Jemedari Said ni mmoja wa wachambuzi ambao hupaswi kupoteza muda wako kuwasikiliza mwaka 2024

Jemedari Said ni mmoja wa wachambuzi ambao hupaswi kupoteza muda wako kuwasikiliza mwaka 2024

Umechelewa sana hakuna mchambuzi pale, yule hata mimi tu tukiwekwa pamoja mezani tuchambue mechi kiufundi namshinda.yule ni mtopokaji tu akijifichia kwenye misimamo ya kipumbavu
 
Kuna watu sababu yupo nyuma ya Kamera au microphone basi anajiona naye ni mchambuzi. Mchambuz ambaye kiukweli namuheshimu ni Ally Mayai ni mchambuzi mkweli na hana ubaya na timu yoyote licha ya kuwa alichezea Yanga lakini ikifika wakati wa uchambuzi anasema ukweli hata kama tatizo lipo yanga anasema.Nadhani kinachomsaidia ni kuongelea kiufundi zaidi kuliko kishabiki. Sasa huyu Jeme yeye hana sifa hata moja amekalia ushabiki wa ajabu. Ukishakuwa mshabiki hufai kuwa mchambuzi kwenye media, labda vijiweni. Mchambuzi kwenye media unatakiwa kuwa fair kwa maana huna upande wowote unaoshabikia. Jeme yeye amekuwa na tabia kuishambulia Yanga bila kuchambua yeye kila kitu ni kukosoa mpaka unajiuliza hakuna zuri hata moja. Ntamshangaa mtu ambaye anamuamini huyu kuwa ni mchambuzi.
Jemedari yeye anaongeleaga mambo ya nje ya uwanja na huwa haongelei zile dk 90 za uwanjan sasa mnamuitaje mchambuzi?

Mchambuzi ni yule anaongelea mpira zile dk 90 za mechi, anachambua mbinu, udhaifu na vinginevyo mfano mzuri wa mchambuzi hapa bongo ni ambagile
 
Kifupi kusikiliza vpindi vya michezo bongo ni kupoteza muda
 
Muda ni mali, ukiupoteza umepotea siku, nimewahi kufanya kazi ya uandishi wa habari kuanzia mwaka 1998 - 2008 nikiandikia magazeti ya Nipashe na Alasiri na kidooogo sana gazeti la Lete Raha, enzi hizo Alasiri ni gazeti hasa.Kwahiyo naifahamu kazi ya uandishi wa habari.

Vyombo vya habari must speak for the people, sio unaongelea mambo yako binafsi ili kumfurahisha mtu au uonekane kuwa una msimamo fulani, Big No.

Simchukii ila mbali na uandishi wa habari niliokuwa nao, kwa elimu yangu pia ya Political Science and Public Administration which I was conferred at the level of Bachelors degree and as of now pursuing LL.B, nawashauri msipoteze muda kumsikiliza Jemedari Said.

Changamoto anazozieleza huyu mshamba wa kusini zipo katika kila institutions, yeye yuko katika media moja but media hiyo ina matatizo kibao, haina motivation, watumishi wanahama, wengine hawazingati maadili katika magazine, unaendaje kazini na jeans, umenyoa kiduku, watumishi aina ya Dkt Kumbukaa ambao elimu yao ni ya kuunga unga matusi kibao kwenye mitandao ya kijamii lakini wao hawasemi, kwahiyo hiyo media unayofanya kazi inawalipa vzr saaaana nyie mbona mwalalamika mishahara, mbona media yenu ina uchale mwingi sana na watu wamekaa tu kimya.

Uchambuzi wake mimi simsikilizi sana ila namuona sana kwenye page yake ila baada ya kumbaini ni msanii, hana ishu, hana uwezo wa kuchambua namu unfollow kuanzia leo na sisikilizi tena redio anayofanyia kazi yeye.Naanza na huyu.
Alimkomalia Karia siku mbili mfululizo aliposema ligi kuu ilikuwa si lolote si chochote kabla ya ujio wa azam tv.
 
Back
Top Bottom