Jeff Lea: Simba hamfiki mbali kwa ulinzi ule

Mpira haupo hivyo, hakuna jinsi ya kuzuia hizo unazoziita kosakosa. Hata Dodoma wangesawazisha iwe 2-2 ingebakia ni matokeo ya mpira. Simba imekosa magoli mengi kwenye mechi ma Tp mazembe, so unaamini ni kwa sababu Mazembe wana beki mbovu? Tungeweza hata kufungwa jana na yangebaki kama matokeo ya mpira. Lakini kuchukua mechi moja ufanye reference ya ujumla na kuja na hitimisho ni uchambuzi uchwara. Rudi nyuma, chukua mechi tano au sita, angalia kama makosa yanajirudia? Tunafungwa magoli ya aina moja? Ndio unaweza kuja na hitimisho kama hilo.
 
Ili goli lifungwe lazima kosa litokee na kosa lazima litoke kwa beki
 
Tanzania kila mwandishi wa habari ni mchambuzi na anajifanya anajua mpira kuliko hata waliosomea football, wewe ujuzi wako ni mambo ya habari, utaalamu wa soka unautoa wapi?
 
Shida yako unataka simba icheze zisiwepo hata kosakosa langoni kwa simba, wale wote uwanjani ni binadamu kuna kuswitch ki akili uwezi ukawa perfect 100% kwenye dk 90. Na hakuna timu duniani itacheza pasiwe na kosa kosa langoni kwake
Naona hatuelewani.
Hapa tunazungumzia makosa kuwa mengi, ama uzembe, kina Ramos, dvb na mabeki wengine nguli duniani nao wanakosea sababu ni binadamu.

Mimi nazungumzia 1. makosa Yale Yale yanayojirudia rudia, 2. Makosa kuwa mengi.

Kufanya mistake kwa Adam Adam tofauti na kina al ahl huko. Makosa 7 goli 3-5, huku makosa ma5 goli 0-2. Utanielewa tukikutana na strikers wasiotaka masihara, km tukiendelea kufanya hizi mistakes bado tuna hali ngumu huko

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Hatuzuii kosa kosa, tunapunguza makosa chief.

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Sawa lakini unguli wa Jeff Lea ni upi ni kocha kwa kusomea? Je, ana utaalamu upi ambao una manlaka hayo ya kusema hivyo?
Neno nguli limetumika vibaya,Jofrey Leo nilimfundisha Green Acres hajafikia hadhi hiyo. Hapa labda angekuwa Leaky Abdalah
 
Uchambuzi wa mtu ambaye amezaliwa anapenda mpira na kutusomea habari za michezo na hajawahi kucheza mpira unaotambuliwa hawezi niumiza kichwa kumsikiliza, ndio maana Skysports wanawaalika wachambuzi unakuta akina Jamie Carragher, Garry Nevile, Rio Ferdinand nk. Watu waliocheza mpira wakikwambia kitu unajua anaongea from experience lakini wachambuzi wa bongo wa kuangalia upepo hamna kitu..
 
Mimi ni shabiki wa Simba na humu ninajulikana hivyo,ila hapa lazima nikiri Jeff yuko sahihi.

Sisemi kwamba Simba haipaswi kufungwa,HAPANA!Ila kinachonikera kama Mwanasimba ni Simba yangu kufungwa aina ile ile ya magoli; free headers huku mabeki wetu wamesimama tu wakimwangalia adui akipaa angani na kufunga. Hii haijatokea mara moja,hivi karibuni imetokea dhidi ya Al Hilaly na Dodoma City.Lakini huko nyuma imetokea mara nyingi zaidi.Hivi mabeki wetu wameshindwa kabisa kufanyia kazi dosari hiyo? (Heko kwa Onyango maana yeye walau yuko vizuri kwenye eneo hilo ila wengine Mmmmmmh!)

Kinachomwogopesha Jeff Lea na mimi ni kwamba makosa ya kijirudia rudia ni mabaya sana,maana ni rahisi maadui zako wa baadaye kusoma consistency ya makosa yako na kuyatumia kukuadhibu. Na Champions League ina watu wanaojua kupiga vichwa hatari na kusoma madhaifu ya muda mrefu ya mpinzani.

Halafu hawa wachambuzi na wasio wachambuzi tusiwaone kuwa ni maadui.Kama wewe huwa hupendi kuambiwa makosa yako ili ujirekebishe basi utakuwa na matatizo. Na kumbukeni ni wachambuzi hawa hawa waliipa tahadhari Simba kumchunga sana Perfect Chikwende kwenye first leg kule Zimbabwe, nadhani wachezaji wa Simba yangu waliwabeza wachambuzi (kama ambavyo baadhi yetu humu tunambeza Jeff) na matokeo waliyaona. Na ni hawa hawa waliitonya Simba kuhusu madhara ya Luis Miquissone akiwa na UD Songo yake,nani alijali?
 
Mchambuzi akitaka 'kutrendi' inabidi aiponde Simba
 
Ahahahaha uko sahihi lakini umekuja kuharibu hapa mwisho, hakuna mchambuzi yeyote hapa bongo alimjua Luis kabla ya kumuona hapa kwa mkapa dhidi ya simba, hata Chikwende wamemuona baada ya kuifunga simba.
Wachambuzi wa bongo ni wa matukio sio watu wa kufuatilia jambo kabla halijatokea. Hao wote simba ilivyowasajili walianza kusema simba inamsajili mchezaji kwa sababu ya performance ya mechi moja.
 
Reactions: BRN
Hivi ukisoma hii comment yako na kilichotokea leo uwanjani na ukalinganisha na alichosema huyo sijui jef leha unatoka na hitimisho lipi mkuu?
 
Hivi ukisoma hii comment yako na kilichotokea leo uwanjani na ukalinganisha na alichosema huyo sijui jef leha unatoka na hitimisho lipi mkuu?
Kama umetazama mpira kosa la Simba ni mid field ilichoka kipindi cha pili.
 
Kusema Simba haina tatizo la beki ni kujidanganya.
 
Kama umetazama mpira kosa la Simba ni mid field ilichoka kipindi cha pili.
Simba tuna kikosi imara na kipana tunaweza kucheza mechi mbili kwa wakati mmoja. Tayari tumeshachukua kombe moja liko kabatini Simba Super Cup
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…