi hawana nafasi wengi wanatembea umbali kama kutoka bunju hadi sinza kwenda kufanya kazi. Nilishawahi kufanya hivyo huko nairobi kuexperiensi hiyo shida kutoka kangemi mpaka industrial area tabu tupu saa yoyote unawezwa gongwa. Yaani hasubui na jioni watu wamejazana pembeni ya barabarani wanatembea kwa masaa kazaa kwenda vibaruani. Alafu kunawale wakenya wanaofanya kazi serikalini na makampuni binafsi na wanalipwa vizuri kidogo, wanajiita mid class bwana hawatumii vidaladala, huko wanaita matatu wao hutumia mabasi special wanayaita shuttles yana sehemu zao pekee za kusimama na saa nyingine wakiwaona watu wa kawaida kandambili tofauti chini wanawapita hawasimami. Hebu niambie wewe kama mtu wa chini utataka ukae hapo au dar angalau utapanda dcm hadi mbagala nauli utakorofishana na konda siku ukikosa kuliko kutembeaa hivyo ukimaliza kazi lol…. Na wakenya wengi wanatamani kuishi bongo wawe na hela au hawana hivyo ndo nilivyoona miye. Hata kukiwa na uchaguzi huko wakenya karibia wengi ambao hawapo kwenye siasa huja bongo. Uganda ndo usiseme kabisaa M7 yupo hapo toka enzi za idi amini ubabe ubabe tuu. Bora siye CCM wanapeyana miaka kumi anaingia mwingine na wapinzani wetu hawapigwi mabomu na kufungwa jela tunasikiaga hoja zao mpaka wanapochoka. Kwa kiasi fulani uhuru wetu unatufanya tuweze kuishi na amani jamani msitake machafuko.
 
Ni kweli kabisa;si ndiyo kichwa cha mwendawazimu hiki au hamlijui hilo!
 
Mahali popote duniani ukikuta kuna migongano ndani ya chama tawala, ujue chama hicho kimeshindwa kuuonoza nchi na kimepoteza umaarufu, amani inayohubiriwa na wanasiasa fulani ni kiini macho.

Nafikiri Tanzania inaongoza kwa ujambazi afrika mashariki, vyombo vya dola kuua wananchi wake, rushwa, ufisadi, vifo vya ajali kuanzia magari mpaka migodi, uporaji wa ardhi ya wazawa na kuwapa wageni kwa jina la uwekezaji n.k.

Kuna mpango mahususi wa viongozi kurithisha watoto wao uongozi au watoto wao kuingilia maamuzi ya serikali au ya kisiasa

Bunge kugeuzwa kuwa bunge la chama tawala

Nchi inapokuwa na matajiri wachache na waliojipenyeza kwenye chama tawala kulinda maslai yao, huku mwananchi wa kawaida hata hata uhakika wa mlo mmoja kwa siku

Kuna nabii alisema Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu
 
Dalili ya mvua ni mawingu

Mahali popote duniani ukikuta kuna migongano ndani ya chama tawala, ujue chama hicho kimeshindwa kuongoza au kusimamia serikali yake na hupoteza umaarufu, hivyo hukipata ya mfa maji.

Amani inayohubiriwa na wanasiasa fulani ni kiini macho kiinachotumika kama mtaji wa kutapeli waTanzania.

Nafikiri Tanzania inaongoza kwa ujambazi afrika mashariki, vyombo vya dola kuua wananchi wake, rushwa, ufisadi, vifo vya ajali kuanzia magari mpaka migodi, uporaji wa ardhi ya wazawa na kuwapa wageni kwa jina la uwekezaji

Kuna mpango mahususi wa viongozi kurithisha watoto wao uongozi au watoto wao kuingilia maamuzi ya serikali au ya kisiasa

Bunge kugeuzwa kuwa bunge la wabunge wa chama tawala kusimamia maslahi yao na chama chao, na si maslahi ya wananchi waliowachagua
au ya taifa

Nchi inapokuwa na matajiri wachache na waliojipenyeza kwenye chama tawala kulinda maslai yao, huku mwananchi wa kawaida hata uhakika wa mlo mmoja kwa siku

Kuna nabii alisema Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu, Manabii waliotangulia walisema kuna kiama, nakweli kinkuja!
 
