Jeff Lea: Simba hamfiki mbali kwa ulinzi ule

Jeff Lea: Simba hamfiki mbali kwa ulinzi ule

Ndugu yangu, huu mpira wenu was takwimu una changamoto sehemu, we unaongelea karuhusu goli chache, vipi zile kosa kosa, tunakoswa koswa saana kwa uzembe, takwimu zisikuongopee, game ya jana chupuchupu iishe droo km sio manula kudaka kile kichwa cha mchezaji was dodoma jiji, game ingekuwa 2-2 ile, vipi game na platnum yule jamaa aliyebaki yeye na goli angefunga? Mchezo ungebadilika siku zile

Sisi hatutaki haya makosa ya kizembe tusubiri adui nae akosee ndio tuwe salama, hata msimu wa kuvuka makundi mpaka tunaingia makundi tulikuwa na rekodi nzuri kitakwimu km ulivyotoa ww, kipi kilitusibu wapinzanj walipoweza kubadili makosa yetu kuwa magoli?? Mwendo wa 5, 5.

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
Mpira haupo hivyo, hakuna jinsi ya kuzuia hizo unazoziita kosakosa. Hata Dodoma wangesawazisha iwe 2-2 ingebakia ni matokeo ya mpira. Simba imekosa magoli mengi kwenye mechi ma Tp mazembe, so unaamini ni kwa sababu Mazembe wana beki mbovu? Tungeweza hata kufungwa jana na yangebaki kama matokeo ya mpira. Lakini kuchukua mechi moja ufanye reference ya ujumla na kuja na hitimisho ni uchambuzi uchwara. Rudi nyuma, chukua mechi tano au sita, angalia kama makosa yanajirudia? Tunafungwa magoli ya aina moja? Ndio unaweza kuja na hitimisho kama hilo.
 
Tanzania kila mwandishi wa habari ni mchambuzi na anajifanya anajua mpira kuliko hata waliosomea football, wewe ujuzi wako ni mambo ya habari, utaalamu wa soka unautoa wapi?
 
Shida yako unataka simba icheze zisiwepo hata kosakosa langoni kwa simba, wale wote uwanjani ni binadamu kuna kuswitch ki akili uwezi ukawa perfect 100% kwenye dk 90. Na hakuna timu duniani itacheza pasiwe na kosa kosa langoni kwake
Naona hatuelewani.
Hapa tunazungumzia makosa kuwa mengi, ama uzembe, kina Ramos, dvb na mabeki wengine nguli duniani nao wanakosea sababu ni binadamu.

Mimi nazungumzia 1. makosa Yale Yale yanayojirudia rudia, 2. Makosa kuwa mengi.

Kufanya mistake kwa Adam Adam tofauti na kina al ahl huko. Makosa 7 goli 3-5, huku makosa ma5 goli 0-2. Utanielewa tukikutana na strikers wasiotaka masihara, km tukiendelea kufanya hizi mistakes bado tuna hali ngumu huko

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Mpila haupo hivyo, hakuna jinsi ya kuzuia hizo unazoziita kosakosa. Hata dodoma wangesawazisha iwe 2-2 ingebakia ni matokeo ya mpila. Simba imekosa magoli mengi kwenye mechi ma Tp mazembe, so unaamini ni kwa sababu mazembe wana beki mbovu? Tungeweza hata kufungwa jana na yangebaki kama matokeo ya mpila. lakini kuchukua mechi moja ufanye reference ya ujumla na kuja na hitimisho ni uchambuzi uchwara. Rudi nyuma, chukua mechi tano au sita, angalia kama makosa yanajirudia? Tunafungwa magoli ya aina moja? Ndio unaweza kuja na hitimisho kama hilo.
Hatuzuii kosa kosa, tunapunguza makosa chief.

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Sawa lakini unguli wa Jeff Lea ni upi ni kocha kwa kusomea? Je, ana utaalamu upi ambao una manlaka hayo ya kusema hivyo?
Neno nguli limetumika vibaya,Jofrey Leo nilimfundisha Green Acres hajafikia hadhi hiyo. Hapa labda angekuwa Leaky Abdalah
 
Akiongea leo asubuhi katika kipindi cha michezo cha Efm mchambuzi nguli wa mpira Jeff Lea asema kwa safu ile ya ulinzi wa Simba dhidi ya Dodoma Jiji jana, mabeki wao wameonesha udhaifu mkubwa sana hivyo kama watakutana na timu yenye washambuliaji wazuri basi hawatafiki mbali katika ligi ya mabingwa Afrika.

Mimi namuunga mkono kwa 100% kwa mbaaaali naona mtu akienda kuchezea goli 5 kwa kila mechi ya ugenini.

