Jelly Silaa amaliza ubunge 2025 kwa maumivu, aswekwa ndani akidaiwa kutaka kupindua matokeo.

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Miongoni mwa mawaziri wote wa Baraza la Mawaziri la 2020-2025, Jerry William Silaa peke yake ndiye waziri aliyeanguka ubunge hivyo kupoteza sifa ya kuteueliwa kuwa waziri tena kwenye baraza lijalo.
Jerry Silaa aligombea ubunge 2025-2030 kwenye Jimbo la Ukonga, Ilala jijini Dar es Salaam kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akichuana na wagombea wa vyama vingine, akiwemo Bakari Shingo wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT- Wazalendo) ambaye ndiye aliyembwaga kwa kishindo na kuibuka kidedea.
Mbaya zaidi, inadaiwa wakati wa zoezi la kuhesabu kura, Silaa alizua taharuki wakati wa kutangazwa matokeo akidai yeye ndiye mshindi hali iliyosababishwa akamatwe na maafande wa polisi na kupelekwa mahabusu ya Central kwa siku kadhaa.
"Wakati wa zoezi la kuhesabu kura za ubunge, Silaa alitaka 'kupindua matokeo' kwa mpinzani wake wa ACT- Wazalendo hivyo akawekwa chini la ulinzi wa polisi na kufikishwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar (Central)," kilisema chanzo hicho.
Wakati Silaa akiugulia maumivu hayo, mpinzani wake, Bakari Shingo 'anashona suti' za kwenda kuapia kwenye Bunge la 13 Mkutano wa Kwanza mjini Dodoma, Novemba 11, 2025.

NI 'LAANA' ZA WATIA NIA WENZAKE AU WAPIGA KURA WAMEAMUA?

Katika Mitandao ya Kijamii, watu wanasema kitendo cha Jerry Silaa ambaye alikuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kushindwa kutetea jimbo lake mbele ya Bakari Shingo, aliyekuwa mgombea ubunge wa ACT katika Jimbo la Ukonga, anakuwa waziri PEKEE aliyeangushwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 ngazi ya ubunge.
Baadhi ya wakazi wa jimbo hilo wameonesha kufurahia kitendo cha Silaa 'kurudi kijiweni' wakisema 'kweli Mola hujibu maombi ya waja wake.'
Watia nia jimboni humo kupitia CCM walikuwa; William Mwila, Alex Msama, Jerry Silaa, Rajabu Nyangasa na Alfred Tukiko.

DALILI ZA SILAA KUTOKUBALIKA JIMBO LA UKONGA ZILIANZA KITAMBO

Kuanzia mwaka 2021 kuelekea 2025, baadhi ya wakazi wa Ukonga walikuwa wakimlalamikia Silaa kupitia mitandao ya kijamii kuwa, hajali ubovu wa barabara jimboni mwake, haonekani jimboni na mambo mengine huku wengine wakitangulia mbele kusema hawatampa kura za 'Ndiyo Mzee' kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Ahadi ambayo imetimia.

ZIARA YA MCHENGERWA JIMBONI UKONGA 2025, SILAA ALISHINDWA KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI?

Wakati wa kuelekea kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi, Silaa alilalamikiwa na baadhi ya watia nia wenzake walidai kuwa, alitumia ziara ya aliyekuwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa jimboni mwake kujifanyia kampeni kipindi ambacho siyo cha kampeni.