Kweli mkuu tulikuwa vijana hadi tunazeeka nchi wameishikilia tu!! Vijana taifa la Kesho!! Kesho itafika lini? Ila tusikimbie tuwachachafye hadi watupe nchi yetu. Ni yetu sote sio ya mtu fulani!
sasa si mpaka upewe hiyo nafasi ya kuijenga hiyo nchi.
 
Nchi ambayo kila kiongozi ana statistcs zake kuhusu kukua kwa uchumi na kupungua kwa umaskini. Inategemea anaongea na kinanani at that time.
 
Nadhani inabidi nifafanue zaidi mada yangu. Nimepigia mfano maisha ya wananchi na si maendeleo mengine ambayo yaelekea wengi hapa, hasa wale wanaofaidi, huona ndiyo maendeleo: kama vile miji, magari nk. Inapokuja katika maisha ya binadamu, mtu, mwanadamu, sijaona nchi binadamu wengi wanaishi maisha duni na ya kudhalilisha kama Bongo. Hii ni pamoja na nchi kama Somalia, Sudan na Chad. Hizi ni nchi nilizozitembelea, na ingawa ni kweli wana matatizo, na mengine hata yanashinda ya Tanzania-vita- ila maisha ya binadamu ni bora maradufu. Hiki ndicho ninachokizungumzia. Kuna watu wengi hapa wanadakia dakia tu bila ya kufahamu mada hii. Ngoja niwape mfano: Sudan, Somalia mtu wa kawaida kabisa anamudu kupikia kwa gesi, na anamudu kuwa na umeme, hadi vijijini. Angalia Tanzania: hata gesi ni ya mtu tajiri na aghalabu anayeishi mjini. Mtungi mmoja wa gesi nakumbuka mwezi Machi kule Moshi ulikuwa unauzwa shs 55,000. Niambie, watu wangapi Tanzania wanaweza kutumia gesi, ambayo, ironically, inatoka Tanzania?

Hapo penye nyekundu.......nina uhakika hujawahi fika nchi hizo.......ungefika au hata kuongea na mtu awaye yote toka huko au kutembelea huko.... usingetamka hayo....... kuna nchi wanaishi maisha ambayo ni ya kukatisha matumaini kabisa......ni sawa uko kwenye death row, acha kusema hivyo ndugu yangu.... hata hapo karibu tu kenya kuna maeneo watu walisha poteza matumaini kabisa.... ukienda nchi ya mali (bamako)...hali ni mbaya.....

Lakini.... sibishii kama kuna uongozi mbovu....lakini hali si kama unavyoikuza katika akili yako... kwa Tanzania marekebisho ambayo yanahitajika ni kufanya watu wote watii sheria zilizopo....nadhani tutapiga hatua..
 