Msijenge chuki, fanyieni kazi mapungufu yenu Simba
Uchambuzi wa mtu ambaye amezaliwa anapenda mpira na kutusomea habari za michezo na hajawahi kucheza mpira unaotambuliwa hawezi niumiza kichwa kumsikiliza, ndio maana Skysports wanawaalika wachambuzi unakuta akina Jamie Carragher, Garry Nevile, Rio Ferdinand nk. Watu waliocheza mpira wakikwambia kitu unajua anaongea from experience lakini wachambuzi wa bongo wa kuangalia upepo hamna kitu..
 
Mimi ni shabiki wa Simba na humu ninajulikana hivyo,ila hapa lazima nikiri Jeff yuko sahihi.

Sisemi kwamba Simba haipaswi kufungwa,HAPANA!Ila kinachonikera kama Mwanasimba ni Simba yangu kufungwa aina ile ile ya magoli; free headers huku mabeki wetu wamesimama tu wakimwangalia adui akipaa angani na kufunga. Hii haijatokea mara moja,hivi karibuni imetokea dhidi ya Al Hilaly na Dodoma City.Lakini huko nyuma imetokea mara nyingi zaidi.Hivi mabeki wetu wameshindwa kabisa kufanyia kazi dosari hiyo? (Heko kwa Onyango maana yeye walau yuko vizuri kwenye eneo hilo ila wengine Mmmmmmh!)

Kinachomwogopesha Jeff Lea na mimi ni kwamba makosa ya kijirudia rudia ni mabaya sana,maana ni rahisi maadui zako wa baadaye kusoma consistency ya makosa yako na kuyatumia kukuadhibu. Na Champions League ina watu wanaojua kupiga vichwa hatari na kusoma madhaifu ya muda mrefu ya mpinzani.

Halafu hawa wachambuzi na wasio wachambuzi tusiwaone kuwa ni maadui.Kama wewe huwa hupendi kuambiwa makosa yako ili ujirekebishe basi utakuwa na matatizo. Na kumbukeni ni wachambuzi hawa hawa waliipa tahadhari Simba kumchunga sana Perfect Chikwende kwenye first leg kule Zimbabwe, nadhani wachezaji wa Simba yangu waliwabeza wachambuzi (kama ambavyo baadhi yetu humu tunambeza Jeff) na matokeo waliyaona. Na ni hawa hawa waliitonya Simba kuhusu madhara ya Luis Miquissone akiwa na UD Songo yake,nani alijali?
 
Mchambuzi akitaka 'kutrendi' inabidi aiponde Simba
 
Ahahahaha uko sahihi lakini umekuja kuharibu hapa mwisho, hakuna mchambuzi yeyote hapa bongo alimjua Luis kabla ya kumuona hapa kwa mkapa dhidi ya simba, hata Chikwende wamemuona baada ya kuifunga simba.
Wachambuzi wa bongo ni wa matukio sio watu wa kufuatilia jambo kabla halijatokea. Hao wote simba ilivyowasajili walianza kusema simba inamsajili mchezaji kwa sababu ya performance ya mechi moja.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Watanzania wajinga sana! Sijui muliumbwa na udongo gani? Jeff Leah ni nani hata kama reference? He is just a nut! So far Simba ndio timu iliyo fungwa magoli machache sana kwenye VPL, Timu bora kama TP Mazembe haja funga goli na walipata wakati mgumu sana kuipenya ile defense ya Simba. Halafu mjinga mmoja anafanya hitimisho kwa kutumia mchezo mmoja! Shame! A hilal pamoja na ubora wao walipata goli moja tu kwa Simba hii.
Hivi ukisoma hii comment yako na kilichotokea leo uwanjani na ukalinganisha na alichosema huyo sijui jef leha unatoka na hitimisho lipi mkuu?
 
Hivi ukisoma hii comment yako na kilichotokea leo uwanjani na ukalinganisha na alichosema huyo sijui jef leha unatoka na hitimisho lipi mkuu?
Kama umetazama mpira kosa la Simba ni mid field ilichoka kipindi cha pili.
 
Hii Ndio shida ya wachambuzi wa bongo, ni watu wa matukio. Ukuta wa simba umecheza mechi nne za mtoano imeruhusu goli moja tu za mashindano ya CAF championship.

Afu Leo unaongea kama umejisahulisha eti kwa ukuta ule wa simba itaenda kupigwa goli nyingi.
Simba ina mabeki 5 wa kati, hapo sioni point yoyote ya msingi
Kusema Simba haina tatizo la beki ni kujidanganya.
 
Kama umetazama mpira kosa la Simba ni mid field ilichoka kipindi cha pili.
Simba tuna kikosi imara na kipana tunaweza kucheza mechi mbili kwa wakati mmoja. Tayari tumeshachukua kombe moja liko kabatini Simba Super Cup
 
Back
Top Bottom