ILIVYOKUWA MITANDAONI

Katika mitandao ya kijamii, baadhi ya watia nia hao walidai hivi;
"Tunashangaa mwenzetu (Jerry Silaa), mbali na kuanza kampeni mapema, jambo ambalo ni kosa la jinai, pia anaonekana kutumia mamlaka yake ya uwaziri huku akiwahusisha viongozi wa juu.
"Mfano, kutumia jina la rais kutaka kutelekeza ahadi ambazo zilimshinda kwa kipindi chote cha miaka mitano aliyokuwa mbunge.
"Mfano mwingine, Jumamosi ya Julai 19, 2025, Silaa aliandamana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa katika kukagua ujenzi wa barabara kutoka Banana hadi Msongola ambapo alidai kuwa, eti alimuomba mheshimiwa rais. Naye akamtuma Waziri Mchengerwa kwenda kuona mradi husika."
"Mambo yaliyomshinda kuyatimiza kwa kipindi cha miaka mitano tena akiwa mbunge na waziri, atawezaje kuyatekeleza kwa miezi michache iliyobaki tena akiwa si mbunge ukiachia mbali kuwa anaweza asipitishwe sababu mojawapo ikiwamo ni kuanza kampeni kabla ya wakati?" Alihoji mtia nia mmoja wa jimbo hilo.
Akazidi kuhoji; kwa nini Silaa alikaa kimya hadi kipindi ambacho kisheria muda wake kama mbunge umeisha ndipo aje kujitafutia umaarufu kwenye mradi ambao ulimshinda wakati akiwa madarakani kama mbunge?
"Je, ni sahihi Silaa kuendelea kujifanya anafanya kazi za kibunge wakati bunge limeishavunjwa? Je, hii ni haki mbali ya kuwa kinyume cha sheria na taratibu?"
Hata hivyo, licha ya mbunge huyo aliyemaliza muda wake kusema alimuomba mheshimiwa rais amtume waziri wake, kakini Mchengerwa alipopata muda wa kuongea, alisema:
“Nimeshuhudia namna gani wananchi (jimboni humo) wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu...”
Kwa mujibu wa maneno ya Waziri Mchengerwa ina maana waziri mwenzake na aliyekuwa mwakilishi wa jimbo (Silaa) aliweza kuwaacha wananchi wateseke kwa muda mrefu, atafanya miujiza gani ya kuwaondolea mateso wakati yeye ndiyo sehemu ya mateso hayo?
Ikahojiwa; Je Silaa anamuongopea nani kwenye jambo ambalo liko wazi kuwa alishindwa vibaya sana kuwaletea wananchi wa Ukonga maendeleo kama alivyowaahidi wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2020 ambazo anazirudia tena wakati watu wanajua kila kitu?
Kuna msemo unasema; “nidanganye mara moja, aibu kwako. Nidanganye mara ya pili, aibu kwangu.”
Katika kuumwa na nyoka mara mbili kwenye shimo moja wa kulaumiwa siyo nyoka, bali ni yule aliyeng’atwa mara mbili kwenye shimo moja.
Kwa vile CCM imeonnesha ukomavu mkubwa kisiasa na viwango vikubwa vya utendaji wa haki, inashauriwa iangalie rafu hii anayocheza Silaa hapa Ukonga.
Mtia nia mwingine akasema: "Tunaiomba CCM imzuie Silaa kutumia mamlaka ya uwaziri kufanya kampeni za ubunge kabla ya muda kufika. Kwani, hii si haki mbali na kutaka kumjengea picha mbaya mheshimiwa Rais kuwa anamuunga mkono au hata kampeni zake ambazo zimeanza kabla ya muda.
"Silaa aambiwe kuwa mheshimiwa Rais ni mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye hana mgombea yeyote kwenye jimbo lolote nchini. Hivyo, aache kumuingiza kwenye kampeni zake ambazo zimeanza kabla ya wakati mbali na kuwa kinyume cha sheria na utaratibu wa CCM na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
"Mwisho, tumashauri mheshimiwa Silaa aache kumuingiza mheshimiwa Rais kwenye mambo ya hovyo kama vile kuanza kampeni kabla ya wakati wake. Tunafahamu.
"Mheshimiwa Rais ana majukumu mengi makubwa ya kitaifa. Hivyo, asiingizwe kwenye siasa za majimbo. Cha msingi, abebe mzigo wake mwenyewe. Silaa acha mara moja kucheza rafu unayocheza Ukonga. Yakupasa kutambua kuwa unachafua jina la chama kwa faida binafsi jambo ambalo ni kinyume na sera na taratibu za CCM.
"Uchaguzi ni haki ya kila Mtanzania, hivyo, unapaswa kufanyika kwa haki na kufuata taratibu mojawapo ikiwa ni kusubiri INEC itangaze siku rasmi ya kuanza kampeni kisheria. Je, Silaa, ana uhakika gani kuwa atapitishwa wakati ameanza kuvunja kanuni na taratibu hata kabla ya mchakato kuisha?" Alimaliza mtia nia huyo kwa mara nyingine jimboni hapa.
Pamoja na malalamiko ya watia nia hao, ilipofika wakati wa kura za maoni, jina la Jerry Silaa liliibuka kidedea akiwashinda wenzake saba, akateuliwa na Tume kushindana na wagombea toka upinzani.
Hata hivyo, pengine 'dua' za watia nia hao na 'ahadi' za wananchi za kutomchagua, vilikamilika Oktoba 29, 2025 kwa Bw. Bakari Shingo wa ACT kujizolea kura za 'kishindo cha Wakoma kilichowakimbiza Washami.'
Bakari Shingo anakuwa miongoni mwa wabunge wanne wa Tanzania Bara walioshinda kupitia tiketi ya chama cha Act Wazalendo ambapo kimepata majimbo manne Tanzania Bara ambayo ni Ukonga, Nkasi Kaskazini, Tunduru Kusini na Kigoma Kaskazini.
Screenshot_20251106_000837_Google.jpg
Screenshot_20251106_021746_Google.jpg
 
Bakari Shingo anakuwa miongoni mwa wabunge wanne wa Tanzania Bara walioshinda kupitia tiketi ya chama cha Act Wazalendo ambapo kimepata majimbo manne Tanzania Bara ambayo ni Ukonga, Nkasi Kaskazini, Tunduru Kusini na Kigoma Kaskazini.View attachment 3497813View attachment 3497814
Kifupi kabisa ni kwamba wote wenye vielement vya magufuli hawatakiwi tena yaani hata wale waliosimamishwa na magufuli wakina tulia sijui nani wote hawatakiwi tena.

Watu wanaenda kujenga serikali mtandao hivyo kuanzia sasa kama wewe sio mwanamtandao unawekwa pembeni kabisa.
 
Hajaangushwa, sema SYSTEM haikumtaka...itakuwa alikanyaga sipo...ukiona JIMBO limeenda Upinzani ni Maamuzi tu ya Mwenyekiti wa Chama Chakavu..ila yote haya ya KUNAJISI sanduku la kura mwanzilishi ni Kambale
 
Hakukuwa na uchaguzi
 
Back
Top Bottom