Kwa kiasi fulani ninakubaliana na wewe lakini jua nchi zote masikini dunia hii zina matatizo ya kuendeswa kwa kiasi fulani vibaya nyingine zinazidi na nyingine ni bora zaidi. Nchi yeyote yenye vita na misukosuko hiyo imeendeshwa vibaya zaidi ya Tanzania kimtazamo wangu siye bado hatujafikia hapo. Nikitaka kuzitaja ni msururu ni nyingi kimtazamo wango nikipewa uraia wao bora mie nibakie bongo. Kwa mfano tuseme kenya, nimekaa kenya miaka mitatu wakenya wanajisifu sana na nchi yao uchumi mkubwa na majengo na mabarabara mazuri kushinda yetu. Lakini matajiri wakubwa huko ni wahindi na watuwengine kutoka manchi ya nje ndo wanaendeleza huo uchumi. watu wa chini nairobi hawana nafasi wengi wanatembea umbali kama kutoka bunju hadi sinza kwenda kufanya kazi. Nilishawahi kufanya hivyo huko nairobi kuexperiensi hiyo shida kutoka kangemi mpaka industrial area tabu tupu saa yoyote unawezwa gongwa. Yaani hasubui na jioni watu wamejazana pembeni ya barabarani wanatembea kwa masaa kazaa kwenda vibaruani. Alafu kunawale wakenya wanaofanya kazi serikalini na makampuni binafsi na wanalipwa vizuri kidogo, wanajiita mid class bwana hawatumii vidaladala, huko wanaita matatu wao hutumia mabasi special wanayaita shuttles yana sehemu zao pekee za kusimama na saa nyingine wakiwaona watu wa kawaida kandambili tofauti chini wanawapita hawasimami. Hebu niambie wewe kama mtu wa chini utataka ukae hapo au dar angalau utapanda dcm hadi mbagala nauli utakorofishana na konda siku ukikosa kuliko kutembeaa hivyo ukimaliza kazi lol…. Na wakenya wengi wanatamani kuishi bongo wawe na hela au hawana hivyo ndo nilivyoona miye. Hata kukiwa na uchaguzi huko wakenya karibia wengi ambao hawapo kwenye siasa huja bongo. Uganda ndo usiseme kabisaa M7 yupo hapo toka enzi za idi amini ubabe ubabe tuu. Bora siye CCM wanapeyana miaka kumi anaingia mwingine na wapinzani wetu hawapigwi mabomu na kufungwa jela tunasikiaga hoja zao mpaka wanapochoka. Kwa kiasi fulani uhuru wetu unatufanya tuweze kuishi na amani jamani msitake machafuko.

Boss tuongee ukweli, huwezi kutembea Kutoka Kangemi hadi Industrial Area ya Nairobi unadanganya watu hapa ili upate tu thanks na Likes, lakini in the real sense of things you dont have a clue in what you are talking about.
Alafu hio ya shuttles, hapa Kenya mtu yeyote anaweza kupanda gari la abiria ili mradi ana nauli yake. Kenya ni nchi ya ubepari na hakuna anayekunyima chochote kama una pesa, thats a fact.

Be truthfull, dont try to get points by lying to people in Jamii Forums, have a honest day.
 
Nawapongeza wote waliochangia mada hii kwa undani na uelewa mkubwa. Sasa ni dhahiri kabisa kwamba Tz maendeleo yake ni yale ya juzi ileee. Kila kukicha ni afadhali ya jana kwa kila kigezo. Haya tumeyabaini sasa watanzania milioni 43 twende Kenya, Uganda, Somalia au Afrika ya kusini? Jibu ni hapana. Maadam ugonjwa umejulikana tuutafutie dawa.

Huu ni wakati muafaka wa kuhamisha fikra zetu kwenye kuainisha yale makosa yote ya awamu zote ili tuyatafutuye dawa ili awamu ya sasa na zile zijazo zipate mahali pa kujipatia mawazo yatakayoleta maendeleo. Tusiishiye kulalama tu bila kutoa mapendekezo. Hapa JF itakuwa 'an ideas shopping forum' juu ya jambo hili na itakuwa juu juu kabisa.

Ninayo mawazo kidogo ya kuanzia.

1. Rural electrification: Fedha zote za EPA, za Madini inayoporwa na mali zingine zinazo fisidiwa zingeingizwa kwenye mpango huu natumaini hata fedha za kuzagaa zinazoshawishi kufisidiwa zisingelikuwepo. Umeme huu unaweza kuwa wa Jua, Upepo, maji ya mito midogo vijijini km Ndolage hospital (Kagera) na Bumbuli hospital (Lushoto). Kwa mpango maaluma vifaa vya mifumo hii ya umeme viinaweza kupungua bei na kuwezekana kwa kila mwananchi kama ilivyo kwa simu za mkononi. Wakiwa na umeme huo ndiyo na vingine vingi vitawezekana kama kuchaji simu, Simu itawezesha upatikanaji wa habari hata za bei za mazao na kuwawezesha kuuza mazao yao kwa faida. Huu utakuwa ukombozi kwa walio wengi. Watawala wakiona wazo kama hili anaweza kulifanyia kazi na tukawa tumesaidia Tanzania ikalike.

