Asili ya TISS ( Usalama wa Taifa) pamoja na mambo mengine ni CCM. Wanaosema TISS asili yake ni Special Branch ya zama kabla ya CCM kuundwa wanaupotosha ukweli.
Baada ya kuundwa kwa CCM, vyombo vyote vya dola viliwekwa chini ya hatamu za CCM. Kwa ivo ilikuwa huwezi kuajiriwa kwenye vyombo vya dola bila ya kuwa kwanza mwana CCM hasa toka Jumuiya ya Vijana Tanzania (UVT).
Kwa ivo hata Sheria ya Usalama wa Taifa ilipokuja, ilikuta mfumo wa kuwapata watu wa TISS ni kutoka ndani ya CCM hasa Jumuiya ya Vijana ya chama hicho.
Lakini kutokana na siasa za vyama vingi je hakuna sababu ya kuibadili TISS yenyewe na mfumo wa upatikanaji wa watu wake?
Na jee dhima ya kuwepo kwa TISS katika zama hizi za maendeleo makubwa ya teknolojia itabakia kuwa ile ile kama zama za mfumo wa chama kimoja?
Nani ni adui wa Taifa ashambuliwe ili Taifa liwe salama?