2. Micro-Irrigation schemes: Ukame umetuandama nchini. Lakini Kila alipo mtanzania kunachanzo cha maji hata kama kidogo. Umwagiliaji ufukiriwe kuanzia kumwagilia mche mmoja wa Sukumawiki, miche mitano ya nyanya, Mche mmoja wa makakala (passion fruits) robo eka ya mahindi mabichi, ekari moja ya vitunguu nk. Alimuradi dhana hii ya umwagiliaji iingizwe kwenye sera za nchi na isimamiwe. Kila mtu amwagilie kwa kufuatana na kiwango cha maji anachoweza kukipata. Hiyo asilimia 80% inayojiita wakulima ikifanya hivi mazao tutatafuta kwa kuyapeleka na haponjia za kupatia pesa zitakuwa nyoofu na za uhakika kwani utegemezi mkongwe wa mvua utapunguwa.

3. Matumizi sahihi ya nguvukazi: Kwenye familia nyingi nguvu-kazi, kama rasilimali, haitumiki kibiashara. Utakuta kinamama ndiyo wanafanya kazi sana huku wanaume na vijana wao wakiranda-randa tu wakisubiri wakati wa maakuli wawahi mezani. Utaratibu mzuri ukiwekwa nguvukazi yote ya Taifa ikitumika kibiashara naamini Taifa liatakwamuka kwenye umaskini na hata kusogea mbele katika viwango vya Ki-Mataifa.

4. Viwanda: Kuwa na sera ya kusindika kila zao tunalozalisha ili kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani. Hapa hatutavuna pesa nyingi tu bali pia tutaongeza ajira na vijana hawatakimbilia mijini. Pia mazao ya mkulima yatakuwa na bei la uhakika kwani yatanunuliwa na viwanda vya hapa nchini. Ni rahisi kwa viwanda kutafuta masoko ndani na hata nje ya nchi.

5. Miundombinu vijijini hasa barabara:

6. n.k.

Wana JF naomba yuongeze listi hii isaidiye kuboresha utawala Tz iboreke siyo iboeshe.

Asanteni.
 
Hapa kuna tatizo kubwa saana la kimtazamo. Nini kipimo cha nchi kuendeshwa vibaya? Tunazengumzia uchumi, siasa na jamii au tunazungumzia nini? Kila kimoja wapo kinapimika kwa tafiti. Zipo Index nyingi zinazoweza kutuonyesha ukweli wa haya maoni. Mtu akienda Somalia au Chad na hata Sudani sina hakika kama anafikia kule vijijini na hata hapo mjini sidhani kama anafikia eneo linalofanana na Manzese. Ukienda sehem fulani si rahisi ukapata taarifa za watu au husika kwa usahihi. Kuna factors nyingi saana zinaweza kusababisha usione mambo mengine. Hivi nani amekwenda Equatorial Guinea au hata nchi nyingine kule west Africa km Gambia etc.
Tukitoa hoja, zitakuwa na maana kama tutaweka kando itikadi vinginevyo hazitakuwa conclusive. Hiyo ya rushwa, jaribuni kupitia transparency International na taasisi nyingine muone.
With the little exposure I have in Western and developing countries, we are still the best. Kuna nchi rais hatukanwi kama hapa. Tusijidanganye, ni kweli kuna changamoto nyingi saana lakini hatujaoza na kuwa wa mwisho.
 
Naanzisha maudhui haya kwa minajili ya kuwafungua macho watu wengi ambao hawajapata nafasi ya kutembea, na ambao siku zote wanalishwa propaganda za watawala. Kwamba nchi ina amani, mshikamano bla bla bla.Zamani walikuwa wanatoa mifano ya South Afrika, Angola, Namibia n.k. jinsi mtu mweusi anavokandamizwa huko na kuwa Watanzania wako huru na inapasa kujivunia nchi yao.Ila mapambano yalipogeuka kuwa ya uchumi wakawa hoja hizo hawanazo. Sasa nadhani hoja moja tu wanayo, nayo ni ile ya amani. Hii pia inatafunwa siku hadi siku kutokana na kupungua mno kwa migogoro Afrika.Katika matembezi yangu, na kusema kweli nimetembelea nchi ambazo zilikuwa katika vita tangu 70 au 80s, kama Chad,Sudan hata Somalia. Ila kitu kimoja ambacho Tanzania ni tofauti kabisa, ni jinsi maisha ya raia wengi yalivyo duni na mabaya. Kwa hili, hata Somalia ina afadhali. Bila shaka, ni uongozi mbaya, tangu uhuru, ndio ilioifanya Tanzania kufikia hapa, ingawaje ina utajiri mkubwa. Kama mtu ana jina la nchi yeyote duniani ambayo raia wake wengi wanaishi maisha duni, ya kudhalilishwa na watawala, kuliko Tanzania....aitaje.
Mkuu Tanzania ina mafanikio makubwa sana tangu uhuru ulipopatikana. Ni vyema ku-recognize kwanza hayo mafanikio kabla hujaanza kutoa shutuma za governance shortcomings ulizozitoa. Angalia jinsi ambavyo Serikali imeboresha huduma za kijamii kama vile Afya, Barabara n.k. Angalia Idadi ya vyuo Vikuu vilivyo hivi sasa ukilinganisha na hali ilivyokuwa wakati wa Uhuru. Angalia jinsi ambavyo Elimu ya Sekondari ilivyosogezwa kwa Wananchi hivi sasa. Ni kweli kwamba kuna mapungufu kama vile kutokuwepo kwa walimu, wahadhiri na madaktari wa kutosha pamoja na mishahara ya kuvutia, lakini ni vyema uka-admit hizo jitihada zilizofanyika. Angalia muda unaotumika hivi sasa kufika Mwanza kwa Basi ukitoka Dar es Salaam na Ulinganishe na kipindi unachokizungumzia. Angalia budget ya Serikali inayoelekezwa katika maeneo ya huduma za jamii kwa sasa (in real terms) ukilinganisha na Wakati wa Uhuru. Linganisha Ada anayolipa mwanafunzi wa Day Shule ya Sekondari ya Serikali (20,000) na katika Shule kama hizo za Binafsi halafu utoe conclusion. Mkuu, Mchambuzi Mzuri wa mambo anaangalia both sides of the coin. Na unapokuwa unafanya "Trend Analysis" unapaswa kuangalia kila Eneo lilikuwaje kipindi cha Nyuma na sasa likoje. Otherwise you will end up with a biased conclusion which will not give any constructive guidance.
 
Nakubaliana na mleta hoja, ni kweli nchi yetu imekuwa mismanaged sana.
Ukichukua umri wetu km taifa huru, ukalinganisha na raslimali tulizonazo, ukaoanisha na kiwango chetu cha maendeleo, utaona ni kweli tunastahili kuwa mbali zaidi ya hapa tulipo.
 
Mkuu Tanzania ina mafanikio makubwa sana tangu uhuru ulipopatikana. Ni vyema ku-recognize kwanza hayo mafanikio kabla hujaanza kutoa shutuma za governance shortcomings ulizozitoa. Angalia jinsi ambavyo Serikali imeboresha huduma za kijamii kama vile Afya, Barabara n.k. Angalia Idadi ya vyuo Vikuu vilivyo hivi sasa ukilinganisha na hali ilivyokuwa wakati wa Uhuru. Angalia jinsi ambavyo Elimu ya Sekondari ilivyosogezwa kwa Wananchi hivi sasa. Ni kweli kwamba kuna mapungufu kama vile kutokuwepo kwa walimu, wahadhiri na madaktari wa kutosha pamoja na mishahara ya kuvutia, lakini ni vyema uka-admit hizo jitihada zilizofanyika. Angalia muda unaotumika hivi sasa kufika Mwanza kwa Basi ukitoka Dar es Salaam na Ulinganishe na kipindi unachokizungumzia. Angalia budget ya Serikali inayoelekezwa katika maeneo ya huduma za jamii kwa sasa (in real terms) ukilinganisha na Wakati wa Uhuru. Linganisha Ada anayolipa mwanafunzi wa Day Shule ya Sekondari ya Serikali (20,000) na katika Shule kama hizo za Binafsi halafu utoe conclusion. Mkuu, Mchambuzi Mzuri wa mambo anaangalia both sides of the coin. Na unapokuwa unafanya "Trend Analysis" unapaswa kuangalia kila Eneo lilikuwaje kipindi cha Nyuma na sasa likoje. Otherwise you will end up with a biased conclusion which will not give any constructive guidance.

MKUU
Pole saana, kama wenzetu walikuwa wanafikiria hivyo sidhani hata hiyo computer unayotumia leo ungekuwa nayo, Ni vema ukatoka kidogo uangalie na mataifa mengine wanafanya nini, kwa huu mtazamo bado tunasafari ndefu saana
 
Kwa kiasi fulani ninakubaliana na wewe lakini jua nchi zote masikini dunia hii zina matatizo ya kuendeswa kwa kiasi fulani vibaya nyingine zinazidi na nyingine ni bora zaidi. Nchi yeyote yenye vita na misukosuko hiyo imeendeshwa vibaya zaidi ya Tanzania kimtazamo wangu siye bado hatujafikia hapo. Nikitaka kuzitaja ni msururu ni nyingi kimtazamo wango nikipewa uraia wao bora mie nibakie bongo. Kwa mfano tuseme kenya, nimekaa kenya miaka mitatu wakenya wanajisifu sana na nchi yao uchumi mkubwa na majengo na mabarabara mazuri kushinda yetu. Lakini matajiri wakubwa huko ni wahindi na watuwengine kutoka manchi ya nje ndo wanaendeleza huo uchumi. watu wa chini nairobi hawana nafasi wengi wanatembea umbali kama kutoka bunju hadi sinza kwenda kufanya kazi. Nilishawahi kufanya hivyo huko nairobi kuexperiensi hiyo shida kutoka kangemi mpaka industrial area tabu tupu saa yoyote unawezwa gongwa. Yaani hasubui na jioni watu wamejazana pembeni ya barabarani wanatembea kwa masaa kazaa kwenda vibaruani. Alafu kunawale wakenya wanaofanya kazi serikalini na makampuni binafsi na wanalipwa vizuri kidogo, wanajiita mid class bwana hawatumii vidaladala, huko wanaita matatu wao hutumia mabasi special wanayaita shuttles yana sehemu zao pekee za kusimama na saa nyingine wakiwaona watu wa kawaida kandambili tofauti chini wanawapita hawasimami. Hebu niambie wewe kama mtu wa chini utataka ukae hapo au dar angalau utapanda dcm hadi mbagala nauli utakorofishana na konda siku ukikosa kuliko kutembeaa hivyo ukimaliza kazi lol…. Na wakenya wengi wanatamani kuishi bongo wawe na hela au hawana hivyo ndo nilivyoona miye. Hata kukiwa na uchaguzi huko wakenya karibia wengi ambao hawapo kwenye siasa huja bongo. Uganda ndo usiseme kabisaa M7 yupo hapo toka enzi za idi amini ubabe ubabe tuu. Bora siye CCM wanapeyana miaka kumi anaingia mwingine na wapinzani wetu hawapigwi mabomu na kufungwa jela tunasikiaga hoja zao mpaka wanapochoka. Kwa kiasi fulani uhuru wetu unatufanya tuweze kuishi na amani jamani msitake machafuko.

Conclusion yako tu umeharibu kila kitu. Jenga hoja upya mkuu
 
Mkuu Tanzania ina mafanikio makubwa sana tangu uhuru ulipopatikana. Ni vyema ku-recognize kwanza hayo mafanikio kabla hujaanza kutoa shutuma za governance shortcomings ulizozitoa. Angalia jinsi ambavyo Serikali imeboresha huduma za kijamii kama vile Afya, Barabara n.k. Angalia Idadi ya vyuo Vikuu vilivyo hivi sasa ukilinganisha na hali ilivyokuwa wakati wa Uhuru. Angalia jinsi ambavyo Elimu ya Sekondari ilivyosogezwa kwa Wananchi hivi sasa. Ni kweli kwamba kuna mapungufu kama vile kutokuwepo kwa walimu, wahadhiri na madaktari wa kutosha pamoja na mishahara ya kuvutia, lakini ni vyema uka-admit hizo jitihada zilizofanyika. Angalia muda unaotumika hivi sasa kufika Mwanza kwa Basi ukitoka Dar es Salaam na Ulinganishe na kipindi unachokizungumzia. Angalia budget ya Serikali inayoelekezwa katika maeneo ya huduma za jamii kwa sasa (in real terms) ukilinganisha na Wakati wa Uhuru. Linganisha Ada anayolipa mwanafunzi wa Day Shule ya Sekondari ya Serikali (20,000) na katika Shule kama hizo za Binafsi halafu utoe conclusion. Mkuu, Mchambuzi Mzuri wa mambo anaangalia both sides of the coin. Na unapokuwa unafanya "Trend Analysis" unapaswa kuangalia kila Eneo lilikuwaje kipindi cha Nyuma na sasa likoje. Otherwise you will end up with a biased conclusion which will not give any constructive guidance.

Mkuu bado sana, hawastahili pongezi yoyote bado
Unaongelea
1 vyuo vikuu-vingapi katika vilivyopo ni vya serikali? Ni mazingira yapi wanafunzi wake wanasomea? Nini ni majaliwa ya wahitimu wa vyuo hivyo?

2 shule za sekondari- hapa hata siongezi comment, wewe mwenyewe umeacknowledge mapungufu lundo yaliyopo. Na udogo wa karo uisemayo the so called alfu 20 haina mantiki kama mwanafunzi huyu huyu unakuja kumpa mzigo wa karo kubwa (kwa kumpatia asilimia pungufu ya mikopo ya ada za chuo) alioshindwa kuubeba katika elimu ya sekondari

3 afya-what a joke.
4 budget-kwa lipi la kuisifia kama haileti nafuu yoyote ya maisha kwetu wananchi?
5 barabara-kwa utajiri wa maliasiri zilizopo nchini inashangaza ati baada ya miaka 50 ya uhuru bado kuna mikoa haijaunganishwa kwa barabara za uhakika mfano mwanza-tabora; tabora-kigoma; tabora-singida; tabora-mbeya etc
 
Naanzisha maudhui haya kwa minajili ya kuwafungua macho watu wengi ambao hawajapata nafasi ya kutembea, na ambao siku zote wanalishwa propaganda za watawala. Kwamba nchi ina amani, mshikamano bla bla bla.

Zamani walikuwa wanatoa mifano ya South Afrika, Angola, Namibia n.k. jinsi mtu mweusi anavokandamizwa huko na kuwa Watanzania wako huru na inapasa kujivunia nchi yao.

Ila mapambano yalipogeuka kuwa ya uchumi wakawa hoja hizo hawanazo. Sasa nadhani hoja moja tu wanayo, nayo ni ile ya amani. Hii pia inatafunwa siku hadi siku kutokana na kupungua mno kwa migogoro Afrika.

Katika matembezi yangu, na kusema kweli nimetembelea nchi ambazo zilikuwa katika vita tangu 70 au 80s, kama Chad,Sudan hata Somalia. Ila kitu kimoja ambacho Tanzania ni tofauti kabisa, ni jinsi maisha ya raia wengi yalivyo duni na mabaya. Kwa hili, hata Somalia ina afadhali. Bila shaka, ni uongozi mbaya, tangu uhuru, ndio ilioifanya Tanzania kufikia hapa, ingawaje ina utajiri mkubwa.

Kama mtu ana jina la nchi yeyote duniani ambayo raia wake wengi wanaishi maisha duni, ya kudhalilishwa na watawala, kuliko Tanzania....aitaje.

My reading of history convinces me that most bad government results from too much government. – Thomas Jefferson
 
Back
Top Bottom